Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Rachuonyo South District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Rachuonyo South District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni lazima
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani,Riwaya , Hadithi
fupiUshairi na fasihi simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A : THAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
LAZIMA
1. “Hizo ndizo athari za utawala mbaya Huwageuza binadamu kuwa wanyama kasoro mkia na
masikio marefu”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala. 4)
b) Fafanua maudhui yoyote manne yanayorejelewa katika dondoo hili (ala.4)
c) Eleza athari zozote sita za utawala mbaya kwa Wanabutangi. (ala. 12)
SEHEMU YA B : RIWAYA
S.A Mohamed : UTENGANO
Jibu swali la 2 au la 3
2. “ Mwanzo alidhani yeye kakamata mpini, lakini kumbe alikuwa kakamata makalini. Sasa ndiyo
kwanza aone kuwa kisu kimemkatakata”.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (ala.4)
b) Ni tamathali zipi mbili za usemi zinazojikoteza katika dondoo hili? (ala. 4)
c) Ni vipi kisu kilimkata mrejelewa (ala.12)
au
3. ‘Malezi ya mtoto wa kike ni kizungumkuti” thibitisha kwa kutoa mifano mwafaka kutoka katika
Riwaya ya Utengano. (ala.20
SEHEMU YA C : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADH NA HADITHI NYINGINE.
Jibu swali la 4 au la 5
4. “Mtoto wa kike ana haki sawa na yule wa kiume……..”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
b) Ni haki ipi inayorejelewa katika dondoo hili. (ala.2)
c) Eleza sifa zozote tatu za msemaji (ala.6)
d) Fafanua jinsi ambavyo haki za Mtoto zimekiukwa katika hadithi hii. (ala.8)
au
5. Mizozo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ni chanzo kikuu cha ukosefu wa amani katika nchi nyingi za Afrika Mashahriki. Dhihirisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea madhara ya vita vya kikabila na suluhu yake kwa mujibu wa Mkimbizi na John Habwe ala 20
SEHEMU YA D: FASIHI SIMULIZI.
6. (a) Mivigha ni nini (ala.2)
(b) Fafanua sifa zozote sita za mivigha. (ala.12)
(c)Mivigha ina Majukumu yapi katika fasihi simulizi? (ala.6)
SEHEMU YA E : USHAIRI
7. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ameumbuwa mwanadamu,kwa lililo zuri umbo,
Basi si wote fahamu, waliyo na sawa mambo,
Wako waliyotimamu, na wengineyo wa kombo
Na mtu kuwa na tumbo, si kwamba mekamilika.
Kuna walo mafidhuli, lugha yao ni matango,
Na kuna wenye kauli, zisokuwa na ushingo,
Kuna wake kwa wavuli, vipofu na wenye tongo,
Na mtu kuwa na shingo, si kwamba mekamilika.
Kuna walo na fikira, na wenye vibovu vitwa,
Kuna walo na subira,husubiri kucha kutwa,
Wengine tabiya ya bora, hino huwanayo katwa,
Na mtu kuwa na kitwa , si kwamba mekamilika.
Kukamilika kwa Mja, ni mbali na kwa moliwa,
Kwa Mja nitakutaja, ili upate kwelewa,
Ni kufikiya daraja, ile aliyoumbiwa,
Hapo ndipo huambiwa, Mja amekamilika.
Aiyelewe duniya, kwa marefu na mapana,
Azipite zile ndiya, za miba mitungu sana,
Avuke bahari piya, zito na virefu vina,
Hiyo ni yangu maana ya mja kukamilika.
Akishafikwa na hayo, si kwamba ndiyo akhiri,4
Lazima awe na moyo, wa kuweza kusubiri,
Kuyasubiri ambayo, yote yatayomjiri,
Kama huyo tamkiri, ni mja mekamilika.
Maswali.
(a)Kulingana na shairi hili ni yapi humfanya mtu kuwa na utu. Taja matano (ala. 5)
(b) Fafanua namna mshairi alivyofaulu kutumia uhuru wake ( ala.4)
(c) Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika shairi ( ala 3)
(i) Vibovu vitwa.
(ii) Tabiya Bora
(iii) Mtu kuwa na kitwa
(d) Msanii anakiri nini kuhusu Mja? ( ala.2)
(e) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari ( ala.4)
(f) Eleza Umbo la shairi hili kwa kuzingatia mizani na vina (ala.2)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers