Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Transmara District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Transmara District Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo
1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu, hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe
mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya watu ambao
wanaamini kuwa jukumu hili muhimu hutekelezwa bora na mama; wengine husema ni jukumu la
baba. Ni kweli kwamba mtoto huwa na mama yake kwa muda mrefu zaidi ya baba lakini kivuli cha baba hakikosi kumwandama na kumwathiri maisha yake.
Uongozi wa mama huanzia siku ya mwanawe kuingia ulimwengu kwa hivyo, mama zaidi ya
baba huwa ndiye chanzo cha chemichemi ya maisha ya mwanawe. Mtoto wa kawaida ana tabia ya
kuiga kila jambo analoliona na kusikia na mambo ya awali ajifunzayo kutokana na mamaye.
Je; mtoto huiga kutokana na mama pekee? Kila utamaduni hasa huku kwetu Afrika, una
taratibu zake zilizopangwa kuhusu malezi ya watoto. Kwa mfano ; akina baba wengine wanaoishi maisha ya kijadi huonelea kwamba ni jukume lao kuwalea watoto wa kiume. Kwa hivyo mvulana anayekulia katika mazingira haya akishachuchuka kiasi cha kujua lipi zuri na lipi baya huanzia kuwa mtoto wa baba zaidi ya kuwa wa mama. Baba huathiri mtoto wake kwa kushauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume. Hupenda kukaa naye katika uga wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume huku akimkataza kukaa jikoni na kumsisitizia kuwa wanawake ni tofauti naye. Aidha, humfunza sifa kama vile ushujaa na uvumilivu kwa namna ambavyo huona kuwa ni ya kiume. Pindi mtoto anapoonyesha tabia za kikekike, baba hujiandaa kuzitadaruki kwa kumkaripia. Baba hutaka kujiona mwenyewe katika hulka ya mwanawe.
Baba kama huyu humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wake wa kiume
kwa jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. Kwa upande mwingine baba huyu huwa na machache ya kuzungumza na bintiye kwa kuwa huona kuwa sistahili yake kufanya hivyo. Mtoto wa kike huachiwa mamake lakini kutokeapo jambo la kulipima mama huona linampita kimo, humwita baba kuingilia kati na angalabu baba naye humwagiza dadake aje atoe suluhisho mwafaka.
Ulezi kama huu una nafasi yake katika jamii, lakini ni lazima tukiri kuwa pia unaendeleza
maisha ya fawaishi na kuanzia taasubi ambayo hatima yake ni mwanamke kukandamizwa na
mwanaume. Wazazi walio na mwelekeo huu katika malezi yao hufikiri kuwa wataishi na watoto wao katika mazingira finyu na kwa hivyo waendelee kuwapulizia pumzi za kuhilikisha. Lakini ni sharti wakumbuke kuwa wao si walezi peke yao na mtoto hawezi kuishi pekee yake na kuwa na tabia ya kipekee. Leo ataishi kwao lakini kesho itambidi atoke aone ulimwengu. Kila atakapotia mguu ataona mambo mapya yatakayompa tajriba mpya na mawazo mapya ambayo aghalabu yataendelea kuathiri hulka yake. Iwapo tabia alizopata kwa wazazi wake hapo awali zilikuwa na misingi isiyokuwa madhubuti na mielekeo finyu, zinaweza kuwa pingamizi katika maingiliano yake na watu wengine.
Mambo haya yanatuelekeza katika kufikiri kwamba maisha ya sikuhizi hayaruhusu ugawaji wa kazi ya malezi ya namna baba na mama wa kijadi. Baba na mama ni walezi wa kwanza ambao kwa pamoja wanapaswa kuelekeza watoto wao katika maisha ya ulimwengu iliyojaa bughudha na
ghuhuri. Ni lazima wazazi watambue tangu awali kuwa katika malezi hakuna cha ubaguzi. Hakuna, mambo ajifunzayo mtoto wa kiume ambayo hayamhusu mtoto wa kike. Uvumilivu, bidii, utiifu na kadhalika ni sifa zinazomwajibikia kila mtoto kama vile upishi, ukulima na usafi. Mwanamke tangu azali ameumbwa kuwa mama na haipasi kulazimishwa kuchagua baina ya mtoto wa kike na wa kiume. Mapenzi na wajibu wa wazazi yapaswa yasiwe na mipaka bali yawe maridhawa kwa watoto wote.
Maswali
(a) Toa kichwa mwafaka cha makala haya. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
(b) Kulingana na kifungu hiki, taja mambo mawili ambayo yanaweza kuwa hatari kwa
malezi ya watoto. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
(c) Kwa nini baba humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wa kiume katika
jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
(d) Eleza mambo mawili ambayo ni ya manufaa katika ulezi wa jadi. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
(e) Kulingana na makala haya, ushahidi gani unaonyesha kwamba kutegemeana katika
ulezi jadi? (al.3)
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
(f) Taja sifa mbili ambazo baba humfundisha mwana wa kiume. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…..……………………………………………………………………………………………………
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu hiki:
(i) chanzo cha chemichemi…
…..……………………………………………………………………………………………………
(ii) Akishachuchuka
…………………………………………………………………………………………………..……
(iii) Hulka
…………………………………………………………………………………………………..……
2. MUHTASARI
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati ya mioyo
yetu uweze kupata ufanisi na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu.
Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa.” Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tofanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja.
Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa la watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao shambani, kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka. Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wake. Wengi ni wale wenye mawazo kwamba lazima aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wageni.
Mafunzo tunayopata nyumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua
mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya mwana Kenya kujua wajibu wake
katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayo tumbaza na kufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu wazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja, “utengano ni uvundo” lugha ya kitaifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuwaza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu, wakati tunapokosea na kufanya masahihisho.
Mara moja kwani; “usipoziba ufa, utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa
makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi.
Sisi tukiwa vijana sharti tujishughulishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashtumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na nyumbani mwetu. Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeeo, amani na upendo; lazima tuwe na bidii, ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo, tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo, basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama utajiri wake. Kwa hivyo basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba au utajiri.
(a) Dokeza mambo muhimu yaliyomo katika aya ya kwanza.(maneno 65-70) (al 8,2 utiririko)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
(b) Fupisha aya ya mwisho kwa kuzingatia mambo muhimu yanayopasa vijana kufanya.
(maneno 35- 45) (ala 4, 1utiririko)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
Nakala safi
………………………………………………………………………………………………………..……
..……………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………..…
3. MATUMIZI YA LUGHA
(a) Jaza mapengo
Kutenda Kutendesha
(i) Chota …………………… …………………………… (al.1)
(ii) Lewa …………………… …………………………… (al.1)
(b) Taja sauti moja ya;
(i) King’ong’o (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kiyeyusho (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(c) Tumia neno “shujaa” katika sentensi kama:-
(i) Kivumishi (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Kielezi (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(d) Tambua vitenzi katika sentensi hii kuvipigia mistari :-
Sisi tulikwisha kutambua alikuwa na nia mbaya. Yeye ndiye mwizi. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(e) Andika wingi wa sentensi hii sentensi hii hali ya ukubwa:-
Kichinjio hiki kilikarabatiwa kwa pesa nyingi. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(f) Eleza maana zinazojitokeza katika vifungu vifuatavyo:-
(i) Jambazi kutoka dukani liliiba. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Liliiba jambazi kutoka dukani. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(iii) Kutoka dukani jambazi liliiba. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(iv) Jambazi liliiba dukani. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(g) Jaza neno ambalo ni kinyume cha lile lililopigiwa mstari katika sentensi:-
(i) Vile vitu ulivyochanganya itakubidi. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Bomba hili limeziba mwite fundi aweze. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(h) Unganisha sentensi hii kwa kutumia ‘o’ rejeshi.
Wavu umekatika. Wavu ni wao. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(i) Eleza matumizi mawili ya “ka” na utunge sentensi kwa kila mojawapo. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(j) Yakinisha sentensi hii
Sijafahamu kwa nini hawamkaribishi mpwa wao. (al.1)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(k) Andika katika usemi halisi:-
Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo. (al.3)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(l) Akifisha sentensi ifuatayo:-
Sijaona kitabu kizuri kama mayai waziri wa maradhi, utaniazima siku ngapi bashiri alimwuliza rita.
(al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(m) Changanua kwa njia ya mishale
Mama anapika na baba anasoma gazeti. (al.4)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(n) Tunga sentensi moja na uonyeshe kwa mstari: (al.3)
(i) Shamirisho kipozi
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Shamirisho kitondo
…………………………………………………………………………………………………..……
(iii) Shamirisho ala/kitumizi
…………………………………………………………………………………………………..……
(o) Tungia vitenzi vifuatavyo sentensi katika hali zilizobanwa; (al.3)
(i) Fa (mazoea)
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) La (kutendeka)
…………………………………………………………………………………………………..……
(iii) Pa (kutendea)
…………………………………………………………………………………………………..……
(p) Tambulisha kishazi tegemezi na kishazi huru. (al.2)
Wanafunzi waliofanya vyema walituzwa jana.
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(q) Pambana viambishi mbalimbali katika sentensi ifuatayo. (al.3)
Waliwapendezea
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
4. ISIMUJAMII
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali:
A: ohh, dada Naomi
B: Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
A: Asifiwe sana
B: Ehh dadangu, miezi…mingi…sijakuona
A: Dada wee…nilitumwa huko kusini…kuwahubiria watu injili (mtuomdogo) singeweza
kukataa…
B: Ehh, usiwe kama yona
A: Habari ya siku nyingi?
B: Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
A: Amen!
B: Nimeendelea kuiona neema yake
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Halleluya
A: Ni Mungu wa miujiza!
B : Amen. Hata nami niko imara katika siku hizi za mwisho
A: Amen!
B: Ni Mungu wa ajabu kweli!
A: Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
Kama Paulo na Sila …Na nikashinda (anatua). Siwezi kumpa shetani nafasi...maana
ameshindwa.
B: Ameshindwa kabisa.
Maswali:-
(i) Hii ni sajili ya wapi? Fafanua (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
(ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii .(al.6)
…………………………………………………………………………………………………..……
(iii) Taja na ueleze mambo mawili yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili Afrika mashariki na
kati. (al.2)
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
…………………………………………………………………………………………………..……
More Question Papers