Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Uasin Gishu District Mock-Kiswahili Paper 2 Question Paper
Uasin Gishu District Mock-Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2006
KISWAHILI
102 / 2
UFAHAMU ( ALAMA 15) *UG*
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali uliyoulizwa
Tsunami, tetemeko la ardhi baharini, iliyotokea Desemba mwaka 2004 katika bara la Asia ilikuwa na athari kubwa sana. Watu wasiopungua 170,000 walipoteza maisha yao kutokana na mawimbi yaliyotufulia na tsunami hiyo katika Bahari ya Hindi. Madhara na maafa hayo yalitanda hadi maeneo ya mbali kama upwa wa Afrika Mashariki ulio na umbali wa takribani kilometa 7,000 kutoka kitovu kikuu cha tsunami hiyo. Janga hili limeibua mjadala kuhusu madhara yanayotokana na nguvu za kimaumbile. Nguvu za kimaumbile zina uwezo wa kuzua majanga yasiyoweza kutarajiwa. Mlima wa volkeno uliotulia unaweza kuvuvumka na kutapakaza zaha ambayo inaweza kuua maelfu ya watu kama ilivyotokea huko nchini Kongo. Majanga ya kimaumbile huweza kusababisha maafa, misiba na tanzia isiyokuwa na mshabaha. Sio rahisi kuweza kutasawari akilini kiwango cha madhara ya majanga haya hadi yanapotokea. Baadhi ya majanga ya kimaumbile ni kama vimbunga vya vumbi, zilizala, mafuriko, tufani, radi, ukame na hata moto.
Licha ya kuwa binadamu hawana uwezo wa kuzuia kutokea kwake, zipo hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa. Kwa mfano, yapo maeneo ambako kutokana na historia ni rahisi kujua ni majanga yepi ambayo huweza kutokea.
Kuna maeneo ambako mafuriko hutokea kila zinaponyesha mvua za mvo. Jamii inayojikuta katika mazingira hayo inapaswa kujua ni hatua zipi za kuchukua. Mathalan ujenzi wa matuta, kuhimiza wakazi kusakini katika maeneo ya juu, kuwepo na huduma za dharura za kupambana na maradhi yanayochimbukana na ungi wa maji na kadhalika. Vivyo hivyo na ukame. Ni muhali kuweza kujua ukame utatokea lini. Hata hivyo, jamii inaweza kuchukua hatua fulani ambazo zinachangia kwenye ukame kamaukataji holela wa miti. Uchimbaji wa chemchemi ni njia nyingine inayoweza kutumiwa hasa kuhakikisha kuwa taraa ukame utazuka, watu hawataathirika kutokana na kuyakosa maji ya kutumia. Wataalamu wameafikiana sasa kuwa baada ya tsunami iliyotokea lazima uwepo mfumo madhubuti wa kuweza kuudodosa mtikisiko wa ardhi ambao hutokea kwa muda kabla ya tetemeko lenyewe. Kwa njia hii watu wataweza kuonywa mapema na labda hasara kama iliyotokea kupunguzwa.
Maswali
(a) Toa kichwa mwafaka kwa makala haya. (Alama 2) *UG*
(b) Ni nini maana ya tsunami? (Alama 2) *UG*
(c ) Ni lipi lililokuwa tokeo kuu la tsunami? (Alama 2) *UG*
(d) Eleza hatua zozote nne anazoweza kuzichukua binadamu kupambana na majanga ya kimaumbile.
(Alama 4) *UG*
(e) Taja methali inayoweza kuufumbata ujumbe wa kifungu hiki. (Alama 2) *UG*
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu hiki.(Alama3) *UG*
(a) Kuvuvumka
(b) Kutasawari akilini
(c) Mvua za mvo
MUHTASARI (ALAMA 15) *UG*
2. Soma taarifa hii ifuatayo kisha ujibu maswali
Kufaulu kwa lugha ya Kiswahili kutumika katika nyanja za sayansi na teknologia kunategemea sana utekelezaji wa mpango wa kwanza wa kutumia Kiswahili kufundisha elimu ya juu. Wanafunzi wakiwa weledi wa kutumia lugha ya Kiswahili katika kujifunza masomo ya sayansi, ufundi itawasaidia kujenga moyo wa udadisi, moyo wa kujiamini na moyo wa kutafuta maarifa ya ziada, wao wenyewe kwa kusoma vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Moyo huu wa udadisi ndio msingi wa mtu kuwa mbunifu na mvumbuzi wa vitu mbalimbali.
Wanafunzi hujenga moyo wa udadisi na kujiamini ikiwa lugha inayotumika kufundisha inaeleweka vizuri kwao. Hali hii hujidhihirisha pale wanafunzi wanapouliza maswali ya kutaka kujua zaidi
kuhusu mada wanazofundishwa darasani au mambo wanayosoma wenyewe katika vitabu vya rejea.
Ari hii ya udadisi miongoni mwa wanafunzi huweza kuonekana kwa kupima aina ya maswali
yanayoulizwa. Kimsingi, maswali yote yanayofikirisha na yasiyohitaji jibu la wazi, la moja kwa moja, yanasaidia sana kukuza moyo wa udadisi na kujiamini.
Kiswahili kinapaswa kuchukua dhima hii mpya ya kutumika katika nyanja za sayansi na teknolojia kwa sababu maendeleo ya jamii hupimwa kwa teknolojia ya kisasa iliyopo. Zamani ulimwengu ulionekana kuwa ni mkubwa lakini sasa hivi kwa kutumia teknolojia mpya ya mtandao wa mawasiliano, ulimwengu sasa unaonekana kuwa sawa na kijiji. Ili tusiachwe nyuma na wenzetu kimaendeleo, hatuhitaji tu kuwa watumiaji bali pia kuwa wachangiaji wa teknolojia hii mpya ya kisasa.
Tunahitaji teknolojia hii kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi zaidi wasiojua kutumia lugha za kigeni (Kiingereza, Kifaransa n.k) waweze nao kujifunza teknolojia hii mpya kwa Kiswahili. Mathalani, kwa kuanzia tunahitaji teknolojia iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili yaani jinsi ya kutengeneza: ’Spellcheck’ ya Kiswahili kwa kutumia kompyuta, ’machine translation’ ya lugha ya Kiswahili na kutumia lugha nyingine muhimu duniani, mawasiliano ya mtandao kwa kutumia barua–e na jinsi ya kutengeneza programu mbalimbali za kompyuta kwa kutumia lugha ya Kiswahili.
Jamii itanufaika sana na teknolojia hii mpya ikiwa tu itakuwa imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
2. MASWALI
a) Andika anwani mwafaka kwa taarifa uliyosoma. (Maneno 5 –6) (Alama 1)*UG*
Matayarisho
JIbu
b) Kwa nini Kiswahili kinafaa kuafiki mabadiliko katika nyanja za sayansi na teknolojia?
(Maneno 55 – 65) (alama 8) *UG*
Matayarisho
Jibu
c) Fupisha aya ya kwanza na ya pili.
(Maneno 50 – 60) (Alama 6) *UG*
Jibu
MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
a) Akifisha sentensi ifuatayo
je utakuja kwetu siku ya alhamisi. (alama 2) *UG*
b) Onyesha kundi Nomino (KN) na kundi Tenzi (KT) katika sentensi zifuatazo(alama 4) *UG*
(i) Filamu hiyo nzuri ilivutia
ii) Mtoto ataimba vizuri
c) Andika sentensi zifuatazo ukizingatia maagizo uliyopewa katika mabano:-(alama 2) *UG*
i) Magari yote yalitiwa vidhibiti mwendo (mazoea)
(ii) Alichora akatuzwa (ngali ya masharti)
d) Tofautisha sentensi zifuatazo kimaana kwa kuongozwa na vivumishi vilivyopigiwa mistari:
(alama 2) *UG*
(i) Mtoto mwenyewe ndiye huyu
(ii) Mwenye mtoto ndiye huyu.
(e ) Bainisha viambishi awali na tamati katika sentensi ifuatayo (alama 2) *UG*
i) Walipigiana
(f ) Tunga sentensi kwa kutumia viunganishi vifuatavyo:- (alama 4) *UG*
i) Jinsi
ii) Sembuse
(g) Kwa kuzingatia upatanishi wa Kisarufi ufaao, tunga sentensi sahihi ukitumia
nomino zifuatazao. ( alama 4) *UG*
i) Ulezi
ii) Mate
h) Andika sentensi hizi tena bila kutumia kirejeshi “amba’’
(i) Mtahiniwa ambaye husoma kwa bidii ndiye ambaye hufaulu mtihani wake
Vizuri (alama 2) *UG*
(ii) Mtahiniwa ambaye amefaulu vizuri mtihani wake hujiunga na chuo kikuu(alama 2) *UG*
(i) Tambua aina za vielezi vilivyotumika katika sentensi zifuatazo.
(i) Nilipomdai pesa zangu alinijibu kimzahazaha (alama 1) *UG*
(ii) Wanafunzi wanacheza uwanjani (alama 1) *UG*
j) Ichanganue sentensi hii kwa njia ya vitawi
Mama alimpikia mtoto uji kwa sufuria. (alama 4) *UG*
k) Kwa kutumia maneno machache, eleza tofauti iliyoko katika sentensi zifuatazo.
(i) Alichekelewa alipofika
(ii) Alichekesha alipofika
(iii) Alichekelea alipofika (alama 3) *UG*
l) Geuza usemi huu uwe wa taarifa:
“ Sikubaliani nawe unaposema mambo haya ni ya kweli“. Msemaji mmoja akamwambia mwingine.
(alama 2) *UG*
m) Tunga sentensi tatu kulingana na maagizo haya:
(i) Sentensi sahili (alama 1) *UG*
(ii) Sentensi ambatano (alama 1) *UG*
(iii) Sentensi ya changamano (alama 1) *UG*
n) Tambua aina za vishazi vilivyotumika katika sentensi hizi zifuatazo
Juma aliyecheza vizuri alituzwa vyema (alama 2) *UG*
ISIMU JAMII (ALAMA 10)
4. Yasome mazungumzo haya kisha ujibu maswali yafuatiayo
MPOTEVU: Nataka pande za Kaya. Hapa Mkanyageni nimejaribu kutafuta rafiki wa kufaa,
nimekosa. Sasa nakaa kule mji wa Kale katika bweni la wageni.
KUPE: Lahaula! Umeshampata mwenyeji atakayekutimizia haja zako zote
MPOTEVU: Ni yupi huyo?
KUPE: Kutafuniwa umeshatafuniwa; kulikobaki ni kumeza tu
MPOTEVU: Mbona sikuelewi?
KUPE: (Akijongeza kiti chake karibu) Basi tuyaache hayo.
Kwani hasa umeletwa na shughuli gani huku kwetu?
MPOTEVU: Oh! Ni kama kufanyafanya biashara na kutalii kidogo ili kutazama
ulimwengu wa Walimwengu
a) Mbinu ya majina iliyotumiwa yatosha kufasri mada. Jadili. (alama 3) *UG*
b) “Lahaula! Umeshampata mwenyeji atakayekutimizia haja zako zote“
Ni mwenyeji gani anayezungumziwa hapa? (alama 2) *UG*
c) Hebu tegua kitendawili kilichomo:“Kutafuniwa umeshatafuniwa; kulikobaki ni kumeza tu.
(alama 2) *UG*
(d) Taja sajili ya mazungumzo haya (alama 1) *UG*
(e) Zitaje sifa mbili za sajili hii. (alama 2) *UG*
More Question Papers