Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Ndhiwa District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Ndhiwa District Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU (alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswahi yanayofuatia.
Mengi yamsesemwa kuhusiana na nchi kuwa na katiba mpya. Kile ambacho hakibainiki hasa, ni
jinsi ambavyo wanasiasa wetu, wamejitwalia nafasi ya ukunga na tena ya uzazi na mama mwenye mtoto kutupwa pembeni. Je, huyu si mtoto wa wanjiku tena?
Huenda visa vya hivi karibuni vinavyohusu familia mbalimbali vikawa na mzizi katika huy
mwan wa wanjiku. Si haba unasikia kisa cha baba ambaye amemwua mwanawe na kumkatakata
vipande vipande na kuyaacha yaoze yakiozeana kwa sababu ya msinyo au msakamo. Akili za binadamu zinapolazimishwa kwenda zaidi ya uwezo wa kawaida, matokeo aidha huwa ni kuingiwa nao wazimu, yaani kupagawa au kuua bila kukusudia.
Aidha kuna wengi ambao huyachukua maisha yao wenyewe kwa kutaka kuondokewa na shida.
Hawa husahau kuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni. Si nadra kwa hivyo kuwa na viumbe
wanaojitia kitanzi mara kwa mara ili kuepuka mng’ang’ano wa maisha yasiyo na tumaini katu. Je, hali hii itandelea hadi lini?
Muujiza mwingine ni ule wa ubakaji wa watoto na maajuza. Nyanya tena si mpenzi
aliyekusanyiwa watoto wa vijana wa kata nzima jioni na wakauzunguka moto wake, na kushiba ngano zake ambazo zilikuwa hazina mwisho. Si nyanya ambaye zao lake kuu likikua viazi vitamu na njugu karanga kwa minajili ya kuwalisha wajukuu wake jioni, na asubuhi kama ndege kuonja umande wa asubuhi? Leo nyanya anaishi kwa woga, hawaamini tena wajukuu. Ni wabakaji. Sasa vipi chemichemi ya furaha kugeuzwa simanzi ya huzuni? Wasemao husema dunia uwanja wa fujo.
Ukizuru magereza yetu ndipo utajua tuna shida katika nchi yetu. Watu wamefungiwa
tumbitumbi. Hadithi zao nazo ni nyingi: Uvutaji bangi, wizi wa kimabavu, kuua jamaa, uchopozi na zaidi. Hakuna mwisho Ashakum si matusi, ugonjwa wa “Kidon” umeanza kuwashika ndugu zetu vilivyo. Asilimia ya watu wanashikwa wakilangua dawa za kulevya haisemeki. Wote huwa na jibu lile lile. Maisha yamekuwa ghali na hapana ila kutumia kila mbinu. Je, hatujaambiwa uhalifu haulipi chochote?
Kukariri usemi huo wa Leoruad mambo mbotela na wengine wengi wenye semi kama hizo
wakiwepo wahubiri mbalimbali ni baraka maana hupunguza makali ya maisha na kutoa nafasi ya
kutabasamu kidogo, ijapo siku moja.
Maswali
(a) Dokeza visa vyovyote vinavyoonyesha msinyo kulingana na makala (Alama 3)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(b) Mwandishi wa makala anawalaumu wanasiasia kwa nini? (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(c ) Nyanya alikuwa na wajibu upi kulingana na kifungu hiki? (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(d) Fafanua “Ugonjwa wa Kidon” (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(e) Eleza ni kwa jinsi gani wajibu wa nyanya umegeuzwa na vijana wenyewe. (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(f) Fafanua msamiati huu kama ulivyotumiwa kwenye makala. (Alama 4)
(i) Tumbitumbi
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Chemichemi
………………………………………………………………………………………………………………
(iii) Ashakum si matusi
………………………………………………………………………………………………………………
(iv) Wanjiku
………………………………………………………………………………………………………………
2. MUHTASARI. (alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha uyajibu maswali yanayofuata.
Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto. Haki ni mambo mema ambayo watoto wanastahili kutendewa. Kwa kutia saini nchi hizi zimetangaza kujitolea kwao kuzilinda na kuhakikisha kuwa hakuna ukiukaji wake na kuwa watoto wote katika hilaya zao wananufaika kutokana na haki zao.
Miongoni mwa haki hizi ni kuwa kila mtoto ana haki ya kuishi na kupata chakula cha kutosha na chenye viinilishe bora. Pili, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu hii inafaa kutolewa bila ada na iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi; kisha kila mtoto ana haki ya kutopigwa na kutodunishwa kwa namna yoyote, iwe kitabaka, kirangi, kijinsia au vinginevyo. Mtoto ana haki pia kutolazimishwa kufanya kazi za kiutumwa, nzito na za kushurutishwa. Halikadhalika, ana haki ya kuishi katika nyumba au makazi bora na salama, kutunzwa na kulindwa dhidi ya hali yoyote inayoweza kumhatarisha.
Anatakiwa ashirikishwe katika kufanya maamuzi. Fauka ya haya, ana haki ya kupata huduma za afya, mahitaji maalum, michezo, upendo na habari. Isitoshe, anastahili kuheshimiwa kimawazo na kihisia.
Haki hizi zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, hivyo serikali za mataifa zimeshirikisha haki hizi katika katiba za nchi zao na sheria zao.
Walakini, haki hizi, bado zinakiukwa. Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao.
La kusikitisha na kukera ni kuwa wanaotarajiwa kuwa vigogo wa kuzilinda haki hizi ndio wanaongoza kuzikiuka. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kunyimwa chakula,
kufanyishwa kazi kipunda, kuteswa, kuishi katika mazingira hatari na hata kuuawa. Kuna watoto wengi wanaolala nje. Wengi hawapati chakula; licha ya kuwa wanatakiwa kupata chenye lishe bora. Kwao kutarajia mlo awamu tatu kwa siku ni njozi kwani hata awamu moja moja ni adimu kupata.
Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Viongozi
katika mataifa haya hawafanyi kitu ila kutazama tu wakati watoto wanaotakiwa kuwalinda, wanageuzwa kuwa mibaba ya kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia huvalishwa mabuti ya kijeshi ambayo ni mizigo mizito ya kubeba. Mbali na bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani wakati wanatakiwa kuwa wamelindwa majumbani na shuleni na wazazi wao na serikali.
Jukwaa la vijiji vya mataifa ya ulimwengu wa tatu limesheheni watoto wasioenda shule kwa
sababu ya lindi la ufukara uliokithir. Elimu ya bure inayogusiwa katika haki za watoto haipo.
Wanaong’ang’ana iwepo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana. Jiulize, watoto wangapi sasa hivi wamo majumbani bila kwenda shuleni kutokana na ukosefu wa karo? Wangapi wamo mitaani wakivuta na kunusa gundi huku wakiombaomba vishilingi?
Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima na kuungana mikono kutafuta
suluhisho la kudumu kuhusu haki za watoto. Twapasa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wako shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na
kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada bungeni kuhusu haki za
watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati bali si kwa chati.
Maswali
(a) Fupisha aya mbili za kwanza maneno (65-70) (Alama 8,Utiririko 2)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
Jibu

(b) Eleza ni vipi ukiukaji wa haki za watoto unaweza kuepukwa. (Maneno 30-35) (Alama 1,Utiririko 1)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
Jibu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
3. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
(a) Taja mojawapo ya sauti zifuatazo (Alama2)
(i) Nazali…………………………………………………………………………….
(ii) Kipasuo cha kaa kaa laini………………………………………………………
(b) Andika kwa usemi wa taarifa.
“Hivi vibanda vilivyo kando ya shule yetu vinatumiwa kulanguzia dawa za kulevya” Mwalimu mkuu
alilalamika. (Alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(c ) Akifisha.
Ah mbona hutaki kuandamana naye. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(d) Andika kwa kuzingatia maagizo (Alama 2)
Polisi mwoga akishindwa kumshambulia mwizi kwa kuhofia kutupiwa risasi.
Anza: Woga……………………………………………………………………………………..………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(e) Bainisha aina za yambwa (Alama 1)
Amina alimtungia mashairi mchumba wake.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(f) Bainisha aina za virai kwenye sentensi ifuatayo (Alama 1)
Leo asubuhi nilichelewa kuja kazini
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(g) Tumia mishale kuchanganua sentensi ifuatayo: (Alama 4)
Mtoto aliutupa mpira uliokuwa mbaya.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(h) Andika kwa udogo – wingi. (Alama 2)
Nyoka aliyekuwa na mkia mrefu aliingia nyumbani
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(i) (i) Tunga sentensi ukitumia; nomino ya wingi (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Onyesha matumizi ya kivumishi cha pekee katika sentensi ifuatayo: (Alama 1)
Wanafunzi wengine walipelekwa hospitalini
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(j) Kwa kurejelea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja (Alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
(k) Andika katika kauli ya kutendama. (Alama 2)
Serikali ina mambo mengi ambayo yamefichwa.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(l) Yakinisha sentensi ifuatayo. (Alama 2)
Wahudumu wasipopokea mishahara yao kesho hawatasherekea Krismasi kwa furaha.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(m) Unda nomino dhahania kutokana na maneno haya. (Alama 2)
(i) Dhulumu…………………………………………………………………….
(ii) Kanusha…………………………………………………………………….
(n) Bainisha matumizi ya viambishi ‘ndi’ na ‘ji’ katika sentensi zifuatazo. (Alama 2)
(i) Sisi ndisi wenye shamba hili
……………………………………………………………………………………………………………
(ii)Mtoto amejikata kidole.
……………………………………………………………………………………………………………
(o) Tunga sentensi itakayodhihirisha “Ka” ya amri na ya ukariri wa vitendo. (Alama 4)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(p) Ainisha mofimu katika neno lifuatalo (Alama 3)
Aliyefiwa
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(g) Andika kwa kinyume (Alama 1)
Hii ni njia nyembamba
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(v) Tumia ‘o’- rejeshi badala ya ‘amba’ (Alama 2)
Mtu ambaye hufungwa ni yule ambaye huhalifu sheria.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
4. ISIMU JAMII (alama10)
1. “Mheshimiwa spika naomba nipewe fursa kutoa maoni yangu kuhusu hoja iliyowasilishwa…”
(a) Weka makala haya katika muktadha wake. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
(b) Eleza sifa za mazungumzo yanayofanywa katika muktadha huo uliotajwa. (Alama 8)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………..…………..
……………………………………………………………………………………………………………
More Question Papers