Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Karatasi La 2 Question Paper

Kiswahili Karatasi La 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2008



Jina ……………………………………………… Namba yako ………………………………...
Shule ……………………………………………. Sahihi ya mtahiniwa ………………...……..
Tarehe ………………………………………
102/2
KISWAHILI
(UFAHAMU)
Karatasi ya 2
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MTIHANI WA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA BONDO-RARIENDA - 2008
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA – (K.C.S.E.)
102/2
KISWAHILI
(UFAHAMU)
Karatasi ya 2
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MAAGIZO:
Jibu maswali yote
KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE
Swali Upeo Alama
1 15
2 15
3 40
4 10
JUMLA

2
Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
1.
UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
Msemo “Ya kale hayako” unatukuzwa sana na vijana na hata wazee ambao wanathamini usasa. Msemo huu
umetishia kuumeza na kuutema utamaduni wa Mwafrika. Utamsikia kijana akiambiwa na mzazi wake, “Jamani
itabidi ujifunze lugha yako ya mama, hivi hatuwezi kuwasiliana na mababu zako kijijini”. Naye kijana huyu
hujibu, huku macho kayatunga kwenye runinga, kidhibiti mbali mkononi. “Hayo ni yako. Lugha inahitajika
kutumiwa pale mtu anapoishi. Mimi kijijini humo nitaishi lini? Na huyu babu, si anajua Kiingereza?”
Huyu ni mfano mmoja tu unaoonyesha mabadiliko ambayo yamezikumba jamii zetu. Watoto na hata watu wa
umri wa makamo wamerithi desturi mchafukoge ambazo hazijulikani kama ni za Kiafrika au Kizungu. Mitindo ya
mavazi ya kushangaza imezuka. Kuna wale wanaopendelea kutembea mabega wazi. Hawa huvaa vizibau
vilivyoning’inizwa kwenye fito za nyuzi. Kuna baadhi ambao huvaa suruali ndefu ambazo zimening’inia kiasi cha
kuvifanya viuno kuwa kwenye miundi. Huu nao ni usasa ati. Unapouliza unazomewa na kuambiwa umechelewa
kutambua hii ni karne ya ishirini na ngapi.
Tofauti za umri zimeanza kuwa finyu mno siku hizi. Si bura kumpata kijana akimpita mzee kama kwamba
hajamwona. Anangoja mzee amsalimu yeye. Vijana wengine hudiriki kujibizana na wazee wao kama kwamba ni
wa rika moja. Hawawapi wazee fursa ya kuzungumza, badala yake huwakata kauli kila mara wanapozungumza na
kuwaudhi. Anapoulizwa kwa nini anamjibu vibaya mzee huyo, anasema nyakati za ‘kuhubiriwa’ bila kuuliza
maswali zimepita na kuzikwa.
Teknolojia mpya imewapunguzia udhia baadhi ya vijana ambao hawapendi kufanya kazi. Katika baadhi ya
familia, utapata kwamba kuna mashine za kufulia nguo na kupangusia sakafu. Vijana wengi wanaoinuka
hawawezi hata kujifulia nguo. Wale ambao kwao hakuna mashine, wana vijakazi ambao huwafanyia kila kitu.
Lao ni kulala tu na kusoma. Mafunzo ya kazi ambayo vijana walipata siku za mababu yameanza kuzikwa kwenye
kaburi la sahau. Hata katika familia ambazo utapata wazazi wana ari ya kuwafunza wanao umuhimu wa kutenda
kazi za nyumbani, utapata kwamba watoto wenyewe hawazipendi kazi hizi. Wanahiari kucheza michezo ya
kompyuta na kutazama kupigana mierekani na masumbwi katika runinga. Si ajabu kwamba wengi wa vijana
wanakua wakidhani njia ya kutatua migogoro ni kupitia kwa makonde migoto vichwani.
Suala unasaba lilikuwa na umuhimu mkubwa katika siku za kisogoni. Neno ndugu lilikuwa na maana pana katika
jamii ya Mwafrika. Watoto wa ami, mjomba na shangazi walihifadhiana na kulindana kama ndugu. Siku hizi
neno ndugu limejikita tu katika uhusiano wa karibu tu; mtoto wa mama au baba yako. Vijana wengi hawajui hata
mabinamu zao. Jambo hii limewafanya wengine kuoa watu wa ukoo wao bila kujua. Baadhi ya vijana
wamezaliwa na kukulia mijini, hawana wakati wa kutangamana na jamaa zao vijijini. Kwa hivyo, hata inapofika
wakati wa kuoa, hao hukutana na wachumba wao mijini.
Ingawa tunapasa kutambua kuwa wakati umebadilika, ni vyema kuwajibika. Hata pale tunapoiga mitindo ya
kisasa kama vile ya mavazi, tuige kwa tahadhari. Mavazi tunayovaa yasikinzane na maadili ya jamii zetu. Elimu
ya kisasa isiwe kisingizio cha kusahau kitovu chetu. Tukumbuke methali isemayo “Usiache mbachao kwa mswala
upitao”.
(a) Mwandishi amedhamiria kichwa mwafaka cha taarifa hii kuwa ya kale hayako. Eleza.
(alama 2)
(b) Tofauti za umri zimeanza kuwa finyu mno siku hizi. Fafanua kauli hii. (alama 2)
(c ) Mabadiliko yaliyokithiri katika jamii ni kutokana na vijana wasiowajibika. Toa ithibati.
(alama 5)
(d) Eleza chanzo cha mabadiliko ya vijana kulingana na taarifa. (alama 4)
(e) Eleza matumizi ya methali usiache mbachao kwa mswala upitao kulingana na taarifa. (alama 2)
2. MUKHTASARI
Soma taarifa ufuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo
Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa
ajili ya kuchochea ashiki ya kuifanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, video,
magazeti, vitabu, muziki, televisheni, wavuti, DVD, n.k.

3
Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa
sababu imeenea ulimwenguni kote mithili ya moto katika mbuga wakati wa kiangazi. Uenezi umechangiwa na
mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi umetokana na kuimarika kwa vyombo vya teknolojia ya habari
na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali vya picha yamesambaza ponografia
ilivyoanza. Hata hivyo, hubuniwa au kutengenezwa na makundi mbali mbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni
watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza
uchafu huu kwa lengo la ama kuvuruga maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni
lile la wanaoichukulia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la
wanotumia matusi haya kama njia ya kuchuma. Kwa mfano, wanamziki ambao hutumia ponografia kuvutia wateja
na hivyo kuzidisha mauzo yao.
Kushamiri kwa wimbi na uonyeshaji ponografia kuna athari kubwa kwa jamii na hasa watoto. Ingawa watu
wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wanaotazama picha za ngono hupata
matatizo. Lazima ieleweke kuwa kinachoonekana na jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikira au hisia. Picha za
matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama masomo watu
huanza kutafakari mambo machafu.
Vijana wengi ni kama bendera. Hivyo basi huanza kuiga wanayoyaona na kusikia. Hili ni tatizo linalowafanya
kuacha mkondo wa maadili. Kutokana na uchafu huu, watu wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono
mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni mengi. Haya ni pamoja na ukahaba,
utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mimba zisizotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa.
Wengine nao huambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo huwaletea mauti.
Inasemekana kuwa akili za binadamu hunata zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha. Si ajabu vijana
huyadumisha matusi haya katika kumbukumbu zao na kuyasanya sehemu ya maisha yao. Wengi huanza
kuandama tabia mbovu kama ushoga, ubasha na usagaji. Kuna wale ambao huanza kujichua. Kujichua ni hali ya
mwanamke au mwanaume kumaliza haja za kimaumbile bila kufanya mapenzi na mtu mwingine. Ponografia
imechangia pakubwa kuenea kwa haya.
Jambo hili limegeuza mielekeo ya vijana. Wanaiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao.
Halikadhalika, huiga lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono. Yote haya yanapingana na desturi za
Mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kila kukuchapo.
Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama unywaji wa pombe, matumizi ya dawa
za kulevya, uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za kuchochea uchu wa ngono. Mambo haya huwapa vijana tabia za
unyama.
Jambo hatari ni kuwa kuendelea kutazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, yaani huondoa
makali. Hata katika utu uzima, mtu atapoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia.
Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya
yasio na kizuizi.
Jambo la kwanza ni kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi. Kwa namna hii itawezekana
kupunguza mahitaji na uuzaji wa pnografia. Aidha ni vizuri watu wazima wawajibike ile wawalinde hasa vijana
kutokana na athari hizi. Inapasa wenye midahilishi, video na sinema wasiwaruhusu vijana kutazama uchafu huu.
Tatizo la kuenea kwa ponografia limeendelea kuwepo kwa sababu ya udhaifu wa sheria. Kilichoko basi ni kuweka
sheria za kuzuia utengenezaji na usambazaji wa upujufu huu. Kuambatana na haya, hatua kali zichukuliwe kwa
wanaovunja sheria hizi. Hali kadhalika, ushirikiano wa karibu baina ya wadau uimarishwe katika ulimwengu
mzima. Serikali na wanaohusika wakabiliwe ipasavyo. Jamii ingependa kuona michakato ya kuharamisha
utengenezaji, usambazaji na utangazaji wa ponografia ikiwekwa.
Wazazi nao wasijipweteke tu bali nao wasaidie. Ni muhimu washikilie kwa shati juhudi zao za kuwaelekeza na
kuwashauri watoto kuzingatia uongofu na kukwepa picha hizi najisi. Watoto lazima waeleweshwe kuwa haifai
kutazama picha au michoro michafu. Itikadi na imani za kidini na utamaduni wa Kiafrika unakataza vikali mtu
kuona uchi wa mtu mwingine. Matokeo ya kuasi makatazo haya yana madhara makubwa kwa watu na jamii.
(a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu, fanya muhtasari wa aya ya pili

4
naya tatu. (maneno 20 – 25) (alama 6, 1 ya utiririko)
Matayarisho
Nakala safi
b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya nne hadi ya tisa. (Maneno 55-60)
(aama 9, 1 ya utiririrko)
Matayarisho
Nakala safi
3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Andika kwa maneno. (alama 2)
(i) 11,001
(ii) 10,001
b) Eleza sifa zinazofananisha na kutofautisha sauti zifuatazo. b na d. (alama 3)
c) Eleza matumizi ya viambishi VITATU vya ngeli ya MAHALI huku ukivitungia sentensi mwafaka.
(alama 3)
(d) Tunga sentensi ukitumia neno ‘kuja’ kama: (alama 2)
(i) Nomino
(ii) Kitenzi
(e) Tunga sentensi ukitumia vielezi vinavyotokana na maneno uliyopewa. (alama 3)
(i) Soko
(ii) Zidisha
(iii) Mtoto
(f) Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Wazazi wanalipia watoto karo kwa hundi.
(g) Tunga sentensi sahili yenye viungo vya sarufi vifuatavyo. (alama 3)
(i) Shina la kitenzi cha silabi moja
(ii) Kauli ya kufanyia
(iii) Kikanushi
(iv) wakati uliopita
(v) Mtendewa nafsi ya tatu umoja
(vi) Kiima nafsi ya pili wingi.
h) Neno ‘tikiti’ hupatikana katika NGELI mbili tofauti. Taja NGELI hizo huku ukitunga sentensi mbili
kubainisha matumizi tofauti. (alama 3)
(i) Tunga sentensi sahihi ukitumia viunganishi vyenye dhana ya:
(i) Kinyume (alama 2)
(ii) Kutowezekana kuwili.
(j) Andika kwa wakati ujao (alama 2)
Ungalifanya kazi kwa bidii usingaliishi maisha ya dhiki.
(k) Tumia neno ‘mpaka’ kama kihusishi cha: (alama 3)
(i) Kiwango
(ii) wakati
(iii) Mahali
(l) Kamilisha sentensi kwa kutumia vivumishi kama ulivyoagizwa. (alama 3)
(i) Rehema ni bibi ……………………………. bezo . (umilikaji)
(ii) Naomba kinywaji …………………………… (ziada)
(iii) Muonye bawabu …………………………….. kwa kutofika mapema. (kusisitiza- mbali kidogo)
(m) Tofautisha kimaana (alama 2)
(i) Aliuawa mnyama.
(ii) Mnyama aliuliwa
n) Tunga sentensi moja kudhihirisha matumizi tofautiya ‘po’. (alama 2)
o) Andika kwa msemo halisi. (alama 2)
Askari alisema angemuona siku hiyo jioni dukanimwe.
p) Tunga sentensi ukitumia ulivyopewa katika kauli ya kutendewa. (alama 2)
(i) Pa
(ii) La
4. ISIMU JAMII
(a) Tofautisha kati ya kuhamisha msimbo na kuchanganya msimbo. (alama 2)

5
(b) Taja mambo mawili yanayoonyesha udhaifu katika mazungumzo na huchangia katika uhamishaji wa
msimbo. (alama 2)
c) Taja kaida mbili zinazotawala matumizi ya maamkizi katika jamii huku ukitoa mifano mwafaka.
(alama 2)
d) Fananisha sifa zozote nne za sajili za maabadini na mahakamani. (alama 4)
Mwisho






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers