Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Karibu darasani Lesson Plans: Grade 1 Kiswahili Activities

Class: Grade 1

Subject: Kiswahili

Level: Primary School

Category: Grade 1 Kiswahili Activities Lesson Plans

Document Type: Pdf and Docx

Number of Pages:

Price: KES: 50            

Views: 1971     Downloads: 6

Lesson Plan Summary

Below is a brief overview of some of its content:

MADA: Karibu darasani

MADA NDOGO: Kuskiliza na kuzungumza (Maamkuzi)

MATOKEO MAALUMU YANAYOTARAJIWA:
Mwanafunzi aweze:
• Kutambua maneno yanayotumiwa katika maamkuzi ili kuimarisha mawasiliano
• Kuamkua na kuitika maamkuzi ili kujenga stadi za kuzungumza
• Kutambua umuhimu wa salamu katika mawasiliano
• Kufurahia kushiriki katika maamkuzi ili kuimarisha ushirikiano.

MASWALI DADISI:
• Tunatumia maneno gani katika salamu?
• Tunatakiwa kusalimiana vipi?
• Kwa nini tunasalimiana?

UMILISI WA KIMSINGI UNAOKUZWA: Mawasiliano na ushirikiano, hamu ya ujifunzaji

MAADILI: Heshima na adabu, upendo

UHUSIANO NA MASWALA, MTAMBUKO: Utangamano wa kijamii

NYENZO:
Tusome mwongozo wa mwalimu 1 uk. 1
Tusome kitabu cha Mwanafunzi 1 uk. 1
Vifaa vya kidijitali kama vipakatalishi, Tabuleti na chati ya watu wakisalimiana

MPANGILIO WA SOMO
Darasani katika vikundi

UTANGULIZI
Wanafunzi waimbe wimbo kuhusu salamu

UTARATIBU WA SOMO
Hatua ya 1: Kuigiza
1. Kutazama na Kujadili picha
Mwalimu amwongoze Mwanafunzi kujadili picha.

2. Kuigiza maamkuzi
• Tunatakiwa kusalimiana vipi?
• Kwa nini tunasalimiana?
Mwalimu aigize maamkuzi pamoja na mmoja wa Wanafunzi
Waongoze Wanafunzi kuigiza maamkuzi wakiwa wawili wawili
Mwalimu aigize maamkuzi ya kimasai.
Waongoze Wanafunzi kuigiza maamkuzi ya kimasai wakiwa wawili.

3. Baada ya kuigiza
Mwalimu awaelekeze na kuwaongoza Wanafunzi katika kujadili umuhimu wa maamkuzi

HITIMISHO
Mwalimu achunguze maigizo ya Mwanafunzi. Mwalimu ampe Mwanafunzi nafasi ya kuuliza maswali ya ufafanuzi. Mwalimu ampe Mwanafunzi kazi ya ziada.

MUHTASARI
Mwalimu asisitize umuhimu wa maamkuzi

Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Mwanafunzi akienda nyumbani aeleze walezi wake umuhimu wa kuamkuana

Maoni
.................................



Below is the document preview. Purchase to access the complete document.

 

More Lesson Plans


View all lesson plans