Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nyahururu District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper
Nyahururu District Mock- Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2010
102/3
KISWAHILI (FASIHI)
KARATASI 3
JULAI 2010.
SAA 2 ½
TATHMINI YA PAMOJA YA WILAYA YA NYAHURURU – 2010
Hati Ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/3
KISWAHILI FASIHI
KARATASI 3
JULAI/AGOSTI 2010.
SAA 2 ½
1. Jibu maswali manne.
2. Swali la kwanza ni la lazima.
3. Jibu maswali hayo mengine matatu kutoka sehemu zingine.
4. Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa wanastahili kuona kuwa maswali yote yako na hakuna yaliyooachwa.
SEHEMU YA A. TAMTHILIA – KIFO KISIMANI – Kithaka Wa Mberia.
LAZIMA.
1. “Askari waliokuwa wa Butangi sasa ni askari wa Mtemi Bokono, jamaa zake na marafiki zake’’.
a) Eleza muktadha wa usemi huu (Alama 4)
b) Ni tukio gani lililochochea usemi huu? (Alama 2)
c) Eleza sifa tatu za msemaji. (Alama 6)
d) Usemi huu unarejelea nini kuhusu utawala wa Bokono? (Alama 8)
SEHEMU YA B. RIWAYA – UTENGANO – S.A – Mohammed.
Jibu swali la 2 au la 3
2. ............“ Mbio za sakafuni huishia ukingoni’’ Sauti yake kama radi. “Mbio zako zimefika wapi?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Taja na uthibitishe kwa mifano aina tatu za tamathali za lugha zilizotumika katika
dondoo hili.
c) Taja mbinu ya uandishi iliyotumiwa kusimulia kisa hiki. (Alama 2)
d) Ukirejelea wahusika wowote wanne thibitisha kwamba mbio zao zilifikia ukingoni.
(Alama 8)
3. Eleza huku ukitoa mifano jinsi mbinu ya sadfa na majazi zimetumika kusaidia
kuendeleza maudhui ya riwaya ya utengano. (Alama 20)
SEHEMU YA C.HADITHI FUPI – Mayai waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine
(K.W.Wamitila)
Uteuzi wa Moyoni – Rayya Timammy.
4. “................Nimechoka, basi hakuna la ziada ila uniache..............................’’
a) Weka maneno haya katika muktadha wake. (Alama 4)
b) Anayetoa tamko hili alichukua hatua mbali mbali kuendeleza maisha yake. Taja
na ufanunue hatua tano. (Alama 10)
c) Anayetolewa tamko hili alikuwa na hulka gani? (Alama 6)
5. Eleza uozo wa jamii unavyojitokeza katika hadithi hizi.
a) Mayai waziri wa maradhi (Alama 10)
b) Msamaria mwema (Alama 10)
SEHEMU YA D: FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 6 au la 7.
6. a) Maghani ni nini? (Alama 2)
b) Taja aina nne mbali mbali za maghani kwa kila aina eleza sifa mbili. (Alama 12)
c) Eleza dhima ya maghani katika jamii. (Alama 6)
7. FASIHI SIMULIZI
Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali.
Ee mpwa wangu
Kwetu hakuna muoga
Uoga ukikufikia huenda ni akina mamayo.
Fahali tulichinja ili uwe mwanamume.
Wewe mpwa wangu kisu ni kikali ajabu.
Iwapo utatingiza kichwa.
Uhamie kwa wasiotahiri.
Wanaume wa mbari yetu.
Si waoga wa kisu.
Wao hukatwa macheo hadi machweo
Iwapo utashindwa.
Wasichana wote.
Watakucheka.
Ubaki msumumu
Sima mmepokea
Ngariba alilala jikoni
Visu ametia makali
Wewe ndiwe wangojewa
Hadharani utasimama
Macho yote yawe kwako
Iwapo haustahili kisu
Jiuzulu sasa mpwa wangu
Hakika tutakusamehe
Mwake kesho unakuja
Asubuhi ndio hii
Mama mtoto aamushwe
Upweke ni uvundo
Iwapo utatikisa kichwa
Iwapo wewe ni mme
Kabiliana na kisu kikali
Hakika ni kikali!
Kweli ni kikali!
Wengi wasema ni kikali!
Mbuzi ataipata
Wa hata shamba la mahindi
Simama Imara
Usiende kwa wasiotahiri.
Maswali
a) Taja a uthibitishe shughuli zozozte za kiuchumi za jamii ya wimbo huu (Alama 4)
b) Nani mwimbaji wa wimbo na anamwimbia nani? (Alama 2)
c) Huu ni wimbo wa aina gani? Thibitisha (Alama 2)
d) Msimulizi wa wimbo huu ana taasubi ya kiume – thibitisha kauli hii (Alama 2)
e) Nyimbo zina wajibu gani katika jamii (Alama 4)
f) Taja mambo yoyote manne ambayo hupambanua muundo wa nyimbo katika jamii
za kiafrika (Alama 4)
g) Ijapokuwa nyimbo ni nzuri zina ubaya wake. Taja mambo mawili yanayoonyesha
ubaya wake (Alama 2)
SEHEMU YA E: USHAIRI
Jibu swali la 8 au la 9
8. 1. Barua yako nadhifu, imewasili mzuri,
Ambayo imenarifu, homa inakuathiri,
Bwana wetu mtukufu, mungu atakunusuri,
Uishi muda mrefu, akupe na afya nzuri,
2. Akupe afya ya mwili, maradhi yajibari,
Tukutane wawili, nikirejea safari,
Ninayemwomba hili, si mkata ni tajiri,
Aweza kubadili, baya likawa zuri,
3. Habari ya uhaini, pia nina ikariri,
Aliofanya mwandani, rafiki yangu msiri,
Sitarudi adhani, lakini bora saburi,
Kwa uwezowe manani, nitarudi Zanzibari.
4. Katika moyo wangu, pendo lilivyoshamiri,
Aelewaye ni Mungu, muelewa wa kila siri,
Walakini mlimwengu, hawezi kulisafiri.
Sidhani mpenzi wangu, kuwa nitaghairi,
5. Nikizidi kuandika, chozi latoka tiriri,
Kwa wingi humiminika, msilinge mistari,
Jawabu lisipofika, kujua yako habari,
Fahamu tasikitika, na kulia nikithiri,
Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa (Alama 2)
b) Andika mambo mawili yaliyotajwa katika barua iliyomfikia mwandishi wa shairi hili.
(Alama 2)
c) Eleza maana ya mishororo ifuatayo.
i) Ninayemuomba hili, si mkata ni tajiri. (Alama 2)
ii) Sidhani mpenzi wangu, kuwa nitaghairi (Alama 2)
d) Eleza uhusiano kati ya mshairi na mwandishi wa barua - (Alama 2)
e) Andika ujumbe wa mshairi kwa mwandishi wa barua - (Alama 4)
f) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Alama 4)
g) Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumiwa katika shairi (Alama 4)
i) Nisilinge.
ii) Mkata
iii) Ghairi
iv) Lilivyoshamiri (Alama 4)
9. Soma shairi Lifuatalo kisha ujibu masawali yafutayo.
1. Vije leo walalama, kwa yale ulotendewa,
Huyakumbuki ya nyuma pindi ulipochachawa
Ulipotenda unyama, uliona ndiyo sawa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
2. Ulizusha uhasama, leo wewe wapagawa
Walia bila kukoma, tungadhani umefiwa
Sasa huna usalama huwezi kujiopowa
Mtenda akitendewa hulalama kaonewa!
3. Tenda mambo kwa kupima, usiruke huna mbawa
Una macho kutazama, na akili umepewa
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa!
4. Dunia haishi njama,sijione umepewa
Ukadhani usalama, binadamu kuwagawa
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.
5. Unapotenda zahama, siku yako itakuwa
Ambapo utaungama, useme umechachiwa
Na uanze kutetema, ulie umeonewa
Mtenda akitendewa, hulalama kaonewa.
Maswali
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka . (Alama 2)
b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2)
c) Eleza muundo wa ubeti wa pili. (Alama 4)
d) Ni kaida zipi za utunzi zilizozingatiwa na mshairi? (Alama 2)
e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (Alama 4)
f) Toa mifano miwili ya idhini ya mshairi. (Alama 2)
g) Kwa nini msemewa hafai kulalamika . (Alama 2)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo.
i) Uhasama
ii) Umepowa (Alama 2)
MWISHO
More Question Papers