Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2010



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2010
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
MTIHANI WA LAICOMET KIDATO CHA NNE
Kenya Certificate of Secondary Education 2010
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULAI / AGOSTI 2010
MAAGIZO
_ Jibu maswali manne pekee.
_ Swali la kwanza ni la lazima.
_ Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani;
(Tamthilia, riwaya, na fasihi simulizi.
_ Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
TAMTHILIA
KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA
1. Lazima
….Huenda watu watanung’unika hapa na pale. Hata hivyo watanung’unika kwa muda mfupi,
kisha watanyamaza ……
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(ii) Taja sifa za msemaji. (alama 4)
(iii) Huku ukirejelea tamthilia, onyesha jinsi wanawake walivyodunishwa. (alama 12)
USHAIRI (JIBU SWALI LA PILI AU LA TATU)
2. HISIA
Ewe hisia!
Umeniamshia ndoto niloisahau zamani,
Umelimsha mwangu moyoni,
nyimbo ya kale,
na mdundo usomuutia,
ila hayawani wa mwangu rohoni,
Tulia sasa tulia,
Hebu tulia ewe hisia ulo mtimani,
Nakataa katu kusisimka,
kwa sauti yako laini,
Kwani njia zetu ni panda,
daima hazioani,
Umesubutu vipi kuniita,
kutoka mwako ngomeni,
ulimosahauliwa tarifu zawaru,
Basi yawache maombulezi yako yaso maoni,
yawateke hao mashujaa wa kale,
watu walo kaburini.,
Hebu tulia usiniingilie,
Usinihanfaishe,
Kukuandama katu haimkini,
Kwani hata sasa…. Kwa kukuwaza tu dakika hini,
naona majuto ya mbali moyoni
kama kwamba nimegawa wangu wakati
na wazimu, majinuzi
Basi nenda zako hisia…shuu…hebu tokomea.
Maswali
a) Huu ni utungo wa aina gani? (Alama 2)
b) Kwa kutoa mifano fafanua sifa zinazoufanya utungo huu kuwa shairi. (alama 4)
c) Eleza mawazo ya mshairi katika shair hili. (alama 5)
d) Taja na ueleze mbinu tatu za kifasihi katika shairi hili. (alama 6)
e) Andika maneno yafuatayo kwa lugha sanifu. (alama 3)
(i) Nililosahau
(ii) Umesubutu
(iii) Mtimani
3. JEMBE
Jembe wangu nifariji, nami nikupe uzima
Jembe wewe ndiwe taji,twakuenzi zote dhima
Jembe wewe nipe mpaji, wa baba na kina mama
Jembe wewe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga
Jembe wewe msifika, utuonee huruma,
Jembe shamba tukifyeka, njoo ufanye kulima,
Jembe njoo pasi shaka, ukija lete mtama,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga
Jembe kwetu ukifika, tunapate usalama,
Jembe kote umeshika, ukweli tausema,
Jembe yakija masika, nawe fika nyuma nyuma,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Jembe jua likitoka, nawe usife mtima,
Jembe usije kuchoka, au kupatwa na homa,
Fanya bila kukongoka, fanya usirudi nyuma,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Mola akupe hakika, usende kamwe mrama,
Nenda upate kufika, kama tunavyokutana,
Sote huko tukifika, tutaishi kwa neema
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga
Maswali
(a) Ni mbinu gani ya sanaa ya uandishi inayotawala katika shairi hili (alama 2)
(b)Eleza maana ya mishororo ifuatayo kama inavyojitokeza katika shairi hili;
(i) Jembe wewe ni mpaji, wa baba na akina mama. (alama 1)
(ii) Jembe shamba tukifyeka, njoo ufanye kulima. (alama 1)
(iii) Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga. (alama 1)
(iv) Jembe usije kuchoka au kupatwa na homa. (alama 1)
(c) Fafanua dhana ya jembe katika kila ubeti . (alama 5)
(d) Andika maneno mengine yenye maana sawa na; (alama 5)
(i) mtima
(ii) kukongoka
(iii) pasi
(iv) mrama
(e) Eleza umbo la shairi hili. (alama 5)
RIWAYA: UTENGANO (JIBU SWALI LA 4 AU LA TANO)
4. Juhudi za wanawake kujikwamua zinasambaratishwa na wanawake wenyewe. Jadili
(alama 20)
5. ‘Mjinga huja akawa mwerevu akajutia werevu wake.’
a) hakiki muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Msemaji alikusudia kumwambia nini mzungumziwa? (alama 6)
c) Maneno haya yanahusianaje na maudhui ya riwaya hii? (alama 10)
SEHEMU HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI (k.w Wamtila)
6. “Kuna majabali yasiyokwewa na mijusi na mimi Kizito Kibambo ni mmoja wao!”
a) Thibitisha namna kauli hii inavyofaa katika hadithi zozote katika kitabu ‘Mayai Waziri wa waradhi na hadithi zingine” (alama 16)
b) Kwa kutoa mifano miwili onyesha ufaafu wa methali ii kitabuni, ‘maji ukiyavulia nguo yaoge’
(alama 4)
FASIHI SIMULIZI
7.a) (i) Eleza maana ya misimu. (alama 1)
(ii) Kuchipuka kwa misimu kunategemea mambo mengi.Taja matano miongoni mwa haya
(alama 5)
(iii) Eleza umuhimu wa isimu katika jamii. (alama 4)
b) (i) Nini maana ya ngomezi? (alama 2)
(ii) Ngomezi ina umuhimu gani? (alama 5)
(iii) Taja udhaifu wa ngomezi katika kuwasilisha ujumbe katika jamii. (alama 3)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers