Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Marejeleo Lesson Plans: Grade 3 Kiswahili Activities
Class: Grade 3
Subject: Kiswahili
Level: Primary School
Category: Grade 3 Kiswahili Activities Lesson Plans
Document Type: Pdf and Docx
Number of Pages:
Price: KES: 50
Views: 1368
Downloads: 2
Lesson Plan Summary
Below is a brief overview of some of its content:
MADA: Marejeleo
MADA NDOGO: Msamiati Kusikiliza na kuzungumza Kusoma hadithi Sarufi
MATOKEO MAALUMU YANAYOTARAJIWA:
Mwanafunzi aweze:
• Kuelezea maana ya mazingira, safi na chafu katika hadithi ili kuimarisha ufahamu.
• Kutunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno mazingira, safi na chafu ili kujieleza.
• Kusoma hadithi ya Wanyama wapenda kazi kwa ufasaha na kuyajibu maswali kwa usahihi.
• Kutoa vinyume vya vitenzi na atambue baadhi ya sentensi kwenye hadithi zilizo na vinyume vya vitenzi.
• Kuchangamkia usomaji bora.
MASWALI DADISI:
Je, wewe unapenda kufanya kazi gani ukiwa nyumbani?
Je, maana ya maneno mazingira, chafu na safi ni gani?
Je, Unafikiria hadithi ya wanyama wapenda kazi inahusu nini?
UMILISI WA KIMSINGI UNAOKUZWA: Mawasiliano na ushirikiano, hamu ya ujifunzaji
MAADILI: Uwajibikaji
UHUSIANO NA MASWALA, MTAMBUKO: Masilahi ya wanyama
NYENZO:
Tusome mwongozo wa mwalimu 3 uk. 1-2
Tusome kitabu cha Mwanafunzi 3 uk. 1-2
Chati, Madaftari na Kalamu, Vifaa halisi
UTANGULIZI
Darasani katika vikundi/Kibinafsi
Utangulizi
Wanafunzi waimbe wimbo kuhusu wanyama pori
Je, wewe unapenda kufanya kazi gani ukiwa nyumbani?
UTARATIBU WA SOMO
Hatua ya 1: Msamiati
Je, maana ya maneno mazingira, chafu na safi ni gani?
Mwalimu afunze msamiati mazingira, Safi na chafu na ayatungie sentensi sahihi
Hatua ya 2: Kusoma matini
Kabla ya kusoma
Mwalimu amwongoze Mwanafunzi kujadili picha
Je, unafikiria hadithi ya wanyama wapenda kazi inahusu nini?
Mwanafunzi atoe utabiri wake kwa wenzake
Mwalimu aeleze jinsi na umuhimu wa kuyaweka mazingira yetu safi.
Wakati wa kusoma
Waongoze wanafunzi kusoma hadithi ya wanyama wapenda kazi kwa ufasaha
Baada ya kusoma
Kuhakiki utabiri uliotolewa
Mwalimu awaelekeze na kuwaongoza wanafunzi katika kujibu maswali ya ufahamu
Hatua ya 3: Sarufi
Mwalimu amwelekeze Mwanafunzi kutambua sentensi zilizo na kinyume cha vitenzi katika hadithi kuziandika
HITIMISHO
Mwalimu asahihishe kazi ya Mwanafunzi. Mwalimu ampe Mwanafunzi nafasi ya kuuliza maswali ya ufafanuzi
Mwalimu ampe Mwanafunzi kazi ya ziada
MUHTASARI
Mwalimu asisitize umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kuyaweka safi
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji: Mwanafunzi atunge sentensi akitumia msamiati uliofunzwa.
Maoni
......................
Below is the document preview. Purchase to access the complete document.
More Lesson Plans
View all lesson plans