Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Borabu/Masaba North District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Borabu/Masaba North District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2012
Jina…………………………………… Nambari yako………………………………/………
Shule………………………………….. Tarehe ….…………………………………………….
Sahihi ya Mtahiniwa…….……………
102/3
KISWAHILI
Karatasi ya 3
(FASIHI)
JULAI / AGOSTI - 2012
MUDA: SAA 2 ½
TATHMINI YA PAMOJA YA WILAYA ZA BORABU NA MASABA KASKAZINI- 2012
Cheti cha Kuhitimu Elimu ya Sekondari
102/3
KISWAHILI
Karatasi ya 3
(FASIHI)
JULAI / AGOSTI - 2012
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO
1. Jibu maswali MANNE pekee
2. Swali la kwanza ni la LAZIMA
3. Chagua maswali mengine matatu kutoka sehemu zilizosalia
4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
5. Kila swali lina alama 20
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote za karatasi ya mtihani zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo
A) MAYAI WAZIR1 WA MARADH1
1. Huku ukirejelea hadithi zozote kumi, thibitisha ukweli kuwa “Ibilisi wa mtu ni mtu”
(Alama 20)
B) UTENGANO S.A.M
2. “Hakupata kuchangamka katika nyumba lIe, mpaka ........Mashaka. Na sasa maadamu
anaondoka …………………..”
a) Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
b) Taja sifa nne za aliyekosa kuchangamka mpaka…………. (Alama 2)
c) Fafanua kwa kutumia wahusika wanne kama vietelezo vya mwanga wa kumaliza dhiki za
Utengano. (Atama 8)
d) Angazia mashaka manne yaliyomsibu anayeondoka alipoondoka. (Atama 4)
e) Badili ya tukio hili, taja mengine mawili yaliyobadili mkondo wa maisha ya baadhi ya
wahusika. (Alama 2)
au
3. Thibitisha kauli kwamba uchochezi ndio umefanikisha Riwaya ya Utengano. (Alama 20)
C) KIFO KISIMANI:Kithaka wa Mberia
4. “Hivi punde utakuwa na kazi. Na usiifanye nusunusu”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Eleza sifa mbili za mzungumzaji na umuhimu wake. (Atama 4)
c) Hatima ya msemaji ni chanzo cha lengo Ia apokeaye tendo. Thibitisha. (ALama 8)
d) Kumetumika mbinu gani ya uandishi katika dondoo hili? Taja na kueleza. (Atama 4)
D) FASIHI SIMULIZI
5. a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo. (Alama 5)
i) Rara
ii) Methali
iii) Lakabu
iv) Ngomezi
v) Ushairi simulizi
b) Vianzio vya ngano vina majukumu mengi. Taja matano. (Alama 5)
c) Taja methali mbilimbili ambazo kwazo istilahi zifuatazo zinajitokeza. (Alama 4)
i) Istiari
ii) Tashbihi
iii) Tashhisi
d) Ili mtampaji afanikishe utambaji wake, anahitaji mazingira yapi? (Alama 3)
e) Eleza njia zozote tatu za ukusanyaji wa fasihi simulizi. (Alama 3)
E) USHAIRI
6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata
Mvuwa iliyonyesha, ya maradi na ngurumo
Kutwa na kucha kukesha, kunyesha pasi kipimo
Haikuwanufaisha, wenye kazi za vihmo
Wenye kazi za vilimo, walifikwa na hasara
Mimeya waloipanda, ilitekukatekuka
Kazi ngumu walotenda, yote ikaharibika
Hawakuvuna matunda, waliyo wakiyataka
Waliyo wakiyataka, yakawa ya mbali nao
Wenye kuicha mvuwa, isiwatose mwilini
Baadhi yao wakawa, wakimbiliya penuni
Wengine hawakutuwa, hadi mwao majumbani
Hadi mwao majumbani, na kukomeya milango
Wenzangu dhihaka kando, nisemayo ni yakini
llibwaga kubwa shindo, mvuwa hiyójamani
Na mijaji kwa mikondo, yakawa barabarani
Yakawa barabarani, mvuwa kwisha kunyesha
Kunyesha iliposiya, kukatapakaa tope
Zilijaa’kila ndiya, isibakiye nyeupe
Ukawa mwingi udhiya, pa kupita zisitup
Pa kupita zisitupe, kwa ndiya kukosekana
Japo hivyo zilikuwa, ndiya hazipitike
Bali mimi haamuwa, kwenenda japo kwa dhiki
Kumbe vile nitakuwa, ni mfano wa samaki
Ni mfano wa samaki, kuiendeya ndowana
Zikanibwaga telezi, sikujuwa kuzendeya
Ningekwenda kwa henezi, yasingenifika haya
Lakini tena siwezi, wendo huo kutumiya
Sitawata kutembeya, ila tabadili mwendo
Maswali
a) Pendekeza kichwa mwafaka kwa shairi ulilosoma. (Alama 1)
b) Kando na kuwa tarbia, pendekeza bahari zingine zozote tatu. (Alama 3)
c) Fafanua maudhui yaliyojitokeza katika shairi. (Alama 4)
d) Uhuru wa kishairi umetumika vipi katika shairi hili ? (Alama 4)
e) Andika ubeti wa sita katika lugha nathan. (Alama 4)
f) Taja na ueleze mbinu zozote mbili za lugha katika shairi hili. (Alama 2)
g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kwa mujibu wa shairi. (Alama 2)
i) Kuicha
ii) Henezi
7.
Nilipoanza safari, ilianza kwa dhiki
Tulishikana kwa an, kwenda safari ya haki
Tukawa ni majabari, nyoyo zisitaharuki
Tukajizatiti
Njaa ikawa thibiti, na kiu kutamalaki
Nasi tulitia dhati, tusijali kuhiliki
Ingawa mbele mauti, dhila na mingi mikiki
Tulijizatiti
Huu mwisho wa safari, tukaambiwa ni haki
Shangwe kwetu na fahari, utumwa hatuutaki
Kuwa mbeie\’a safari, juhudi iIiyobki
Tulijizatiti
Ile ilikuwa ndoto, mwisho wake mafataki
Nguvu zimechomwa moto,sahili ‘mekuwa dhiki
Wagombania kipato, utashi haukatiki
Na kutabakari
Msafara ukasita, kwenye mIima wa haki
Kijasho kinatupita, miima haupandiki
Basi sote ‘kajipeta, kukikwea kima hiki
Twataka hazina
Tukiwa migongo wazi, tukainama kwa shaki
Tukawa ‘chia ukwezi, kileleni wadiriki
Wakapanda bila kazi, kuteremsha miliki
Wakaitapia
Wakafikia makazi, yapumbao na ashiki
Huko wakajibarizi, kwenye raha lakilaki
Wakaisahau ngazi, ya umma ulomiliki
Mbele ya safari
Na hazina yetu sote, kuishusha hawataki
Wamo wanatema mate, kwea umati halaiki
imezima nia yote, kiza hakitakasiki
Mbeie ya safari
Maswali
a) Pendekeza mada moja kuu inayoafiki ujumbe wa shairi. (Alama 2)
b) Shairi hill ni la bahari gani ? Taja na ueleze zozote tatu. (Alama 3)
c) Taja matatizo ya watu kulingana na shairi. (Alama 3)
d) Wanaohusishwa na shairi hill wana sifa gani? (Alama 4)
e) Ni upi muundo wa shairi hili? (Alama 4)
f) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Alama 4)
More Question Papers