Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Mutomo/Ikutha Districts Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Mutomo/Ikutha Districts Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
JINA: .................................................................................... NAMBA YAKO: ..................................
SHULE ………...................................................................... TAREHE: .............................................
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
MUDA: SAA 2½
TAMTHMINI LA PAMOJA WILAYA YA MUTOMO/IKUTHA - 2011
Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Sekondari Kenya (K.C.SE)
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
MUDA: SAA 2½
MAAGIZO
karatasi hii ina kurasa 10 watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
1. SEHEMU A: UFAHAMU (Alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yote
Mgomo uliingia siku ya tano.
Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu.
Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu
vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake.
Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake
walioachwa pweke vilisikika.
‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja.
‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume
wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’
Mjini kulikuwa na vilio vyake.
‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje?
Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja.
‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’
Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu.
Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani.
( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed)
MASWALI
1. Toa anwani mwafaka kwa makala haya. (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………………..
2. Thibitisha kuwa asubuhi hiyo ilikuwa mbaya. ( alama 1)
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
3. Mauaji ya Makame yalikuwa ya kikatili. Eleza. (alama 4)
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
4. ‘Kufa kwa wengi arusi’. Thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea taarifa uliyosoma.(alama 4)
……………………………………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………………………..
5. Watu walikamatwa kwa nini? (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
6. Kwa nini wasaliti hawakupata nafasi yao kusaliti ? (alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………………..
…………………………………………………………………………………………………………..
7. Eleza maana ya (alama 2)
i) makuli
…………………………………………………………………………………………………………..
.………………………………………………………………………………………………………….
ii) Ukimuathiri
………………………………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………….
2. SEHEMU B: UFUPISHO (Alama 15)
Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo
yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba.
Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu.
Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo.
Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu.
Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa
Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa.
Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao.
Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya.
Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa upitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi
haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri.
a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo
(maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 )
Nakala chafu/maadalizi
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
Jibu
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho
(maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko)
Nakala chafu
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
Nakala Safi
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
3. SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
a) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3)
(i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Mti ulikatika ukaanguka
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4)
Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2)
(i) Onea
………………………………………………………………………………………………………..
(ii) Umia
………………………………………………………………………………………………………...
d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2)
Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa
© 2011,Mutomo/Ikutha District Exam 8
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4)
Sauti ghuna na sauti sighuna
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3)
Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2)
“Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2)
i. Posa
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
ii. Poza
……………………………………………………………………………………………….………..
………………………………………………………………………………………………………..
i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano
(alama 4)
i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4)
Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2)
Nguo zote zimekaushwa na jua
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2)
Nomino kuwa kivumishi
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
m) Andika kwa wingi (alama 2)
Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2)
Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1)
Asiye na nadhari…
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1)
Kwenda mbago…
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
4. SEHEMU D: ISIMU JAMII (Alama 10)
a) Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii
(alama 4)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
b) Lugha huchangia vipi kuleta
(i) Utengano katika jamii (alama 3)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Utangamano katika jamii (alama 3)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
More Question Papers