Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nyamira North District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Nyamira North District Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2010
Jina.........................................…………………………................ Nambari.....…….................................
Shule .......………………….......................................................... Sahihi………………………………..
Tarehe.................................................
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA 2
LUGHA
JULAI/AGOSTI 2010
MUDA: MASAA 2 ½
TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA NYAMIRA KASKAZINI
Hati ya Kuhitimu Kisomo cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI 2
JULAI/AGOSTI 2010
MUDA: MASAA 2 ½
MAAGIZO:
1. Jibu maswali yote
2. Andika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa.
Hakiksha kuwa kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo
1. UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Tukilinganisha maisha ya zamani na ya siku hizi tutaona kwamba mambo mengi sana
yamebadilika. Si watu wazima, si watoto; sote tumeathirika si haba. Mitindo mipya ya kimaisha na mazingira yanayobadilika kasi ni baadhi tu ya mageuzi haya. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitizamo, mawazo na mielekeo tu bali katika vipengele vingi vingine.
Mavazi ya zama hizo yalikuwa yakitengenezwa kutokana na maganda ya mti au ngozi za
wanyama kama vile mbuzi, kondoo, punda, ngamia, ng’ombe na hata pengine wanyama wa
mwituni. Kwa vile kila mtu alifuga wanyama wengi, hakukuwa na shida ya kuzipata ngozi kama
hizo wakati wowote ule haja itokeapo. Magome ya miti yalipatikana mwituni – na kwa kuwa
katika enzi hizo hakukuwa na hifadhi za wanyama wa mwitu wala miitu yenyewe, watu waliweza
kuingia katika pori lolote na kubambua maganda au kuua wanyama kama walivyohitaji. Mavazi
yalikuwa rahisi kupatikana kuliko zama zetu; licha kwa upande wa ndarama, hata kwa upande wa sheria pia. Zaidi, katika enzi hizo watu hawakujali kwenda uchi au walipachika kipande tu cha vazi mwilini. Siku hizi gharama ya maisha imepanda mno.
Siku hizi hatuwezi kuwaua wanyama wa mwituni vururu mtende eti kwa chakula, kama
walivyofanya babu zetu. Enzi hizo matunda yalining’inia mitini na njaa zilikuwa si nyingi.
Chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo. Vinywaji vilikuwa kwa mpango – wazee wa ngambi
walikuwa na vinywaji vyao; wazee wa kawaida, wanawake na watoto hirimu hawakusahauliwa.
Watu waliheshimiana; vijana walikuwa wenye adabu na walifahamu fika kuwa walipaswa
kuwaheshimu wakubwa kwa vyovyote vile. Siku hizi vyakula ni haba na ghali na vingi vyazua
magonjwa tata.
Siku hizi kuna weledi wengi, hasa wa sayansi. Mja akitaka kwenda safarini huchukua
kidubwasha fulani na huyoo! Kaenda zake; barabarani, angani au hata katikati ya kilindi cha
bahari. Leo twajivunia ujuzi na maendeleo ya kiafya na madawa yapunguzayo mno unyofu wa
binadamu lakini bado kuna pengo kubwa kati ya vikongwe na watu wa makamo, kinyume na
zama hizo. Maisha ya karne hii yamekuwa kama zile nguo ziitwazo“bwaga – mtwae’’, ambazo
hazibali kufumka au kukwajuka.
Hivi leo, mtu akiumwa na kichwa hukimbilia kwa daktari. Mwingine akiumwa na nyoka
popote pale, hukimbilia hospitalini akapate sindano ambayo hata jina lake halijui. Zamani
ilikuwa mtu achimbechimbe mizizi ya upuzi upuzi, aitafune na alipata nafuu! Wa kisasa
twawapuuza wa kale eti hawakujua elimu ya usafi tuijuavyo sisi, ilhali walikuwa wakiichoma
miili ya watu waliokuwa wamekufa kwa ukoma au kifua kikuu. Wakati mwingine walikihama
kijiji kilichoingiliwa na maafa ya ndui. Hata sasa wagonjwa kama hao hutengwa hospitalini huku maradhi kama vile UKIMWI bado yakikosa tiba.
Mengi tuliyonayo sasa, mathalan tarakilishi na eropleni yalivumbuliwa au kugunduliwa na
hao wa zamani. Fanaka zetu zote na ustawi tulionao asili yake ni watu hao wa zamani. Akili ni mali na kila mtu ana zake. Kuongezeka kwa watu duniani, mchanganyiko au matumizi mabaya ya madawa mengi pamoja na uchafuzi wa hali ya anga pia yameongezea kuleta hasara kubwa. Kweli sikio haliwezi kushinda kichwa.
(a) Kulingana na mwandishi, kwa nini maisha ya kale na ya sasa hayalingani? (alama 3)
.............................................................................................................................................................
(b) Kupata mavazi zama zile kulikuwa nafuu. Toa sababu. (alama 2)
.............................................................................................................................................................
(c) Kwa kusema siku hizo, ’chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo,’ mwandishi anamaanisha nini?
(alama 2)
.............................................................................................................................................................
(d) Taja sababu za magonjwa na maafa kukithiri siku hizi licha ya hatua kubwa katika elimu na afya.
(alama 3)
.............................................................................................................................................................
(e) Fafanua usemi, ’sikio haliwezi kupita kichwa’ kwa mujibu wa taarifa. (alama 2)
(f) Eleza maana ya:
(i) Magome –
(ii) Vururu mtende –
(iii) Hazibali - (alama 3)
2. UFUPISHO
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali.
Ukimwi ni ufupi wa ukosefu wa kinga mwilini. Uwele huu ni wa zinaa ambao hauna tiba, dawa
wala kafara. Insi anaweza kupata wiche ya ukimwi kwa njia ainati. Mathalani ni; kujamiiana
baina ya mwanamume na mwanamke japo wote au mmoja ana wiche ya virusi vya ukimwi. Nina
aliyehimili anaweza kumtia wiche mtotowe akijifungua au kwa kumnyonyesha. Katika harakati
na mikakati ya kutoa damu, au ngeu hiyo kuchangamana na jeraha nyevu. Cheche akilia mfiche
kuku, ama fisi akimia mwele funga mlango.
Tuupige ukimwi vita shadidi, kwani si lelemama. Tutahadharike kabla ya athari kwani hadi sasa hakuna tiba hususan, ya uwele huu. Tarakimu zinabainisha kwa kina kuwa vijana wengi ndio wanaoathirika. Wengi wao wamefufutika na kugugunwa wakabakia mifupa. Hali kama hii
ikishitadi kujiradidi nchi hii yetu itakosa viongozi wa mustakabali.
Wimbo mui hauongolewi mtoto. Wazazi wanafaa kuwa kielelezo chema kwa wana wao. Mwana
akibebwa hutazama kisogo cha ninake. Ni jambo la fedheha na kukereketa mtima kuwaona
baadhi ya wazee wakichana mtaani vipara moto. Vijana hutegwa kwa chachu na kunaswa kwa
ulimbo. Pengine huingia mitegoni kwa ghiliba chache tu za pesa nane. Enyi vijana jihadharini!
Wazee hawa ni vitaange watawatosa demani.
Mila na tamaduni nyingine zimepitwa na wakati. Wala hazina nafasi katika dunia ya sasa.
Tunafaa kutembea na wakati kwani tusipoukata utatukata. Swala la kuingia mafa wajane
wafaruku limekita mizizi miongoni mwa makabila humu nchini. Hili ni swala nyeti linalohitaji kuvuliwa nguo livaliwe nduruga. Serikali sharti iingilie kati na kukata kauli kuukomesha uozo na uvundo wa namna hii.
Ukata na uchochole umechangia pakubwa katika kuupalilia mbolea ukimwi. Kwa sababu ya
uchechefu wa fulusi za karo, shababi wengi hawamudu kuendelea na masomo. Kitembo cha elimu
hakikiuki elimu ya msingi. Zaidi, mwanamume wa kisasa ambaye bado amefungwa pingu na
taasubi za kiume hapendezwi na hali hii na huuma kidole akitamani ya kale. Shingo upande
analazimika kukubali kuwa mabadiliko ni jambo la aushi.
Mla kunde hunya kunde. Vijana lazima watahadharishwe na malimwengu. Wasije kufa na laiti
ningalijua, na chanda kili kinywani. Wengi wamezizika mila na tamaduni katika kaburi la sahau.
Hawaoni hawasikii kwa sababu hawana ashiki. Wameuvua utu wakajivika uchu. Matongozi
yamejaa tadabui tena, masikio yamejaa komango yasiweze kusikia.
Ukimwi unawagegeda na kuwakeketa kama umwa. Utamu unapoisha wanatemwa na kutiwa
mavani kama makapi. Wanafaa kuaswa waasike kwa maaso yenye adili. Ulimwengu kokwa ya
fuu haiishi utamu, anayeisha ni binadamu.
Maswali
(a) Fupisha ujumbe unaojitokeza katika aya tano za kwanza za makala haya. [Maneno 50 – 60]
[Alama 8,2 za utiririko]
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
Jibu
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(b) Katika aya za sita na saba, mwandishi anawashauri waja. Toa nasaha hiyo. (Maneno 35 – 45 )
(Alama 7, 1 ya utiririko)
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………….........
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
………………………………………………………………………………………………………
Jibu
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
3. MATUMIZI YA LUGHA
(a) Akifisha kifungu kifuatacho. (alama 3)
nilipowasili tu nilishika tama nikashangaa loo moto huo ulianza vipi na ulikuwa umesababishwa
na nini nilishikwa na bumbuwazi magoti yangu yakaanza kuchezacheza.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(b) Tunga sentensi moja katika umoja kisha uigeuze ili iwe katika wingi ili kudhihirisha ngeli ya
LI – YA. (alama 2)
(i) ……………………………………………………………………………………………………
(ii)……………………………………………………………………………………………………
(c) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali. (alama 2)
Baba anafyeka nyasi ilhali mtoto anaambua viazi
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(d) Andika katika msemo wa taarifa: (alama 4)
Zainabu : Aa! Mbona umeketi peke yako kaka?
Wenzako wajistarehesha huku na huko, wewe umekaa pweke, kwa nini?
Una mkasa gani?
Kagame: Sina mkasa wowote, dada, ila nasumbuliwa na ugeni tu. Niliwasili
hivi juzi na sijapata sahibu hata mmoja, ndiyo sababu ukaniona
katika hali hii ya upweke
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(e) Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana.
(i) Mtume mwenye wamefika ni mrefu. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Twiga hukimbilia mbio ingawa ni ndefu. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
(f) Andika kwa wingi: (alama 2)
(i) Uta uu huu ndio aliotumia kumfuma swara.
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Ugomvi wake ulisababisha kutalikiwa kwake
………………………………………………………………………………………………………
(g) Unda nomino mbilimbili kutoka kwa vitenzi: (alama 2)
(i) Fuata
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Zika
………………………………………………………………………………………………………
(h) Bainisha maana katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
(i) Isije ikawa Maria anahusiana naye
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(ii) Huenda ikawa amepitia njia nyingine.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(i) Andika upya ukitumia – o –ote (alama 2)
7
(i) Kitabu kikipendwa na wasomaji wengi huwa maarufu.
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kila askari apitaye hapo humchapa.
………………………………………………………………………………………………………
(j) Tunga sentensi moja itakayodokeza matumizi mawili tofauti yas kiambishi ’ka’ (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(k) Badilisha hadi katika hali ya udogo. (alama 2)
(i) Uta..........................................................................................................................................
(ii) Kijiko.......................................................................................................................................
(l) Toa maana mbilimbili kwa kila moja ya maneno haya: (alama 2)
(i) Kata
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(ii) Ua
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(m) Andika sentensi ifuatayo katika umoja. (alama 2)
Nyua zenu zanuka kwa sababu hamzitumii kwa uangalifu.
………………………………………………………………………………………………………
(n) Tunga sentensi moja sahihi ukitumia kivumishi kimilikishi. (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
(o) Bainisha wakati na hali katika sentensi: (alama 2)
Utakapofika nitakuwa nimekula.
………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………........
(p) Iandike upya sentensi ifuatayo ukifuata agizo. (alama 2)
Hakika Mogeni alimcharaza mno Manoti, lakini sidhani kuwa kichapo pekee kingepelekea
aliyetwangwa kulazwa hospitalini:
(Anza: Sidhani...........................)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(q) Eleza maana za: (alama 1)
(i) Kuteka nyara
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kujenga nyumba za karata (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(r) Taja methali moja inayofungamana na maelezo yafuatayo: (alama 1)
Wakati mwingine mtu hujikuta au hupatikana asipotarajiwa, asipokusudia ilhali hana makosa au hitilafu yoyote.
………………………………………………………………………………………………………
(s) (i) Kanusha:
Waimbaji walio maarufu wamepata tuzo. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Andika kinyume cha sentensi:
Mama alimeza dawa yote. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII
(a) Pambanua sifa zozote sita za lugha rasmi (alama 6)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
(b) Ni mambo yapi yanayotambulisha sajili ya vijana? (alama 4)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………….........
MWISHO
More Question Papers