Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Bondo District Mock-Kiswahili Karatasi 3 Question Paper

Bondo District Mock-Kiswahili Karatasi 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/3
FASIHI
KARATASI 3
FASIHI SIMULIZI
1. a) Huku ukitolea mifano mwafaka, taja tanzu za fasihi simulizi alama 12*BND*
b) Eleza umuhimu wa ngomezi alama 3*BND*
c) Fafanua sifa zozote tano (5) za mighani alama 5*BND*
TAMTHILIA
Kithaka wa Mberia: Kifo Kisimani
2. “ Umejaribu mara kadha. Lakini jaribu tena na tena---------- bandu bandu huisha gogo! Nenda
ukawalilie tena askari------------- Dunia haipendi wenye kukata tamaa”.
a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake alama 4*BND*
b) Taja fani zozote tatu (3) za lugha katika dondoo na uzitolee mifano na maana alama 6*BND*
c) Ni nini anachoshauriwa kujaribu tena? Alama 2*BND*
d) Askari wamekuwaje vizuizi kwa anayeambiwa kujaribu tena? Alama 2*BND*
e) Taja na ueleze maudhui yoyote matatu yanayojitokeza katika muktadha huu alama 6*BND*
3. a) Mapinduzi hayaji bila ya mwongozo bora
Eleza sifa zilizomwongoza Mwelusi kufanikiwa katika azma yake alama 8*BND*
b) Jadili nafasi ya wanawake katika jamii ya tamthilia ya Kifo Kisimani. alama 12*BND*
RIWAYA
Z. Burhani: Mwisho wa Kosa
4 a) Barua ni mojawapo ya mbinu zilizotumiwa katika ’Mwisho wa Kosa’ ili kuwasilisha ujumbe.
Eleza barua na umuhimu wa ujumbe wake alama 12*BND*
b) Je, wananchi wangenufaika vipi kwa ujenzi wa kiwanda katika riwaya ya ’mwisho wa kosa?’
alama 8*BND*
5. “Hata kama nilikunywa hapo zamani nilikuwa sijui mengi ninayoyajua sasa“
a) Weka dondoo hili katika Muktadha wake alama 4*BND*
b) Ni mambo yapi anayoyajua msemaji? alama 2*BND*
c) Jadili sifa na umuhimu wa:
(i) Mzungumzaji: alama 7*BND*
(ii) Mzungumziwa alama 7*BND*
HADITHI FUPI
E. Kezilahabi: Mayai Waziri wa maradhi na hadithi nyingine
6. a) Kwa kurejelea hadithi ya uteuzi wa moyoni, eleza jinsi itikadi, mila na desturi
zinavyodhalilisha maendeleo katika jamii husika alama 10*BND*
b) Fafanua tabia za mhusika Ali katika hadithi hiyo alama 4*BND*
c) Majuto ni mjukuu huja kinyume’. Eleza jinsi methali hii inavyooana na hadithi hii
alama 6*BND*
USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kwa makini halafu ujibu maswali yanayofuata
1. Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini
2. Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?
Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
3. Naja nije rudi papo, panigedeme mgando
Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo
Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
4. Naja sitapakimbiya, ningambwa kuna vimondo
‘Takuja kuvilekeya, vinganijiya kwa vundo
nilipozawa tafiya, sikimbii kwenda kando
nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
5. Naja hiwa ‘mekomaa, kuzidi nilivyo mwando
Tena n’najiandaa, kwa fikira na vitendo
Kwetu nije kuifaa, na kuitiliya pondo
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
6. Naja na ingawa naja, siwaeki mifundo
Moyo wangu ushatuja, mawi nalotendwa mwando
Ela wataoningoja, na vyao viwi vitendo
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
7. a) Eleza jinsi ‘uzalendo’ wa mshairi unavyojitokeza katika beti za 1 na 2 alama 4*BND*
b) Fafanua jazanda zinazopatikana katika mshororo:
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando? alama 2*BND*
c) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari alama 4*BND*
d) (i) Katika ubeti wa 5 mshairi amebadilika Eleza alama 2*BND*
(ii) Ananuia kufanya nini pindi arudipo? Alama 2*BND*
e) Eleza ujumbe unaopatikana katika ubeti wa 6 alama 2*BND*
f) Andika maneno haya katika kiswahili sanifu alama 2*BND*
a. Mwando
b. Ningambwa
g) Kibwagizo cha shairi kinampa sifa gani mshairi? Alama 2*BND*






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers