Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Karatasi La 3 Question Paper

Kiswahili Karatasi La 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2008



Jina ……………………………………………… Namba yako ………………………………...
Shule ……………………………………………. Sahihi ya mtahiniwa ………………...……..
Tarehe ………………………………………
102/3
KISWAHILI
(FASIHI YA KISWAHILI)
Karatasi ya 3
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MTIHANI WA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA BONDO-RARIENDA - 2008
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA – (K.C.S.E.)
102/3
KISWAHILI
(FASIHI YA KISWAHILI)
Karatasi ya 3
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MAAGIZO:
??Jibu maswali manne pekee
??Swali la kwanza ni la lazima
??Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Tamthilia, Riwaya,
Ushairi na FAsihi Simulizi
??Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.

2
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
HADITHI FUPI ( LAZIMA)
MAYAI WAZIRI WA MARADHI
1. a) Kwa kutoa mifano mwafaka, fafanua jinsi wanaume walivyosawiriwa katika hadithi za
Uteuzi wa Moyoni (Rayya Timammy) na Ngome ya nafsi. (Clara Momanyi).
(alama 16)
b) Kwa mujibu wa hadithi ya Uteuzi wa Mayoni fafanua athari ya kudhalilishwa kwa
wanawake
(alama 4)
RIWAYA
Z. BURHANI: MWISHO WA KOSA
Jibu swali la 2 au la 3
2. Dhihirisha dhana ya kuwa kukithiri kwa madhara / athari mbaya katika riwaya ya Mwisho wa Kosa
kumeletwa na kutowajibika kwa wahusika wenyewe. (alama 20)
3. “Sikiliza niondoke hapa mlangoni na ujinga wako. Watu kama nyinyi haina faida kukuambieni lolote”.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Eleza makosa mbali mbali aliyofanya mzungumzaji. (alama 6)
c) Toa mtazamo wa mzungumzaji kuhusu mgogoro wa elimu hapo baadaye. (alama 4)
d) eleza hulka za mzungumziwa. (alama 6)
TAMTHILIA
KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani
Jibu swali la 4 au la 5
4. Ukirejelea tamthilia ya Kifo Kisimani onyesha jinsi mwandishi alivyowasawiri wanawake.
(alama 20)
5. Anwani ya Kifo Kisimani ina mshikamano thabiti na yaliyomo katika tamthilia. Fafanua rai hii kwa
mifano mwafaka. (alama 20)
USHAIRI
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
WANANAMBIA MCHAFU
1. Wananambia, naharibu utu wangu
Wananambia, nalizika jina langu
Wananambia, na kutaja siri zangu
Bali wanashidwa, kuchungua kisa changu.
2. Wananisubu, machafu matendo yangu
Wananisubu, najivua nguo zangu
Wananisubu, siujali uke wangu
Bali wanashindwa, kuchungua kisa changu.
3. Wanahujumu, asili ya damu yangu
Wanahujumu, tonge na kivazi changu
Wanahujumu, nyendo na shughuli zangu
Bali wanashindwa, kuchungua kisa changu.
4. Wananilani, baba hata mama yangu
Wananilani, wasema sihofu Mungu
Wananilani, hawaji mazishi yangu
Bali wanashindwa, kuchungua kisa changu
5. Hawatafuti, wakajua shida zanuu
Hawatafuti, kisa cha uchafu wangu
Hawatafuti, tamu na wangu uchungu
Bali wanashindwa, kuchungua kisa changu
6. Nawauliza, nani apendaye pingu?
Nawauliza, Machafu ya ulimwengu
Nawauliza, nielezeni wenzangu
Bali wanashindwa, kuchungua kisa changu
7. Nawaeleza, nimemaliza mizungu
Nawaeleza, uchafu si haja yangu
Nawaeleza, nawapeni siri yangu
Bali wanashindwa, kuchungua kisa changu
MASWALI
a) Shairi hili ni la bahari gani? Toa sababu ya jawabu lako. (alama 2)
b) Mshairi analaumiwa kwa mambo gani? (alama 4)
c) Eleza muundo wa beti mbili za kwanza. (alama 4)
d) Eleza kwa kutumia mifano jinsi mshairi alivyotumia idhini ya ushairi. (alama 6)
e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
(i) Utu
(ii) Wananisubu.
(iii) Tonge
(iv) Mizungu. (alama 4)
FASIHI SIMULIZI
7. Isome hadithi hii kisha ujibu maswali yafuatayo.
Katika kijiji cha Nyapiedho, katika wilaya ya Bondo paliishi shaibu mmoja aliyeitwa Munubi. Maisha yake
yalikuwa si ya kuridhisha kwani ni ya mabaa na ya huzuni. Nyumba ilikuwa ya kibanda kidogo cha ufukara.
Mzee Munubi aliishi peke yake. Alikuwa hana mke wala mtoto. Nguo zake alizokuwa akizivaa zilikuwa za
virakaviraka na si za kistaarabu, mzee, masikini alikuwa hafanyi kazi na njia ya kujipatia chake ilikuwa ni shida.
Kijijini hapo palikuwa na mto mmoja mpana na wa kina kirefu sana. Wakati mto ukifurika hauvukiki kwa njia
yoyote, labda kwa mitumbwi. Munubi alikuwa akiishi kando kando ya mto. Siku moja mto ulipofurika, watu
hapo kijijini walipata taabu sana ya kuvuka mto kwenda ng’ambo ya pili katika kijiji kingine.
Maisha yalikuwa ni ya taabu mno, hasa katika upande wa chakula kwani watu katika vijiji hivi viwili waliweza
kubadilishana miseto na kushirikiana kwa njia mbali mbali lakini hayo yalikuwa yakikatishwa na mafuriko ya mto.
Mzee Munubi alikuwa fundi sana utengenezaji wa ngalawa, basi akatengeneza mmoja wa kuwavusha watu.
Ulipokamilika aliweza kuwavusha watu salama, na kwa njia hii aliweza kujipa riziki, tia kiasi kidogo cha hela cha
kununulia nusu kibaba cha unga na vipande vya papa na nguni kila siku. Aliendelea kuishi vivyo hivyo.
Watu walikuwa wanavushwa kila siku hata siku moja mzee mwenzake mnyonge alikuwa avushwe. Alifiwa
ng’ambo ya pili na mjukuu wake. Kwa kuwa wazee hawa walikuwa marafiki, hawakutozana kitu. Alimsaidia
rafikiye.
Mzee Mnyonge aliingia ngalawani. Mto pia ulikuwa mpana na ulichukua muda mwingi kuvuka. Katika
mtumbwi, Mzee Mnyonge alishangaa sana kuona jinsi rafiki yake alivyokuwa mchafu, lakini hakuthubutu
kumwambia au kuguna na kutoa masihara ya aina yoyote.
Walipofika ng’ambo ya pili, mze Mnyonge alimshukuru rafiki yake sana, lakini alionelea kumtaradhi kidogo.
Alimfokea Mzee Munubi na kumtukana kwa uchafu wake. Aliapa kabisa eti hawezi kupanda mitumbwi ya watu
wachafu ambao hawafai nguo zao na wanaonuka beberu kando.
Mzee Munubi alikuwa hana la kusema, yake yalikuwa ni macho na masikio. Lililotoka kinywani mwake ni neno
‘hewalla ‘bwana”. Alilia sana kwa uchungu.
Muyonge alipomaliza kumshtumu mwenzake aliendelea na safari yake na alisahau kwamba saa ya kurudi ni moja.

Punde si punde Mzee Mnyonge alimaliza shida yake mara akatokea mtoni ati Munubi amvushe tena. Munubi
alikuwa hajasahau matapishi aliyopikiwa wakati uliopita, kwa hayo alighairi na kukataa kumvusha adui yake.
Mzee Mnyonge hakuweza kuvuka. Ama kwa kweli, mnyonge alimtukana mkunga hali uzazi alikuwa bado nao.
Je, huo ni uungwana kweli? Kumtukana mwenzako halafu uombe msaada kwake tena? Naam, tusiwe wepesi wa
kusahau kuwa mchama ago hanyeli huenda akauya hapo.
MASWALI
a) Eleza dhamira ya hadithi hii. (alama 2)
b) Tambua sifa zozote tatu za hadithi katika hadithi hii. (alama 3)
c) Taja methali mbili zinazolenga kisa cha mzee Munubi na Mzee Mnyonge. (alama 2)
d) Eleza maana bayana, batini na matumizi ya methali ( c) huku ukirejelea hadithi uliyoisoma.
(alama 4)
e) Eleza umuhimu wa hadithi katika jamii. (alama 3)
f) Taja na kufafanua sifa nzuri za utambaji wa hadithi. (alama 4)
g) Kuna tofauti gani baina ya ngano za mtanziko na ngano za kiayari. (alama 2)
MWISHO






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers