Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Sokoni Lesson Plans: Grade 3 Kiswahili Activities

Class: Grade 3

Subject: Kiswahili

Level: Primary School

Category: Grade 3 Kiswahili Activities Lesson Plans

Document Type: Pdf and Docx

Number of Pages:

Price: KES: 50            

Views: 1733     Downloads: 4

Lesson Plan Summary

Below is a brief overview of its content:

MADA: Sokoni

MADA NDOGO: Msamiati Kusoma- Ramani dhana. Sarufi

MATOKEO MAALUMU YANAYOTARAJIWA:
Mwanafunzi aweze:
• Kuelezea maana ya msamiati hufurika, madalali na vibanda katika hadithi ili kuimarisha ufahamu.
• Kutunga sentensi sahihi Kusoma kichwa cha hadithi, kujadili picha, kutoa utabiri, kusoma hadithi, kuhakiki utabiri kuyajibu maswali kwa usahihi kwa kutumia ramani dhana.
• Atambue matumizi ya vihusishi nje ya na ndani ya.
• Athamini uwepo na umuhimu wa soko.

MASWALI DADISI:
Sokoni huuzwa nini?
Watu gani hupatikana sokoni?

UMILISI WA KIMSINGI UNAOKUZWA: Mawasiliano na ushirikiano, hamu ya ujifunzaji

MAADILI: Uwajibikaji

UHUSIANO NA MASWALA, MTAMBUKO: Elimu ya fedha

NYENZO:
Tusome mwongozo wa mwalimu 3 uk. 72-73
Tusome kitabu cha Mwanafunzi 3 uk. 56-57
Madaftari na Kalamu, chati, picha ya soko
Mpangilio wa somo
Darasani katika vikundi/Kibinafsi

UTANGULIZI
Sokoni huuzwa nini?

UTARATIBU WA SOMO
Hatua ya 1: Msamiati
Mwalimu amwongoze Mwanafunzi kueleza maana ya msamiati hufurika, madalali na vibanda

Hatua ya 2: Kusoma
Mwalimu amwongoze Mwanafunzi Kusoma kichwa cha hadithi,
Kujadili picha, kutoa utabiri, kusoma hadithi,
Kuhakiki utabiri kuyajibu maswali kwa usahihi kwa kutumia ramani dhana.

Hatua ya 3: Sarufi
Mwalimu amwongoze Mwanafunzi kutoa mifano ya sentensi zenye vihusishi
Kueleza matumizi ya vihusishi ndani ya, nje ya

HITIMISHO
Mwalimu asahihishe kazi ya Mwanafunzi. Mwalimu ampe Mwanafunzi nafasi ya kuuliza maswali ya ufafanuzi
Mwalimu ampe Mwanafunzi kazi ya ziada

MUHTASARI
Mwalimu asisitize umuhimu wa soko

Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji: Mwanafunzi amweleze mlezi wake kuhusu vitu vinavyopatikana sokoni

Maoni
...........................



Below is the document preview. Purchase to access the complete document.

 

More Lesson Plans


View all lesson plans