Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Transmara District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Transmara District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni lazima
• Maswali hayo mengine matatu ya chaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Riwaya, Hadithi fupi,
Fasihi simulizi na ushairi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A : THAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
LAZIMA
1. Huku ukitumia mifano mwafaka kutoka tamthilia ya kifo kisimani, fafanua mikakati inayotumiwa na
viongozi wa Afrika ili kuushikilia na kuudumisha utawala wao. (Alama 20)
SEHEMU YA B : RIWAYA
S.A Mohamed : UTENGANO
Jibu swali la 2 au la 3
2. Eleza jinsi maudhui ya unafiki yanavyojitokeza katika riwaya ya utengano. (Alama 20)
au
3. Fafanua jinsi wahusika wafuatao wanavyoafiki anwani ya riwaya ya utengano ;
(i) Maksuudi (Alama 10)
(ii) Maimuna (Alama 10)
SEHEMU YA D : USHAIRI
Jibu swali la 4 au la 5
4. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatayo.
Una moyo gani, ninakuuliza, wangu muhisani?
Na kiasi gani, unavyojiweza, ijapo tufani?
Ukiwa laini, utajipoteza, usijaribaini,
Kusimama pweke kwataka makini.
Zitavuma pepo, zitakupuliza, uanguke chini,
Ela uwe papo, unajikweleza, na kujiamini,
Utikishapo, umejiumiza, pigo la moyoni,
Kusimama pweke kwataka makini.
Utie migati, ya kukuoteza, hapo ardhini,
Kwa nia na dhati, usiogeuza, au kuihuni,
Zidata baruti, uwe wapwiza, weleke usoni,
Kusimama pweke kwataka makini.
Sishike vishindo, na mauzauza, ya kukuzaini,
Kita kama nyundo, ukiniuliza, unayoamini,
Na uje mkondo, utadidimiza, kujipa mizani,
Kusimama pweke kwataka makini.
Wengine wasiwe unaoweleza, yaliyo maani,
Wewe ndiwe wewe, utawageuza, pindipo mwakani,
Ela jichukuwe, pia kujikaza, katika midani,
Kusimama pweke kwataka makini.
Maswali
(a) Mshairi anasema kusimama pweke kuna hatari gani? (Al.2)
(b) Ni mashauri gani anayotoa mshairi kwa msimama pweke ? (A.2)
(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Utie migati ya kukuoteza, hapo ardhini” ? (Al.2)
(d) Ubeti wa tatu una maana gani? (Al.2)
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi; (Al.4)
(i) tufani
(ii) unajikweleza
(iii) kuihuni
(iv) mauzauza
(f) Mshairi ametumia bahari ngapi katika shairi hili. Zitaje bahari hizo na ufafanue. (Al.8)
5. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Yamerundikwa machicha, na maganda ya matunda,
Na mwiko uliochacha, na mabli uliorunda,
Harufu inaposecha, yanukia nipenda,
Hakuna inomchusha, bustani ya maua.
Mianzi yetu ya pua, imeota pasigaa,
Hasia zinobagua, mara mbili zinafaa,
Kibaya tunarundua, kizuri kina balaa,
Tope ziwe ni halua, na samli imekaa.
Macho yameota kungu, ila yanaona yote,
Hata likitanda wingu, anga linatanda kote,
Ni mzuri ulimwengu, na furaha na wa kite,
Na bustani wenzangu, kipita siteme mate.
Mahame na maanguko, machoni yanapumbaza,
Kifusi na mafuniko, moyoni yanaliwaza,
Mapakacha ya rundiko, topasi yanampoza,
Hakuna inomchusa, bustani ya maua.
Kuku anapara kucha, na bata tope aponda,
Mbwa pua inapucha, pipani anamowinda,
Taka zimejenga picha, inovutia kushinda,
Vitalu vyenye mahaba, ni lazima kuvilinda.
Mbu wanazaiana, panya wanadunduiza,
Njiani tunapishana, nzi wanatumbuiza,
Maradhi huzidiana, twacheka tukipuuza,
Liwazo kubwa si haba, bustani yapendeza.
Maswali
(a) Ni nini dhamira ya mtunzi katika shairi hili. (al.2)
(b) Vitaje vitu vya kuchukiza ambavyo mshairi anavizungumzia katika shairi hili. (al.3)
(c) Kwa nini mshairi anasema kuwa macho yameota kungu ubeti wa tatu ? (al.2)
(d) Ni nini ujumbe wa mshairi hili. (al.3)
(e) Eleza muundo wa shairi hili. (al.4)
(f) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa shairi hili (al.6)
(i) imeota pasigaa
(ii) kibaya tunarandua
(iii) macho yameota kungi
SEHEMU YA C : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI wa MARADHI na HADITHI NYINGINE: K.W. WAMITILA
6. Kwa kurejelea kitabu cha mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine, fafanua jinsi tatizo la ufisadi
lilivyokita mizizi katika jamii. (al.20)
SEHEMU YA D: FASIHI SIMULIZI.
7. (a) (i) Ngomezi ni nini ? (al.2)
(ii) Fafanua sifa zote tano za ngomezi. (al.5)
(iii) Ni nini umuhimu wa ngomezi katika jamii. (al.5)
(b) Eleza njia za kukusanya kazi ya fasihi simulizi. (al.3)
(c) Kwa nini ni muhimu kukusanya kazi ya fasihi simulizi. (al.5)
More Question Papers