Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nandi Central-Usahihisho Wa Karatasi Ya Tatu Question Paper

Nandi Central-Usahihisho Wa Karatasi Ya Tatu 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2009



WILAYA YA NANDI YA KATI - 2009
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SWALI LA LAZIMA
FASIHI SIMULIZI

1. (a) Maghani ni utungo wa kishairi ambao hutongolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya
uimbaji na uzungumzaji (alama 2)

(b)
(i) Vivugo ni ushairi wa kujisifia unoatungwa papo kwa hapo aghalabu na janani mwanaume.

(ii) Tondozi - utungo wa kutukuza watu, wanyama vitu kama magari, miti, ng’ombe, milima nk.

(iii) Pembezi - ni aina ya tondozi ambayo imekusudiwa kusifia watu wa aina fulani katika jamii kutokana na matendo yao au mchango wao katika jamii.

(iv) Rara: Ni utungo wa kishairi wenye ubunifu mkubwa unaukusudiwa kusisimua.
(Hoja4 x 2 = 8)
(c) Uhodari wa kuzungumza au kuiga mazungumzo kwa usanii na uhodari mkubwa
(alama 2)
(d)
? Ujuzi wa kina wa utamaduni, desturi, mila na sheria za jamii
? Mzingiro mpana wa maisha
? Ufundi wa kutumia lugha, semi, mafumbo n.k.
? Uwezo wa kutumia mbinu mbali mbali za kuwasiliana mfano, nyimbo, ushairi n.k.
? Umahiri wa kughani, kusema kwa mfululizo na mwendo wa kasi.
? Kutumia sauti inayosikika bila shida.
? Ufundi wa kutumia kunga za maswali
(Zozote 4x1 =8)
UTENGANO
2. (a)
? Ni nyumbani kwa Kazija
? Mzungumzaji ni Kazija
? Mzungumziwa ni Mussa
? Ni usiku ambapo Mussa alifumaniwa na babake (4x1=4)
(b) Kejeli (alama 2)
(c) Mzungumzaji ni Kazija
Sifa:
? Jasiri
? Muasherati
? Ana tamaa
? Ni fasiki
? Mweka kisasi
? Mnafiki
? Mwenye chuki (Zozote 4x1=4)

(d) Maudhui ya mabadiliko
(i) Mussa:
? Awali alikuwa na tabia zisizoafikiana na maadili ya kijamii. Alifuata vimada na maisha yalikuwa ya kushiriki ulevi. Ulevi na kuandamana na ureda unamsababishia aibu kwa Kazija anapofumaniwa na babake
? Baada ya kichapo kutoka kwa babake pale kwa Kazija anaamua kuendelea na masomo yake chuoni. Anasoma mpaka anahitimu udaktari
? Mussa hashiriki ulevi wala uredi bali ameshajipatia mke, Sihaba na anatekeleza wajibu wake kazini (2x1=2)
(ii) Maksuudi
? Mwanzoni alikuwa maskini. Baada ya uhuru alibadilika na kuwa tajiri
? Alikuwa dhalimu na katili baada ya kutoka jela alianza kutafuta familia yake kwa moyo wa huruma. (2x1=2)

Maimuna
? Alikuwa adilifu na baada ya kutoroka nyumbani akabadilika na kuwa mwasherati
? Anapokutana na Kabi, anabadilika wanapendana hadi kuoana
? Anapoolewa anaacha mapenzi ya pesa, akampenda Kabi na kuwa mchapa kazi.
(2x1=2)
Farashuu
Mwanzoni alikuwa amejaa kisasi dhidi ya familia ya maksuudi na baadaye kubadilika na
kumruhusu Maimuna, mwanamke Maksuudi aolewa na mjukuwe Kabi na hata kusikitishwa na kifo cha Maksuudi (2x1=2)

Biti Kocho
Alikuwa kijakazi mpole kabla ya Maksuudi kumpiga mkewe kwa kuzalishwa na mkunga kutoka nje. Maksuudi anapomchapa mkewe kiasi cha kumwua, biti Kocho anamkemea
Ujasiri unamwingia kwa sababu ya uchungu na hata kumfanya Maksuudi kumwachilia Bi. Tamima (2x1=2)
Hoja moja kwa kila mhusika na kufafanuliwa vizuri
(1x2=2. jumla alama 10)
3. (a)
(i) Ukahaba/ udanguro
Wanawake wengi wamejitosa katika ukahaba k.m. Dora, Maimuna, Kazija n.k./ wanaume pia kujiingiza k.m. Maksuudi
(ii) Ulevi
Wengi washiriki katika ulevi tajiri na maskini k.m. Mussa, Maimuna, Shoka
(iii) Ufisadi
Viongozi kama Maksuudi na Zanga, viongozi wa polisi, wanalangua mali ili kujitajirisha
(iv) Kisasi
Farashuu anapanga njama kufarakisha jamii ya Maksudi
(v) Ubabedume
Maksudi alitumia uonevu wa kijinsia kumkandamiza Mwanasururu, Tamima, Maimuna
(vi) Uonevu wa kijinsia
Wanawake wanaonewa na kubaguliwa, kielimu k.m. Maksuudi kuonea Mwanasururu, Maimuna
(vii) Utawa
Wanawake wanatawishwa huku wanaume wakiachwa huru kufanya watakalo k.m. Tamima, Maimuna/ Mussa, Maksuudi.
(viii) Wizi
Viongozi kama Maksuudi wanaiba mali ya umma/ pesa za Mama Jeni zinaibiwa na Maimuna asingiziwa
(ix) Hongo
Mke wa Bakari alitoa hongo kwa Maksudi ili amtilie sahihi Biti Kocho alitaka kumhonga anayetoa viwanja vya biashara Maksudi alitaka kumhonga Inspekata Fadhili
(x) Utabaka
Wenye mali waliishi katika mitaa ya kifahari/ maskini vibanda vibovu. Maskini walilazimika kunyenyekea
(xi) Chuki
Kazija anawachukia wanaume, Farashuu anamchukia Maksuudi
(xii) Wivu
Wasichana kwenye danguro wanamwonea wivu Maimuna
(xiii) Vita
Maimuna alizoea kupigana katika kilabu/ Maksuudi kumpiga Tamima na Mussa
(xiv) Ukatili
Maksudi anawafanyia mke na watoto wake ukatili, anawatawisha, kuwapiga, kuwataliki
(xv) Talaka
Zinafanywa kiholela k.m. Maksuudi kwa Mwanasururu na Tamima
(Zozote 10x2=20)
KIFO KISIMANI - MWONGOZI
4. (a)
? Ni katika ukumbi wa utawala wa Butangi
? Batu (mhusika B) anazungumza na Kame (mhusika A)
? Wanabishana juu ya kisa cha Mwelusi kutoroka gerezani
? Hapo kabla, askari wa II alikuwa amewaarifu kuwa Mwelusi alikuwa ametoroka
? Baadaye Bokono anawasihi na kupata habari ya kutoroka kwa Mwelusi
(Zozote 4x1 =4)
(ii)
? Washauri wa Bokono kutoelewana juu ya namna ya kumnyamazisha Mwelusi
? Hali ya Kame kumhurumia Mwelusi na kumuunga mkono huku Batu akitaka auawe
? Hali ya Batu kutaka Askari waliokuwa wakimlinda Mwelusi walaumiwe kwa kutofanya kazi yao vyema huku Kame akipendekeza uchunguzi ufanywe ili kujua ukweli halisi
? Hali ya Kame kuwa mshauri ambaye alitaka Bokono aambiwe ukweli huku Batu akiwa barakala/ mwongo
(Zozote 3x2=6)
(b) Mbinu za lugha
(i) Uzungumzi nafsi
? Bokono alizungumza peke yake kuhusu uongozi wake
? Mwelusi alizungumza peke yake alipoachwa na watesi wake
? Gege anajizungumzia baada ya Tanya kuondoka
? Gege anajisemea mwenyewe kimoyomoyo (kimawazo) jinsi alivyojaribu kumshauri Mwelusi
(1x4=4)
Maana alama = 2
Maelezo alama 2x1=2
(ii) Lugha ya matusi
? Askari wa I na III walitusiana pale nje ya gereza
? Bokono anatumia lugha ya matusi kwa mkewe Nyalwe (1x2=2)
(iii) Taswira
? Kipigo anachokipata Mwelusi gerezani
? Ndoto ya Bokono usiku akizikwa akiwa hai
? Mali atakayotunukiwa Gege akikubali kushirikiana na utawala kumkomesha Mwelusi
? Nyalwe alipokuwa akieleza jinsi mumewe anavyobadilika kutoka mtu mzima hadi anapokuwa mimba katika tumbo la mamake
? Maelezo ya Mweke na Talui juu ya urembo wa Alida
Maana – alama 2
Maelezo 2x1=2
5. (a) Mwanamke kama kiumbe aliyedhulumiwa
? Ni kifaa cha kazi – ndiye wa kuandaa mahali pa kufanyia mkutano wa kisiasa kama Kaloo na Azena
? Ndiye wa kufanya kazi za nyumbani kama kuteka maji kisimani k.m Andua
? Chombo cha burudani - ndiye wa kuchezea wageni muziki mfano Kaloo
? Chombo cha mapenzi – askari wa III anamfanyia Andua mzaha kumpapasa kifuani. Aidha Bokono anamtaka Bi Kaloo kimapenzi
? Ananyimwa uhuru wa kutangamana na jamii yake. Atege anachukuliwa kuwa mchumba wa Mwelusi kwa sababu anashirikiana naye tu
(5x2=10 ifafanuliwe vizuri)
(b) Maudhui ya tamaa
? Tamaa ya uongozi. Bokono hataki kubanduka madarakani
? Tamaa ya anasa. Askari wa II, III na Bokono wanaonyesha hali hii kwa njia nyingi
? Tamaa ya mali. Viongozi wamejilimbikiza mali tele. Bokono na wafuasi wake
? Tamaa ya vyeo. Gege anafanywa kuwa kiongiozi wa vijana na tuzo ya cheo cha mkuki wa Almasi
? Tamaa ya utawala mzuri. Hii ilikuwa tamaa ya wanabutangi wote isipokuwa wafuasi wachache
(Zozote 5x2=10. Ifafanuliwe vizuri)

MWONGOZO – MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE
6.
? Utamanduni umetumiwa kumkandamiza mwanamke na kumpendelea mwanaume
? Babake Zena hakuwaelimisha binti zake
? Mabinti walilazimishwa kuolewa – Zena
? Mumewe Zena alimdhulumu - kumpiga
? Mumewe Zena hakuwa mwaminifu katika ndoa na hakutaka kuulizwa
? Utamaduni haukumruhusu Zena kurudi kwao
? Malalamishi ya Zena hayakukubaliwa na mamake Ali wala mzee Saidi
? Zena kulaumiwa kwa sababu ya talaka ilhali mume ndiye mkosa
? Zena kunyimwa kura kwa sababu ni mwanamke
? Wanawake kumtania na kukataa kumuunga mkono anapowania ubunge
? Wanawake kufanyishwa kazi za nyumbani
(Zozote 10x2=20)
MWONGOZO WA USHAIRI
7.
(a) Kufunza maana mbalimbali za maneno (1x2=1)
(b) Maana za neno ‘chungu’
(i) Tele/ ingi
(ii) Chachu
(iii) Kifaa cha kupikia (3x1=3)
(c) Nitapanda juu ya mti, mahali ambapo nimechuna tunda lililoiva kwa sababu siwezi kutulia mpaka nilipate ili nimpe mpenzi wangu ndipo jioni niweze kupapasa titi (alama 3)
(d) (i) - Lina mishororo mitatu – ni tathlitha
? Kila mshororo una vipande viwili
? Vina havifanani
? Lina beti kumi
? Mizani 16 (8, 8) (5x1=5)
(e) (i) Tabdila, mfano – usikile – usikie
(ii) Inkisari, mfano – kaseme – ukaseme
- mi - mimi
- kaziyo - kazi yako
- takwea - nitakwea
(iii) Kuboronga sarufi – Na kesho kija shambani
-Na ukija shambani kesho
(iv) Lahaja - Ola,
- Ona (Zozote 2x2)
Kutaja alama 1 mfano alama 1
(i) Makondeni – mashambani
(ii) Jitwike – weka kichwani/ mgongoni
(iii) Kiola – kiona/ kiangalia/ kitazama (3x1=3)

















More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers