Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nandi North District Mock -Kiswahili Paper 3 Question Paper
Nandi North District Mock -Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2006
KISWAHILI
102 / 3
USHAIRI*NDI*
1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. *NDI*
LAU HAKUNA MAUTI. Na Abdalla Said Kizere*NDI*
1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
2. Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
3. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
4. Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
5. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
6. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
7. Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
8. Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
MASWALI
a) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza (alama 2) *NDI*
b) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi (alama 4) *NDI*
c) Eleza umbo la shairi hili (alama 4) *NDI*
d) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano (alama 4) *NDI*
e) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi (alama 2) *NDI*
f) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili
(alama 2) *NDI*
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na shairi (alama 2) *NDI*
(i) Tiati _________________
(ii) Shani_________________
TAMTHILIA
Kifo kisimani: kithaka wa Mberia
2. “Yaliyopita hurejea. Amekutaja tena jana. Aliniambia nikwambie umuone. Ni bahati nzuri
tumekutana leo“
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4) *NDI*
b) Eleza sifa za anayezungumziwa (alama 8) *NDI*
c) Eleza migogoro yoyote minne katika tamthilia ya kifo kisimani (alama 8) *NDI*
3. “Kifo Kisimani“ ni kielelezo cha ukatili na ufisadi. Thibitisha (alama 20*NDI*
RIWAYA: MWISHO WA KOSA(Z. Burhani)
4. Huku ukitoa mifano ifaayo, fafanua jinsi mtunzi wa riwaya ya Mwisho wa Kosa alivyojadili
maswala yafuatayo:
a) Ubinafsi
b) mabadiliko
c) Utamaduni
d) Nafasi ya mwanamke (alama 20) *NDI*
5. “Inaonyesha kuwa rafiki yetu huyu hajui namna wengine wanavyoishi, ha-ha-ha’’ Lakini kicheko
kilimkauka alipoendelea kuisoma.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) *NDI*
b) Kwa nini kicheko kilimkauka msemaji? (alama 2) *NDI*
c) kiini cha habari hii ni nini? (alama 4) *NDI*
d) Taja na ueleze mbinu zozote tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili.(alama3) *NDI*
e) Msemaji aliathirikaje? Eleza athari zote na namna alivyojinusuru. (alama 7) *NDI*
HADITHI FUPI – Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi
Nyingine (Mhariri K.W. Wamitila)
6. Huku ukirejelea hadithi ya ’Mkimbizi’ na John Habwe, eleza matatizo yanayosabishwa na vita vya
kikabila barani Afrika . (alama 20*NDI*
FASIHI SIMULIZI
7. a) Eleza umuhimu wa tanzu zifuatazo
(i) Nyimbo (alama 6) *NDI*
(ii) Vitendawili (alama 4) *NDI*
b) Taja na ueleze sifa zozote tano za ngano (alama10)*NDI*
More Question Papers