Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Vyakula Vya kiasili 1 Lesson Plans: Grade 1 Kiswahili Activities
Class: Grade 1
Subject: Kiswahili
Level: Primary School
Category: Grade 1 Kiswahili Activities Lesson Plans
Document Type: Pdf and Docx
Number of Pages:
Price: KES: 50
Views: 12594
Downloads: 31
Lesson Plan Summary
Below is a brief overview of some of its content:
MADA: Vyakula Vya kiasili 1
MADA NDOGO: Kusikiliza na kuzungumza Sauti na majina ya herufi kusoma msamiati Sarufi
MATOKEO MAALUMU YANAYOTARAJIWA:
• Kutambua sauti za herufi zilizofunzwa katika maneno ili kuimarisha mazungumzo
• Kusoma silabi na maneno
• Kujadili maana ya msamiati na kutunga sentensi.
• Kusoma hadithi na kujibu maswali.
• Kueleza matumizi ya –angu na –etu
• Kufurahia kuandika herufi kwa hati nadhifu.
MASWALI DADISI:
Je, ni vyakula vipi vya kiasili unavyovijua?
Unapenda chakula kipi?
UMILISI WA KIMSINGI UNAOKUZWA: Mawasiliano na ushirikiano, hamu ya ujifunzaji
MAADILI: Heshima na adabu, upendo
UHUSIANO NA MASWALA, MTAMBUKO: Utangamano wa kijamii
NYENZO:
Tusome mwongozo wa mwalimu 1 uk. 73
Tusome kitabu cha Mwanafunzi 1 uk. 56-57
Vifaa vya kidijitali, Kadi za herufi, mfuko wa kadi za herufi, chati za herufi
MPANGILIO WA SOMO
Darasani katika vikundi/kibinafsi
UTANGULIZI
Unapenda chakula kipi?
UTARATIBU WA SOMO
Hatua ya 1: Ufahamu wa fonimu
Mwalimu afunze ufahamu wa fonimu sauti /b/
Ufahamu wa herufi b, o, na u
Kusoma silabi. Mwanafunzi asome silabi
Kusoma maneno kutumia silabi- boga, analila, anasema, mboga
Hatua ya 2: Kusoma matini
Kabla ya kusoma
Kufunza maana ya msamiati – boga, mboga
Kusoma na kujadili kichwa cha hadithi Boga tamu
Unaona nini katika picha? Mwalimu amwongoze Mwanafunzi kujadili picha
Mwanafunzi atoe utabiri kwa wenzake
Wakati wa kusoma
Mwalimu awaongoze wanafunzi kusoma hadithi
Baada ya kusoma
Mwalimu awaelekeze na kuwaongoza wanafunzi kuyajibu maswali ya ufahamu
Mwalimu achore jedwali, awaongoze kusoma jedwali na kuunda maneno kutokana na jedwali
Hatua ya 3: Sarufi
Je, unatumia maneno gani kurejelea kitu ni cha nani
Mwalimu afunze Mwanafunzi matumizi ya –angu na –etu.
HITIMISHO: mwalimu ampe Mwanafunzi nafasi kuuliza maswali ya ufafanuzi; Mwalimu ampe Mwanafunzi kazi ya ziada.
MUHTASARI
Mwanafunzi aulize na kujibu maswali
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji
Mwanafunzi aandike herufi hizi: b, B, o mara tano tano katika daftari lake
Maoni
...........................
Below is the document preview. Purchase to access the complete document.
........
More Lesson Plans
View all lesson plans