Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Thika District Mock - Kiswahili Paper 1 Question Paper

Thika District Mock - Kiswahili Paper 1 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



102/1
KISWAHILI
KARATASI YA 1
INSHA
JULAI 2011
MUDA : SAA 1 ¾
MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA MKOA WILAYANI THIKA – 2011
HATI YA KUHITIMU ELIMU YA SEKONDARI KENYA (K.C.S.E)
KISWAHILI
KARATASI YA 1
INSHA
MUDA : Saa 1 ¾
MAAGIZO
(a) Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
(b) Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia
(c) Kila insha isipungue maneno 400
(d) Kila insha ina alama 20.
(e) Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa
(f) Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote za karatasi ya mtihani zimepigwa
chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. Wewe ni katibu wa kamati inayotafuta masuluhisho ya matatizo yanayowakumba waathiriwa
wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini. Andika ripoti ya kamati hiyo.
2. Mfumo wa elimu nchini Kenya hauambatani na mahitaji ya nchi. Jadili.
3. Zidiko la mwoga ni kemi.
4. Andika insha itakayomalizika kwa:
. . . walifungua mlango huo hatimaye , wengi hawakuzuia hisia zao. Waliangua vilio kwa
maafa waliyoshuhudia.
MWONGOZO
INSHA
1. Swali la lazima.
Muh: Ni insha ya kiuamilifu na hivyo sura izingatiwe. Vipengele vyote vya ripoti
vizingatiwe.
Baadhi ya hoja ni:
(i) Kununuliwa mashamba na serikali.
(ii) Kupewa mawaidha/ nasaha/ ushauri.
(iii) Kupewa msaada wa kibinadamu.
(iv) Kupewa huduma za kijamii-elimu ,tiba n.k.
(v) Serikali kubuni sera za maridhiano na utangamano wa kijamii.
(vi) Kuwepo na sheria za ardhi /mashamba nchini.
(mwalimu akadirie hoja zaidi)
2. Mfumo wa elimu
(i) Wanafunzi wanaohitimu hawajitegemei wanapofika viwango fulani vya elimu
(ii) Hautayarishi watu kikamilifu kwa taaluma wanazozisomea.
(iii) Taaluma zingine zimepitwa na wakati / hazina manufaa yoyote kwa taifa.
(iv) Wakuza mitaala hawaelewi hali halisi ya wanafunzi/ kutopanga vizuri utaratibu wa
mitaala.
(v) Masomo mengi yasiyowapa wanafunzi nafasi ya kuingiliana au kukua kijamii bali
yanasisitiza kupita mitihani ili wafaulu maishani.
(vi) Mfumo wa elimu kutooana na mifumo ya elimu ya kimataifa.
(vii) Baadhi ya taaluma muhimu ni ghali mno hivyo serikali/ taasisi hutoa mafunzo kwa
wanafunzi wachache mno.
(mwalimu akadirie hoja zaidi)
3. Mwanafunzi atambue kwamba hii ni methali
Maana: mtu mwenye shida akieleza husaidiwa bali asipoeleza hawezi kusaidiwa.
Mat: Atesekaye kimyakimya bila ya kuomba msaada , huzinduliwa kwa methali hii.
Mwanafunzi asimulie kisa kinachoonyesha alivyoteseka pasi kusema mpaka alipoamua
kusema ndipo akapata msaada.
– Mwanafunzi ashughulikie pande zote mbili za methali.
4. Mwanafunzi abuni kisa kinachoafiki tamati hii.
1. Asiache na asiongeze neno lolote .
2. Kisa kionyeshe juhudi za kufungua mlango.
3. Kisa kidhihirishe maafa yaliyotekelezwa na binadamu.






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers