Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Manga District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Manga District Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2009
Jina ………………………………………………………… Nambari Yako ……………………
Shule ………………………………………………………. Sahihi ……………………………..
Tarehe …………………………….
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA 2
(Ufahamu, Muhtasari, Matumizi ya Lugha na Isimu jamii)
JULAI / AGOSTI 2009
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA PAMOJA – WILAYA YA MANGA - 2009
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Upili.
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA 2
(Ufahamu, Muhtasari, Matumizi ya Lugha na Isimu jamii)
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO:
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Tia sahihi yako ipasavyo.
• Jibu maswali yote.
• Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa, watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU
Soma makala yaftiatayo kisha ujibu maswali.
Zamani watoto wetu walisoma kipepe wakavalishwa kipepepe, wakaiga mambo yote ya kipepe
katika kusema, kula, mavazi, mila na hata tabia Wakapinga karibu desturi zetu zote za zamani na kupendelea desturi zote za kigeni zilizoletwa na mabadiliko ya wakati bila kuchunguza. Uchomaji wa nywele, uvaaji wa nguo fupi za kubana, uendaji sinema na wasichana usiku wakifuatana na wavulana wasioaminika wala kutambulikana kwa wazee wao, wavulana na wasichana kuzubaazubaa pamoja mabarabarani. Wakaanza kujibizana na wazazi bila adabu wakati
walipokemewa na kadhalika. Zamani za kiza baba na mama walitaka taadhima. Hayo yote
yanayoenea sasa ni matokeo ya ukoloni, ukabila na ubepari.Vijana hao wakaupinga kabisa
ustaarabu, fikara, mitindo ya mavazi na hata imani za kizazi cha kale. Kwao kale ikawa imepita na mambo yake. Tatizo likaletwa kwa kuwa watu wa vizazi hivi viwili yaani watoto waliozaliwa wakati wa utawala wa mkoloni na dahari yetu tulipozaliwa; lazima kukaa pamoja. Sasa na kale ni watu wa jamaa moja.
Lakini kwa kuwa wana fikara mbalimbali na wamekuzwa katika nyakati mbali mbali,
hiyau mgongano ukawapo Jambo peke yake liliweza kuondoa matatizo hayo ni elimu ya kitititi
Tukawafundisha kuwa kuiga desturi za kigeni, ambazo hazina maana na wala hazipatani na
utamaduni wetu wa kitititi, huko si kuendelea lilah, bali ni kurudi nyuma.
Kwa kweli si vibaya sisi kuiga baadhi ya mambo kutoka kwao lakini ni lazima tuwe
waangalifu sana wa kuiga yale yenye maana kwetu na kuacha yasiyo na maana. Kama ikiwa
hatukuwa macho basi tutajishtukia tunafanya kama nyani na kasuku, yaani tunaiga lolote lile jema na la upotovu. Hii haifai lilah, kwani baadaye utajikuta katika kiza cha ujinga. Hata hivyo ni ujinga mtupu kama tungekataa kabisa kuiga baadhi ya mambo ya kigeni kwa kuchagua yale tunayoona ni mema kwa kufuatana na utamaduni wetu.
Walakini hii ni sehemu ndogo ya kazi. Inatupasa tusisahau sehemu hii ya pili ndiyo
kuangalia sana mambo ya kwetu na kupambanua yafaayo zaidi na yasiyofaa. Katika yale yafaayo
labda baadhi yake yafaa kidogo tu siku hizi. Lakini tujaribu kuyarekebisha vizuri ili yakawe ali ali kabisa baadaye. Hivi ndivyo tunavyojitahidi wanahari wa laili bila ya dharau, tukiyahifadhi na kuyatengeneza,
Kama tungefuatisha tu ustaarabu ule wa kikabila na kibepari, isingewezekana kupata maendeleo tuliyo nayo hivi sasa. Tungekaa katika kiza cha ujinga. Tukaendelea kuwa mbumbumbu kama mzungu wa reli. Njia tuliyotumia ni kujifunza kwa wageni na tukahifadhi na kuyatengeneza mambo yetu hasa yaliyo murua. Hatukutumia nguvu bali siasa na tabasuri. Njia yetu hii inaendelea kusaidia kujenga ustaarabu tulionao hivi leo.
(a) Andika kichwa kifaacho kwa makala haya. (alama 1)
…………………………………………………………………………………………..
(b) Mwandishi anamaanisha nini kwa kusema
“Watoto wetu walisoma wakavalishwa kipepe ?“ (al-ama 2)
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
(c) Mabadiliko ya wakati yaliletea watoto athari gani? (alama 2)
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
(d) Taja mifano minne ya desturi ambazo ni ithibati kwamba vijana wamepotoshwa
na ukoloni, ukabaila na ubepari. (alama 4)
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
(e) Hatua gani iliyoehukuliwa na viongozi kutatua mgongano kati ya wafuata fikara
za kizazi cha kale na kile cha leo? (alama 1)
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
(f) Eleza matokeo mawili ambayo yangeikumba jamii iwapo ingeukumbatia ustaarabu
wa kikabaila na kibepari (alama2)
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
(g) Mwandishi anatoa ushauri gani kuhusu mila zetu za kigeni? (alama 1)
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
(h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama ya1ivyotumika katika kifungu. (alama 2)
i) Elimu ya kitititi
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
ii) Wanahari wa laili
………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………….
2. MUKHTASARI
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali’
Miongoni mwa starehe ambazo Waswahili wamezihifadhi mpaka leo ni kutoleana hadithi na
kutegeana vitendawili. Starehe hizo ambazo kwa kawaida hufanywa nje huwa njiani an uani, ama ndani chumbani au ukumbini, aghalabu hufanywa wakati wa magharibi au usiku baada ya kila
mtu kumaliza kazi za nyumbani, dukani shambani., ofisini na kadhalika. Mambo haya
yakitazamwa sana itaonekana kuwa hayakufanywa vivi hivi.
Tangu zamani wazee wa Kiswahiii waliwakataza wana wao kucheza mchana.
Hawakupenda vijana wajizoeshe uvivu kwa kupiga malapa. Walisadiki kuwa mwana ambaye
hakukanywa dhidi ya utiriri huu hangeweza kujifaa yeye mwenyewe na wala hata watu
wengine.Isitoshe nani asiyejua kuwa ajizi ni nyumba ya njaa? Vijana walihimizwa kusaidia katika makazi mbali mbali yanayofanywa majumbani,mashambani an mahali popote palipohisiwa kuwa mtu angalifanyiwa jambo Ia kumpa riziki. Ndiposa ungesikia wazee wakiwaambia watoto wao, “ukisimulia hadithi rnchana utaota mkia.” Ingawa kwa watu wazima maneno haya yangekuwa
masihara, kwa watoto yaliaminika sana kwa hivyo wazazi wakapata mradi wao.Hii ndiyo maana
Waswahili wanasimuliana hadithi na kutegeana vitendawili jioni au usiku usiku.
Wazazi ambao hawataki watoto wao watembeetembee au wacheze michezo ambayo
itawafanya wakimbiekimbie na kujihasiri huwaita ndani ili wawe nao kuanzia magharibi.
Waswahili wana itikadi nyingi zinazohusiana wakati wa magharibi. Ni ajabu kuwasikia wakisema kuwa magharibi huwaleta pamoja na kutoleana hadithi. Na hata kama si hivyo hii huwa ni fursa nzuri kwa wazazi kuzungumza na watoto wao ambao kutwa nzima huwa hawakupata nafasi kuwa nao.
Starehe hizi pia huongea elimu, na kama wahenga wasemavyo, elimu ni mwanga
uangazao.Kwa mfano watoto watategewa vitendawili, jambo hili litawafanya wafikiri.Na kufikiri huku kutawafanya wavumbue mambo mengi ambayo mengine hapo awali hawakuyajua na
kuyathamini.Vile vile huwafunza werevu wa kufumba na kufumbua mafumbo ambayo ni elimu
inayohitaji kiwango kikubwa cha busara.
Kutoleana hadithi ni miongoni mwa starehe ambazo kwazo hujifunza mambo mengi
sana.Katika hadithi watoto wanaweza kujifunza mambo yanayohusu mila na desturi, katika
mambo haya watu hujifunza tabia nzuri, heshima, uvumilivu.Pia katika hadithi mtu anaweza
kujifunza mambo ya historia na pia ya mazingira aliyoyazoea na hata mambo ambayo hayajui.
Aidha hadithi ni chombo ambacho wazee hukitumia kuwafundishia watoto mbinu za
kuzungumzia. Wazee wenye busara aghalabu huwapa nafasi watoto wao wabuni na wasimulie
hadithi zao.Wakati mwingine jamaa mbili jirani huweza kukutana kufanya mashindano ya
kutambiana hadithi. Mazoezi kama haya huwawezesha vijana kufikia viwango vya juu vya
ufasaha wa matumizi ya lugha na ujasiri na ukakamavu wa kuweza kusema mbele za hadhara
kubwa katika maisha yao. Baadhi ya watambaji wakubwa waliopata kusifiwa haikosi mwanzo
wao ulikuwa wa namna hii. Hadithi pia huwafundisha watu kuhusu maisha duniani. Zinaweza
kuwafunza jinsi ya kuishi na ndugu, majirani, marafiki, wake au waume. Ulimwenguni humu
tunamoishi mna mambo mengi yanayomtatiza binadamu kwa namna mbalimbali. Hadithi
zinaweza kupendekeza mambo ya kufanya na kuonyesha njia zenye mapato mema tunapofikiwa
na adha wa kadha. Zinaweza pia kukanya na kuonyesha faida ya kutoserna uwongo ama kuishi
katika maisha yasiyo muruwa, yaliyojaa kiburi na majivuno. Hapana shaka hadithi zinaweza
kuongoza na kuwafanya watu wawe watiifu na raia wema katika nchi zao.
Maswali:
(a) Kwa nini mwandishi akaoanisha utambaji wa hadithi na wakati wa jioni? (Maneno 40) (alama 5)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
(b) Kwa maneno kati ya 50 na 60 eleza umuhimu wa kutambiana hadithi na kutegeana
vitendawili, kulingana na mwandishi, (a1ama7)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
Utiririko (alama 3)
Jumla alama 15
3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Tunga sentensi ambayo imedhihirisha (alama2)
i) Kitenzi kishirikishi kipungufu
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
ii) Kitenzi kishirikishi kikamilifu
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
b) Tumia visawe vya maneno uliyopewa katika sentensi (alama2)
i) Daktari……………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………..
ii) Kiwewe …………………….. …………………………………………………….
……………………………………………………………………………………..
c) Andika kwa msemo halisi (alama3)
Okemwa alisema kwamba angemwona siku hiyo jioni dukanimwe na akataka
ahakikishiwe kwamba angekuja.
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
d) Andika kwa wakati ujao (alama1)
Ungalifanya kazi kwa bidii usingaliishi maisha ya dhiki.
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
e) Ainisha silabi na mofimu katika neno ‘Mgeni’ (alama1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
f) Bainisha yambwa katika sentensi: (alama2)
Yohana alimkatia Osoro gauni kwa makasi.
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
g) Tumia kirejeshi ‘O’ katika sentensi hizi; (alama2)
i) Mvua imenyesha na kuharibu mali.
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
ii) Limeandikwa na kuwa
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
h) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya vishale (alama3)
Askari yule aliyekuwa mgeni alimpiga sana mfungwa
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
i) Ainisha viwakilishi katika sentensi hii (alama2)
Watatu wameingia chuoni sasa.
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
j) Fuata maagizo (alama2)
i) Mgonjwa amelazwa mapema (Kauli ya kutendesheka)
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
ii) Ameinjika chungu (Tendua)
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
k) Eleza maana zozote tatu katika sentensi (alama3)
Mara tu alipofika aliwekewa mikono
i) ………………………………………………………………………………….
ii) ………………………………………………………………………………….
iii) ………………………………………………………………………………….
l) Unda sentensi yenye vijenzi vifuatavyo vya kisarufi (alama2)
W + V + T + E
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
m) Tunga sentensi moja kudhihirisha matumizi ya (alama2)
posa
poza
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
n) Nomnio hizi hupatikana katika ngeli gani? (alama3)
i) Kithembe ……………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………….
ii) Zilizala …………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………….
iii) Zinguo ………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………….
o) Toa methali niayoafiki maelezo haya (alama2)
Matatizo ya mwenzako huonekana mepesi
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
p) Andika katika udogo na wingi (alama2)
Ukitaka kumla nguruwe chagua aliyenona
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
q) Tofautisha maana ya kauli hizi kwa kueleza (alama2)
i) Huenda ikawa ……………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
ii) Isije ikawa ……………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………
r) Akifisha sentensi hii kuleta maana mbili tofauti (alama2)
Anataka akuzungumzie
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
s) Andika katika wingi: (alama2)
Farasi aliumia ukwato wake alipokuwa akipita uani
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………..
4. IS1MU JAMII
WAKILI I: Je, Bwana Kim Kimani unakubali kuwa hupingi ushahidi wa Inspekta Onyango kuwa
wewe ukiwa peke yako au pamoja na Bi Stacy Wanjala kama kundi ulihusika au
ulilazimika kuhusika katika kifo an mauji ya……..
WAKILI II: Mweshimiwa Taji napinga mkondo wa maswali anaoufuata msomi mwenzangu kwa mteja
wangu. Kulingana na Sheria za nchi ibara 13 sehemu 2(b)(i) lazima kudhibitishwe kuwepo
kwa Corpus Delict ndipo kesi iendelee.
JAJI: Kulingana na kifungu3(d)(ii) cha ibara hiyo mkuu wa sheria atahusika tu kama Amicus
Curiae na hivyo basi……………
1. Hii ni sajili gani? (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………….
2. Eleza sifa zozote tano zinazodhihirika katika sajili hii (alama 5)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
3. Eleza sababu nne za matumizi haya ya lugha. (alama 4)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
More Question Papers