Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Trans-Nzoia West District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Trans-Nzoia West District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2008




Jina ………………………………………………………… Namba Yako ……………………
Shule ……………………………………………………….
102/3
KISWAHILI
Karatasi ya 3
(Fasihi)
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MTIHANI WA MAJARIBIO (MWIGO) WILAYA YA TRANS-NZOIA MAGHARIBI - 2008
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI-KCSE
102/3
KISWAHILI
Karatasi ya 3
(Fasihi)
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MAAGIZO:
• Jibu maswali manne peke yake
• Swali la kwanza ni la lazima
• Maswali yako mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Tamthilia,
Riwaya, Ushairi na Fasihi Simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka kitabu kimoja
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
HADITHI FUPI
1. Onyesha kwa kutolea mifano mwafaka pengo kati ya matajiri wa maskini katika hadithi
zifuatazo.
(i) Kachukua Hatua Nyingine. (alama 10)
(ii) Msamaria Mwema. (alama 10)
RIWAYA: MWISHO WA KOSA
2. a) Jadili maoni ya mwandishi kuhusu Elimu. (alama 10
b) Huku ukitoa mifano, eleza sifa za Monika zinazothibitisha hali yake ya kukengeuka.
(alama 10)
3. “Alimshukuru, alihisi kama aliyekuwa amebeba mzigo mzito mgongoni na sasa amepata wa
kumpokea”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Onyesha matatizo aliyoyapata kwa kuubeba mzigo huo. (alama 8)
c) Fafanua matumizi manne ya Jazanda katika riwaya hii. (alama 8)
TAMTHILIA: KIFO KISIMANI; KITHAKA MBERIA
4. “Sikuangalii kwa ubaya lakini nina wasiwasi na hali yako”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Kwa nini msemaji ana wasiwasi na hali ya anayemwambia. (alama 4)
c) Taja na ueleze sifa nne za anayeambiwa maneno haya. (alama 4)
d) Eleza maudhui manne yanayoendelezwa na anayeambiwa maneno haya.
(alama 8)
5. “Haki za wafungwa ni haki za kibinadamu”
a) Fafanua kauli hii ukirejelea Kifo Kisimani. (alama 10)
b) Jadili jinsi mwandishi anavyoisawiri jinsia ya kike. (alama 10)
FASIHI SIMULIZI
6. a) Tofautisha baina ya
(i) Hurafa na Hekaya. (alama 4)
(ii) Hadithi za mazimwi na hadithi za mtanziko. (alama 4)
(iii) Usuli na visasili. (alama 4)
He! He! He! Weee!
Unayeogopa kutahiriwa
Nani atatahiri badala yako
Eh, eh…. Ni babu yako
Eh, Eee!.... kisu kikali mno!
Lakini nitavumilia.
b) (i) Wimbo huu huitwaje? (alama 1)
(ii) Nini dhamira ya wimbo huu? (alama 2)
(iii) Taja sifa zozote tano za utanzu wa nyimbo kwa jumla. (alama 5)
USHAIRI
SEHEMU C:
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Ameumbwa mwanadamu, kwa lililo zuri umbo
Bali si wote fahamu, waliyo na sawa mambo
Wako waliyo timamu, na wengineyo wa kombo
Na mtu kuwa na tumbo, si kwamba mekamilika
Kuna walo mafidhuli, lugha yao ni matango
Na kuna wenye kauli, zisokuwa na ushingo
Kuna wake kwa wavuli, vipofu na wenye tongo
Na mtu kuwa na shingo, si kwamba mekamilika
Kuna walo na fikira, na wenye vibovu vitwa
Kuna walo na subira, husubiri kucha kutwa
Wengine tabiya bora, hino hawanayo katwa
Na mtu kuwa na kitwa, si kwamba mekamilika
Kukamilika kwa mja, ni mbali na kwa Moliwa
Kwa mja nitakutaja, ili upate kwelewa
Ni kufikiya daraja, ile aliyoumbiwa
Hapo ndipo huambiwa, mja amekamilika
Aiyelewe duniya, kwa marefu na mapana
Azipite zile ndiya, za miba mitungu sana
Avuke bahari piya, zilo na virefu vina
Hiyo ni yangu maana, ya mja kukamilika
Akishafikwa na hayo, si kwamba ndiyo akhiri
lazima awe na moyo, wa kuweza kusubiri
Kuyasubiri ambayo, yote yatayomjiri
Kama huyo 'tamkiri, ni mja mekamilika.
7. a) Kwa kuzingatia shairi, fafanua mambo muhimu yanayomfanya mtu kuwa na utu.
(alama 5)
b) Andika ubeti wa 5 kwa lugha ya nathari. (alama 4)
c) Eeza muundo wa shairi. (alama 4)
d) Onyesha kwa kutoa mifano, uhuru wa kishairi alioutumia mtunzi. (alama 4)
e) Eleza maana ya maneno haya yalivyotumika katika shairi. (alama 3)
(i) Wavuli
(ii) Katwa
(iii) Akhiri.
Mwisho






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers