Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Uasin Gishu District Mock-Kiswahili Paper 3 Question Paper

Uasin Gishu District Mock-Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



KISWAHILI
102 / 3
USHAIRI
1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Jama, Jama, Jamani
Mbona twabebeshwa mateso hivi
Mizigo mikubwa ya dhiki kama
Kwamba hatuna haki ya kusema
Kukataa ndoa za lazima
Kukataa kuozwa wazee
Kukataa kukatishwa masomo
Kukataa tohara ya lazima
Jama, Jama Jamani
Iweje tuteswe mateso haya
Na watu wasio kuwa hata na haya kama
Kwamba hatuna haki ya kulalamika
Kulalamikia kutumikishwa kama mayaya
Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama
Kulalamikia kutolindwa na sheria
Jama, Jama, Jamani
Sasa hii ni awamu nyingine
Na macho tumeyafungua kabisa
Tumekataa kudhalilishwa kabisa
Tumekataa kuteswa kama watumwa
Tumekataa tohara ya lazima
Tumekataa kuozwa....... Tumekataa! Tumekataa
Hii awamu ya ’Haki ya mtoto wa kike’
Maswali
a) Taja mambo matatu muhimu yaliyozungumzwa na mshairi kisha ueleze kila
moja. (Alama 6) *UG*
b) Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4) *UG*
c) Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kisha ueleze kila moja(Alama 4) *UG*
d) Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni ’awamu’ nyingine? (Alama 3) *UG*
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama 3) *UG*
(i) awamu
(ii) kudhalilishwa
(iii) Dhiki
TAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia.
2. “Nakubaliana nawe! Unazijua vizuri sana kanuni za ardhi. Na hapo ndipo pana tatizo,
unazijua vyema lakini wakati huo huo unazipuuza kama kwamba hazipo“
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha. (Alama 4) *UG*
(b) Eleza hulka za mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 6) *UG*
(c) Huku ukirejelea mzungumzaji onyesha jinsi maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza katika
tamthilia ya kifo Kisimani. (Alama 10) *UG*
3. Jadili jinsi mwandishi wa Kifo Kisimani alivyofaulu katika matumizi ya mbinu ya Kinaya katika
tamthilia yake. (Alama 20) *UG*
RIWAYA
MWISHO WA KOSA : Z. Burhani
4. Mwandishi wa Riwaya ya Mwisho wa Kosa amemchora
“ Mwanamke“ kama kielelezo bora cha maadili katika jamii. Jadili ( Alama 20) *UG*
5. “Nieleze hasa sababu ya kuumwaga uji wangu namna ile, ndio nini? Ndio mchafu kuunywa leo?“
a) Ni akina nani wanaorejelewa katika muktadha wa dondoo hili? (Alama 2) *UG*
b) Weka dondoo hili katika muktadha wake. ( Alama 8) *UG*
c) Eleza kwa kina tabia za aliyemwaga uji. ( Alama 10) *UG*
HADITHI FUPI
Mayai waziri wa Maradhi na Hadithi nyingine Na K.w Wamitila (mhariri)
6. Ngome ya Nafsi – Na Clara Momanyi
a) Eleza kwa kina Masaibu yaliyomkumba Naseko. (Alama 10) *UG*
b) Je masaibu haya yanatokana na nini? Fafanua ( Alama 4) *UG*
c) Naseko ni mtu wa namna gani? Eleza ( Alama 6) *UG*
FASIHI SIMULIZI
7. a) (i) Eleza umuhimu wa nyimbo katika usimulizi. ( Alama 2) *UG*
(ii) Taja na kueleza tanzu / aina za nyimbo ( Alama 10) *UG*
b) SEMI
Tofautisha semi hizi
i) Nahau na misimu (Alama 2) *UG*
ii) Eleza maana ya nahau hizi (Alama 4) *UG*
(a) Hawapikiki katika chungu kimoja
(b) Yeye ni jamvi la wageni
(c) Amemwaga mtama
(d) Amechomekwa mizizi
iii)Taja na kufafanua misimu yoyote miwili. (Alama 2) *UG*






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers