Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Mwili Wangu 2 Lesson Plans: Grade 1 Kiswahili Activities
Class: Grade 1
Subject: Kiswahili
Level: Primary School
Category: Grade 1 Kiswahili Activities Lesson Plans
Document Type: Pdf and Docx
Number of Pages:
Price: KES: 50
Views: 1560
Downloads: 11
Lesson Plan Summary
Below is a brief overview of some of its content:
MADA: Mwili Wangu 2
MADA NDOGO: Kusikiliza na kuzungumza Sauti na majina ya herufi Kusoma Sarufi msamiati Kusoma
MATOKEO MAALUMU YANAYOTARAJIWA:
• Kutambua sauti za herufi zilizofunzwa katika maneno ili kuimarisha mazungumzo
• Kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma
• Kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusoma
• Kutumia wingi na umoja wa majina
• Kutambua na kutumia msamiati uliotumika katika hadithi
• Kusoma hadithi na kujibu maswali.
MASWALI DADISI:
Unaweza kusoma silabi na maneno yapi?
Je, unajua mbinu zipi za kudumisha usafi wa mwili?
Ni maneno yapi unayajua kwa umoja na wingi?
UMILISI WA KIMSINGI UNAOKUZWA: Mawasiliano na ushirikiano, hamu ya ujifunzaji
MAADILI: Heshima na adabu, upendo
UHUSIANO NA MASWALA, MTAMBUKO: Utangamano wa kijamii, afya
NYENZO:
Tusome mwongozo wa mwalimu 1 uk. 124
Tusome kitabu cha Mwanafunzi 1 uk. 106-107
Vifaa vya kidijitali, Kadi za herufi, mfuko wa kadi za herufi, chati za herufi
MPANGILIO WA SOMO
Darasani katika vikundi/kibinafsi
UTANGULIZI
Unaweza kusoma silabi na maneno yapi?
Marudio kuhusu kipindi kilichotangulia
UTARATIBU WA SOMO
Hatua ya 1: Ufahamu wa fonimu
Mwalimu afunze ufahamu wa fonimu sauti /ch/
Ufahamu wa herufi ch, h na w
Kusoma silabi – che, chi, cho
Kusoma maneno kutumia silabi – msichana, kuchana, chake, kucha
Hatua ya 2: Kusoma matini
Kabla ya kusoma
Kufunza maana ya msamiati – kusugua meno, kuchana nywele, kudumisha
Kusoma na kujadili kichwa cha hadithi- Gacheri ajifunze usafi
Unaona nini katika picha? Mwalimu amwongoze Mwanafunzi kujadili picha
Mwanafunzi atoe utabiri wake
Wakati wa kusoma
Mwalimu awaongoze wanafunzi kusoma hadithi na kuambatanisha picha
Baada ya kusoma
Kuhakiki utabiri
Mwalimu awaongoze wanafunzi kujibu maswali ya ufahamu
Hatua 3: Sarufi
Mwalimu afunze matumizi ya umoja na wingi wa majina na awaelekeze wanafunzi ifuatavyo
HITIMISHO: mwalimu ampe Mwanafunzi nafasi kuuliza maswali ya ufafanuzi; Mwalimu ampe Mwanafunzi kazi ya ziada.
MUHTASARI
Mwalimu atoe muhtasari wa somo
Mapendekezo ya shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji
Waongoze wanafunzi washiriki mchezo wa kuigiza kuhusu usafi wa mwili wakiwa katika vikundi
Maoni
...............................
Below is the document preview. Purchase to access the complete document.
More Lesson Plans
View all lesson plans