Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nyahururu District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper
Nyahururu District Mock- Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2010
Jina…………………………………………………………….... Nambari yako……………………....
Shule…………………………………………………………….. Sahihi.................…………………….
Tarehe……………………………….
102/2
KISWAHILI
Karatasi ya 2
(LUGHA)
JULAI/AGOSTI - 2010
MUDA: SAA 2 ½
TATHMINI YA PAMOJA YA WILAYA YA NYAHURURU – 2010
Hati Ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/1
KISWAHILI
Karatasi ya 2
LUGHA
JULAI/ AGOSTI- 2010
MUDA: SAA 2 ½
Maagizo:
1. Jibu maswali yote.
2. Majibu yawe katika nafasi zilizotengwa.
SEHEMU UPEO ALAMA
UFAHAMU 15
MUHTASARI 15
MATUMIZI YA LUGHA 40
ISIMU JAMII 10
JUMLA 80
Karatasi hili lina kurasa 12 zilizo pigwa chapa.
Mwanafunzi angalie kwa makini ili kuhakikisha kuwa
kurasa zote zimepigwa chapa na hakuna maswali yanayokosa
1. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
UFAHAMU
Mengi yamesemwa kuhusiana na nchi kuwa na katiba mpya. Kile ambacho hakibainiki
hasa, ni jinsi ambavyo wanasiasa wetu ,wamejitwalia nafasi ya ukunga na tena ya uzazi na mama mwenye mtoto kutupwa pembeni. Je, huyu si mtoto wa Wanjiku tena?
Huenda visa vya hivi karibuni vinavyohusu familia mbalimbali vikawa na mizizi katika
huyu mwana wa Wanjiku. Si haba unasikia kisa cha baba ambaye amemwua mwanawe na
kumkatakata vipandevipande na kuyaacha yaoze yakiozeana kwa sababu ya msinyo au msakamo.
Akili za binadamu zinapolazimishwa kwenda zaidi ya uwezo wa kawaida, matokeo aidha huwa ni
kuingiwa na wazimu, yaani kupagawa, au kuua bila kukusudia.
Aidha, kuna wengi wengine ambao huyachukua maisha yao wenyewe kwa kutaka
kuondokewa na shida. Hawa husahau kuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni. Si nadra kwa
hivyo kuwa na viumbe wanaojitia kitanzi mara kwa mara ili kuepuka mng’ang’ano wa maisha
yasiyo na tumaini katu. Je, hali hii itaendelea hadi lini?
Muujiza mwingine ni ule wa ubakaji wa watoto na maajuza. Nyanya tena si mpenzi
aliyekusanyiwa watoto na vijana wa kata nzima jioni na wakauzunguka moto wake, na kushiba
ngano zake ambazo zilikuwa hazina mwisho. Si nyanya ambaye zao lake kuu 1ilikua viazi vitamu na njugu karanga kwa minajili ya kuwalisha wajukuu wake jioni, na asubuhi kama ndege kuonja umande wa asubuhi? Leo nyanya anaishi na woga, hawaamini tena wajukuu. Ni wabakaji. Sasa vipi chemchemi ya furaha kugeuzwa simanzi ya huzuni? Wasemao husema, dunia uwanja wa fujo.
Ukizuru magereza yetu ndipo utajua tuna shida katika nchi yetu. Watu wamefungiwa
tumbitumbi. Hadithi zao nazo ni nyingi: uvutaji bangi, wizi wa kimabavu, kuua jamaa, uchopozi na zaidi. Hakuna.mwisho.
Ashakum si matusi, ugonjwa wa “Kidon” umeanza kuwashika ndugu zetu vilivyo.
Asilimia ya watu wanaoshikwa wakilangua dawa za kulevya haisemeki. Wote huwa na jibu
lilelile. Maisha yamekuwa ghali na hapana ila kutumia kila mbinu. Je, hatujaambiwa uhalifu
haulipi chochote?
Kukariri usemi huo wa Leonard Mambo Mbotela na wengine wengi wenye semi kama
hizo wakiwemo wahubiri mbalimbaii ni baraka maana hupunguza makali ya maisha na kutoa
nafasi ya kutabasamu kidogo, ijapo siku moja.
MASWALI (Jumla maki 15)
a) Dokeza visa vyovyote vitatu vinavyoonyesha msinyo kulingana na makala. (Alama 3)
.............................................................................................................................................................
b) Mwandishi wa makala anawalaumu wanasiasa kwa nini? (Alama 2)
.............................................................................................................................................................
c) Nyanya alikuwa na wajibu upi kulingana na kifungu hiki? (Alama 3)
.............................................................................................................................................................
d) Fafanua “Ugonjwa wa kidon’’ (Alama 2)
.............................................................................................................................................................
e) Eleza ni kwa jinsi gani wajibu wa nyanya umegeuzwa na vijana wenyewe (Alama 2)
.............................................................................................................................................................
f) Fafanua msamiati huu kama ulivyotumiwa kwenye makala (Alama 3)
i) Tumbitumbi
.............................................................................................................................................................
ii) Chemchemi

...........................................................................................
iii) Ashakum si matusi
.............................................................................................................................................................
MUHTASARI
Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha jibu maswali.
Sayansi ya lugha kwa mujibu wa matumizi yake katika jamii ni taaluma mpya sana katika
silabasi ya somo la Kiswahili kwa shule za Sekondari. Taaluma hii mpya imeibuka na kuibua hali ya taharuki si kwa wanafunzi, si kwa walimu na si kwa washikadau wote wa kitengo maalum cha kukuza lugha nchini.
Wanapoulizwa sababu ya taharuki yao, jibu huwa ni moja, “Kuku mgeni hakosi
kamba mguuni” Jambo la kimsingi ni kuwa mahuluki hutumia lugha katika shughuli ainati.Aidha ni dhahiri shahiri kwamba katika shughuli hizi kuna matumizi ya lugha — ama maneno kwa sauti au ishara kama zile za vipofu na viziwi.
Lugha itumiwapo katika shughuli au taaluma fulani mahsusi, huwa pana msamiati fulani
wa kipekee unaotawala katika shughuli hiyo. Istilahi hizi ndizo huunda sajili. Mathalani, katika taaluma ya zaraa kuna istilahi kama vile kulima, kupalilia, kuchimba makoongo, kuandaa weu, kupiga matuta, miche, mbegu, mbolea, jembe, koleo, mundu, mifugo, mazao na istilahi nyinginezo. Msamiati kama huu ndio huunda istilahi za sajili ya zaraa.
Mbali na zaraa, kuna sajili nyingine kama sajili ya matangazo ya mpira utibabu,
mazungumzo ya watoto wa mitaani; biashara, sheria na mahakama, dini ya Kikristo, Kiislamu na ya Kihindu na sajili nyinginezo.
Waama, bila lugha matendo yote ya wanadamu yangegonga mwamba na kudorora. Je,
viongozi wangetawala vipi? Wafanya biashara wangenadi vipi bidhaa zao? Walimu
wangefunzaje’? Bila shaka jibu ni moja tu: ingekuwa vigumu sana.
Hivyo basi lugha ni chombo muhimu sana. Katika maisha ya waja. Shime kila mtu,
tuendeleze lugha yetu ya Kiswahili. Tusiwe wendaguu kwani makofi hayalii ila kwa viganja
viwili.
a) Fupisha aya tatu za mwanzo kwa maneno yasiyozidi 60. (Alama 7)
Matayarisho
.............................................................................................................................................................
...........................................................................................
Jibu

b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno yasiyozidi 40. (alama 5)
Matayarisho
.............................................................................................................................................................
Jibu
.............................................................................................................................................................
...........................................................................................MATUMIZI YA LUGHA
3. a) Toa neno moja lililo na sauti tatu za konsonanti mwambata (alama 1)
.............................................................................................................................................................
b) Eleza matumizi yoyote manne ya kiambishi ’ku’ (alama 2)
.............................................................................................................................................................
c) Andika kwa kauli mabanoni (alama 3)
i) Takata (tendesheka) –
.............................................................................................................................................................
ii) Unga (tendama) -
.............................................................................................................................................................
iii) Zoea (tendeka) -
.............................................................................................................................................................
d) 1) Tumia “huku’’ kama (alama 5)
(i) Kivumishi
.............................................................................................................................................................
ii) Kielezi

iii) Kiwakilishi
.............................................................................................................................................................
2) Tumia “ila’’ kama
(i) Kiunganishi
.............................................................................................................................................................
(ii) Nomino.

e) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi (alama 3)
Simba waliojeruhiwa jana walikimbia vichakani
.............................................................................................................................................................
f) Andika kinyume cha sentensi hii.
Walizama walipokuwa wakikusanya mchanga. (alama 2)
.............................................................................................................................................................
g) Tambua kijalizo katika sentensi ifuatayo
Ali alikuwa mwalimu. (alama 1)
.............................................................................................................................................................
.............................................................................................................................................................
h) Ainisha
HATUTAWAPIGISHA (alama 3 ½ )
.............................................................................................................................................................
i) Eleza maana mbili za
Aliletewa ng’ombe na mtoto wake (alama 3)
.............................................................................................................................................................
j) Kamilisha jedwali (alama 3)
Kitenzi Kivumishi
Potea
Karimu
Dhuluma
k) Andika ukubwa wa sentensi
Mwana mwenye kichwa kikubwa ataadhibiwa. (alama 2)
.............................................................................................................................................................
l) Bainisha aina ya kirai kilichopigwa mstari
i) Waalimu wa kigeni watawasili leo (alama 2)
.............................................................................................................................................................
ii) Mkimbiaji alikimbia kasi mno ajabu (alama 2)
.............................................................................................................................................................
m) Akifisha
Tulikuwa watu watatu wanaume wawili na mwanamke mmoja (alama 1)
.............................................................................................................................................................
n) Eleza maana tatu za neno “kuta’’ (alama 1 ½ )
.............................................................................................................................................................
o) Yakinisha
Asipobisha hatafunguliwa (alama 1)
.............................................................................................................................................................
p) Andika kwa wingi
Upanga wa mjomba ulikuwa umetiwa makali (alama 2)
.............................................................................................................................................................
q) Onyesha aina za shamirisho katika sentensi hii
Hasani amechapishiwa na kampuni riwaya (alama 2)
.............................................................................................................................................................
...........................................................................................
r) Andika kwa usemi halisi
Njoroge alisema alikuwa amepata alama zote katika mjarabu wa siku iliyotangulia
11
(alama 2)
.............................................................................................................................................................
...........................................................................................
4. ISIMU JAMII
Huku ukitoa mifano, orodhesha mambo yoyote matano yanayoleta makosa katika kutumia lugha
(alama 10)
.............................................................................................................................................................
...........................................................................................
MWISHO
More Question Papers