Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Turkana District Mock-Kiswahili Paper 2 Question Paper

Turkana District Mock-Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



JINA——————————————————————NAMBARI____________________________
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA 2
(UFAHAMU, MUHTASARI, MATUMIZI YA LUGHA, ISIMU JAMII)
JULAI/AGOSTI - 2006
MUDA: SAA 2 ½
WILAYA YA TURKANA BARAZA LA MITIHANI- 2006
Hati Ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari (K.C.S.E.)
102/2
KISWAHILI
KARATASI 2
(UFAHAMU, MUHTASARI, MATUMIZI YA LUGHA, ISIMU JAMII)
MUDA: SAA 2 !/2
Maagizo.
- Jibu maswali yote
- Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa wanastahili kuona kuwa maswali yote yako na hakuna yaliyooachwa.
UFAHAMU(15)
Soma kifungu kufuatacho halafu ujibu maswali uliyoulizwa
Tsunami, tetemeko la ardhi baharini, iliyotokea Desemba mwaka 2004 katika bara la Asia ilikuwa na athari kubwa sana. Watu wasiopungua 170,000 walipoteza maisha yao kutokana na mawimbi yaliyotifuliwa na tsunami hiyo katika Bahari ya Hindi. Madhara na maafa hayo yalitanda hadi maeneo ya mbali kama upwa wa Afrika mashariki ulio na umbali wa takriban kilometa 7,000 kutoka kitovu kikuu cha tsunami hiyo. Janga hili limeibua mjadala kuhusu madhara yanayotokana na nguvu za kimaumbile. Nguvu za kimaumbile zina uwezo wa kuzua majanga yasiyoweza kutarajiwa. Mlima wa volkeno uliotulia unaweza kuvuvumka na kutapakaza zaha ambayo inaweza kuua maelfu ya watu kama ulivyotokea huko nchini Kongo.
Majanga ya kimaumbile huweza kusababisha maafa, misiba na tanzia isiyokuwa na mshabaha. Sio
rahisi kuweza kutasawari akilini kiwango cha madhara ya majanga haya hadi yanapotokea. Baadhi ya majanga ya kimaumbile ni kama vimbunga vya vumbi, zilizala, mafuriko, tufani, radi, ukame na hata moto. Licha ya kuwa binadamu hawana uwezo wa kuzuia kutokea kwake, zipo hatua ambazo zinaweza
kuchukuliwa kwa mfano, yapo maeneo ambako kutokana na historia ni rahisi kujua ni majanga yepi ambayo huweza kuchukuliwa kawa mfano, yapo maeneo ambako kutokana na historia ni rahisi kujua ni majanga yepi ambayo huweza kutokea.Kuna maeneo ambako mafuriko hutokea kila zinaponyesha mvua za mvo. Jamii inayojikuta katika mazingira haya inapaswa kujua ni hatua zipi za kuchukua..Mathalan ujenzi wa matuta, kuhimiza wakazi kusakini katika maeneo ya juu, kuwepo na huduma za dharura za kupambana na maradhi yanayochimbukuna na ungi wa maji na kadhaliki.
Vivyo hivyo na ukame. Ni muhali kuweza kujua ukame utatokea lini. Hata hivyojamii inaweza
kuchukua hatua fulani ambazo zinachangia kwenye ukame kama ukataji holela wa miti. Uchimbaji wa chemchemi ni njia nyingine inayoweza kutumiwa hasa kuhakikisha kuwa taraa ukame utazuka, watu hawataathirika kutokana na kuyakosa maji ya kutumia.
Wataalamu wameafikiana sasa kuwa baada ya tusunami iliyotokea lazima uwepo mfumo madhubuti
wa kuweza kuudodosa mtikisiko wa ardhi ambao hutokea kwa muda kabla ya tetemeko lenyewe.
Kwa njia hii watu wataweza kuonywa mapema na labda hasara kama iliyotokea kupunguzwa.
MASWALI:
1. Ipe taarifa hii kichwa mawafaka. (alama 2)

3
2. Ni nini maana ya tsunami, (alama 2)
3. Ni lipi lililokuwa tokeo kuu la tsunami? (alama 2)
4. Eleza hatua anazoweza kuzichukua binadamu kupambana na majanga ya kimaumbile. (alama 4)
5. Taja methali inayoweza kuufumbata ujumbe wa kifungu hiki. (alama 1)
6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katikakifungu hiki:
a) Kuvuvumka
b) Kutasawari akilini
c) Mvua za mvo
d) Ungi wamaji
e) Zilizala
(alama 5)
2. UFUPISHO (ALAMA 15) SOMA HABARI IFUATAYO KISHA
JIBU MASWALI:
MAADILI
Ikiwa ungewauliza wanahistoria, "Je, maadili ya watu leo ni bora au ni mabaya zaidi kuliko awali?" huenda wengine wakajibu kwamba ni vigumu kulinganisha maadili ya vipindi tofauti tofauti au wengine wakawa na maoni kwamba kila kizazi chapasa kuonwa kulingana na jinsi kilivyo.Hata hivyo, jambo fulani tofauti kabisa na baya sana - kwa kweli lisilo na kifani - lilitukia katika karne ya 20 na lingali linatukia.
Katika miaka ya 1930 visa vya uuaji - kimakusudi na uuaji wa binadamu viliongezeka tena na mwelekeo huu umeendelea kwa zaidi ya nusu karne. Insha moja iliyohusu falsafa za maadili yasema hivi; "Mtu aweza kuona waziwazi kwamba maoni ya jamii kuhusu ngono (mapenzi) na mambo yanayokubalika kiadili yamebadilika sana katika miaka ya 30 hadi 40 iliyopita - zamani jamii ilionyesha waziwazi mambo yanayofaa kiadili, kupitia sheria kali, siku hizi kuna maoni ya kibinafsi nay a uhuru." Kipindi hiki basi ni kisicho na kanuni zozote; mawazo ya kidesturi ya linalofaa na lisilofaa yamepuuzwa hatua kwa hatua. Hali hii imekuwako kwa vizazi viwili.
Wanahistoria na wachanganuzi wengine husema kuwa mabadiliko haya yametokana na kupuuza dunia. Watu wamepewa fursa ya kuchukua msimamo wa maoni tofauti tofauti kujitegemea kwani wamekataa Biblia kuwa chanzo cha pekee cha ukweli. Hivyo, dini, hasa zile za jumuiya ya Wakristo, hazitegemewi kuandaa mwongozo wa kiadili kama zilivyotegemewa sana zamani.
Maendeleo ya haraka ya kitekinolojia na kiuchumi katika jamii mnamo karne ya 20 yamechangia kwa kiasi kikubwa hisia hizi. Hili limeongoza kwenye mfumo wa soko huru unaotegemea mashindano na kuchochewa na ubinafsi. Tokeo Hmekuwa kuongezeka kwa unyama/ukatili na ufisadi. Watu hujifikiria wenyewe na kutosheleza tamaa zao kwa kiwango kikubwa zaidi. Kwa mfano, Wamarekani wengi leo huhofu kuwa tamaa ya pesa imetangulizwa kuliko maadili mengine kama vile watu kustahiana, ufuatiaji wa haki kazini na kushirikiana katika jumuiya zao. Tatizo linalohusu ufuatiaji wa faida miongoni mwa wasimamizi wa biashara ni kwamba mtazamo wao huathiri wengine na kupunguza kiwango cha maadili miongoni mwa watu kwa ujumla.
Jambo jingine kuu linalochangia kuzorota kwa haraka kwa maadili ni utamaduni wa vyombo vya habari.
Watayarishaji wa vipindi vya runinga, wahusika mashuhuri katika sinema,watangazaji - mitindo, waimbaji wa rapu ya magenge ya mitaani na wengine wengi huathiri sana watoto wetu leo. Watu hawa wanaoanzisha mitindo huathiri sana utamaduni wetu na mtazamo wa watoto wetu. Ajabu ni kwamba mara nyingi hawakubali kulaumiwa kwa kueneza maadili yenye kudhuru.
Wazazi wanaochukua madaraka kwa uzito leo wanapambana vikali na utamaduni wa vyombo vya habari ili kubainisha ni nani atakayelea watoto wao na kuwa na uvutano juu yao. Wao wanajua kuwa mambo anayotanguliza mtoto katika maisha yake huweza kuathiriwa hasa na kile anachojifunza kwenye runinga, sinema na redio yenye CD.na hivi karibuni tunaweza kuongeza mtandao wa Internet kwenye orodha hiyo.
Athari za mavutano hayo kwa vijana ni kuwa katika miaka ya hivi karibuni watoto matineja wengi zaidi wamefanya vitendo vikatili na vya ujeuri dhidi ya watoto wengine na hata watu wazima. Kwa mfano, katika nchi moja, kijana mmoja alimuua mamake kwa kumpiga risasi. Madaktari waliweza kuthibitisha kuwa alikuwa ameusikiliza muziki uliotaja kuua kwa mama usiku kucha kabla ya kitendo hicho.
Tukio jingine ni magonjwa ya akili. Profesa mmoja alidokeza kuwa asilimia 15 hadi 20 ya wafungwa wote katika nchi yake ni wagonjwa wa akili. Hawana hisia-mwenzi, wanafikiria sana na hawawezi au hawataki kuelewa dhana ya jema na baya. Kwa mfano, walipoulizwa wangefanya nini ikiwa wangekabiliwa na uamuzi kati ya kuokoa uhai wa mnyama kipenzi chao au wa binadamu mwenzao wasiyemjua, wengi wa vijana walisema wangechagua mnyama huyo.
MASWALI.
a) Kwa maneno 70 - 80, ni mambo gani ambayo yamesababisha kuzorota kwa
maadili katika miaka ya hivi karibuni? (ALAMA 8)
Matayarisho
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
...........................................................................................
Nakala safi
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................


MATUMIZI YA LUGHA
a. Jibu maswali yafuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
(i) masaibu yaliyowapata yaliwafanya wapoteze matumaini. (andika kwa umoja) ( alama 2)
(ii) Ukimnunulia chumvi atakuja kukuzibia ufa (Andika kwa wingi) (alama 2)
b. Zisahihishe sentensi zifuatazo
(i) Ua ya stima itajengwa kando. (alama 1)
(ii) Nilimpatia pesa zake alinidai (alama 2)
(c) Andika sentensi ifuatayo kwa wakati uliopita hali timilifu (i) Alijifunza kuendesha gari.
(alama 2)
(ii) Andika sentensi ifuatayo wakati wa sasa hali ya kuendelea Alikuwa ameenda sokoni. (alama 2)
(d)(i) Kanusha sentensi ifuatayo kwa ukubwa.
Mbwa huyo anapenda kubwekabweka bila sababu yoyote (alama 2)
(ii) Kanusha sentensi ifuatayo.
Kwenda kwake kazini kulimfanya apandishwe cheo (alama 2)
(e) Pambanua mofimu mbalimbali zinazounda maneno yafuatayo.
(i) zilizochomeka (alama 2)
(ii) Mama (alama 2)
(f) Tunga sentensi mbili kuonyesha maana mbili tofauti ya maneno yafuatayo:
(i)Fuo
(ii) Ota
(g) Andika visawe vya maneno yafuatayo
(i) Shaibu …………………………………………………………
(ii) Zaraa …………………………………………………………..
(h) Tumia - enye au - enyewe kukamilisha sentensi zifuatazo.
i) shule —————————shida daima husaidiwa. (ii) Kucheza ————————kulikuwa
kwa kupendeza.
(alama 2)
(i) Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo vikiwa katika hali ya kufanyiza
(i) La
(ii) Nywa
(iii) Fa
(alama 6)
(j) Andika neno moja lenye sauti king'ong'o (alama 1)
(k) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia kielelezo cha mstari.
Samaki huogelea mtoni. (alama 6)
4. ISIMU - JAMII ( ALAMA 10)
1. Taja na ueleze sifa tano za lugha ya michezoni. (alama 10)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers