Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Mathira District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Mathira District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2010




JINA: ____________________________________________________________
NAMBA YA MTIHANI _____________________
SAHIHI YA MWANAFUNZI ________________
TAREHE: _________________________________
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULAI/AGOSTI 2010
MUDA - SAA 2 ½
MTIHANI WA PAMOJA - MATHIRA
MAAGIZO
a. Jibu mwaswali manne pekee
b. Swali la kwanza ni lazima.
c. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobakia. Yaani,
Tamthilia Riwaya, Hadithi Fupi na Ushairi.
d. Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.
A. FASIHI SIMULIZI
1. (LAZIMA)
(a) Taja aina zozote tano za nyimbo. (alama 5)
(b) Eleza sifa tano za nyimbo (alama 5)
(c) Popoo mbili zavuka mto
i. Tambulisha kipera kilichotajwa (alama 1)
ii. Taja sifa zozote nne za kipera hiki (alama 4)
iii. Taja mbinu zozote mbili zilizotumika katika kipera hicho. (alama 2)
iv. Eleza dhima ya kipera hiki katika jamii. (alama 3)
B. RIWAYA
SA Mohammed: Utengano
Jibu swali la 2 au la 3
2. Kwa kurejelea riwaya ya Utengano, fafanua maudhui yafuatayo. (alama 20)
a. Utengano
b. Nafasi ya mwanamke katika jamii
c. Kisasi
d. Uasi
3. “…………..…… moyo ulimpiga wala hakuweza kujua kwa nini … akamwona jinsi
alivyonawiri na kushiba nguvu; kijana mwenye sura ya kiume ya kuvutia……..”
a. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b. Eleza sifa za mhusika anayewaziwa katika dondoo. (alama 6)
c. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo na utolee mfano. (alama
4)
d. Kwa kurejelea matukio mengine katika riwaya, eleza mifano mitatu ya uozo
katika jamii. (alama 6)
C. TAMTHILIA
Kithaka wa Mberia: kifo kisimani
Jibu swali la 4 au la 5
4. Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao katika tamthilia ya kifo kisimani.
(alama 20)
a. Bokono
b. Atega
5. [Kwa ujeuri] Ungependa! Kwani wewe ni nani ufanye mambo unavyopenda? Wekeni
vikapu chini na mwondoke mara moja!
a. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b. Mbali na mgogoro huu, jadili migogoro mingine inayojitokeza katika
tamthilia ya kifo kisimani. (alama 16)
D. HADITHI FUPI
6. Jadili jinsi maudhui yafuatayo yanavyojitokeza katika Mayai Waziri wa Maradhi na
Hadithi Nyingine. (alama 20)
a. Taasubi ya kiume
b. Ukimbizi
c. Utovu wa nidhamu shuleni
d. Ushirikina
E. USHAIRI
7. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata
SIGOMBEE KIVULIE; Mathias Mnyapala
Ndege akiwa angani, usiseme wangu mie
Mngoje atuwe chini, na ndipo mgombanie
Lakini yupo hewani, tama isikwingie
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Ndege apaa angani, sigombee kivulie
Mnapigana machoni, mwagombea uzuri e
Mwalizana kama nyani, matunda mwagombeae
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Shika awe mkononi, ndipo ukajivunie
Umshikapo mwilini, chukua kajifugie
Kama utavyo moyoni, kufuga ama mwachie
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Usimlilie nyuni, kwanza akukaribie
Na sauti mdomoni, aimbapo usifie
Saburi ndicho kiini, kila jambo sivamie
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Mwaingia ushindani, kwa magumi mpanie
Ninyi nyote ufukani, ndege juu muanie
Ndege atatua lini? Pengine ajiendee
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Siingie ujingani, majambo mfkirie
Sirukie kifanani, ndege juu muanie
Utafanywa hayawani, jirani wakubeue
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Atuapo matawini, kwa jicho kuangalie
Awaone dharauni, na mbawa awapigie
Na mate yamo kinywani, katu asiwasogee
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
Kaditama upigani, akheri amuambae
Wawindaji pendaneni, mwachie ndege apae
Lisha aliye tunduni, wa juu sitegemee
Sigombee kivulie, ndege apaa angani.
a. Eleza dhamira ya shairi hili (alama 2)
b. Taja na utoe mifano ya mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi hili. (alama 4)
c. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
d. Eleza jinsi uhuru wa mtunzi unavyojitokeza katika shairi. Tolea mifano jibu lako.
(alama 4)
e. Eleza umbo/muundo wa shairi hili. (alama 4)
f. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi (alama 2)
i. Nyuni
ii. Wakabeue






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers