Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nyamira North District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Nyamira North District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2010



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
JULAI/AGOSTI - 2010
MUDA: MASAA 2 ½
TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA NYAMIRA KASKAZINI
Hati ya Kuhitimu Kisomo cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
JULAI/AGOSTI - 2010
MUDA: MASAA 2 ½
Maagizo
• Jibu maswali manne.
• Swali la kwanza ni la lazima.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu B.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa wanastahili kuona kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU A: TAMTHILIA
1. (LAZIMA)
KIFO KISIMANI – Kithaka wa Mberia
“Kazi ya mikono yangu mwenyewe. Nimeuchomoa mwiba tayari. Kisu kilimpata vizuri tumboni.
Pengine kwenye ini au wengu. ”
(a) (i) Liweke dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
(ii) Ni mambo yapi yaliyomfanya mnenaji hata kuuchomoa mwiba? (alama 6)
(iii) Taja na ueleze mbinu ya uandishi inayoibuka katika dondoo hili. (alama 2)
(b) Huku ukitolea mifano mwafaka, onyesha migogoro yoyote minne inayojitokeza katika
tamthilia “Kifo Kisimani. ” (alama 8)
SEHEMU B: RIWAYA
UTENGANO – S.A. Mohamed.
2. Wanawake wengi katika jamii ya “Utengano’’ wamesawiriwa kuwa waovu. Thibitisha kauli hii.
(alama 20)
3. “...... ni wewe. Nilikutarajia. Nilikuwa nakusubiri kwa hamu. Ndiyo...... nitafanya kama
ulivyoagiza..... yah, nitamlipa. Lakini kesi yake mbaya..........’’
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Eleza sifa zozote sita za mhusika huyu. (alama 6)
(c) Fafanua maudhui yanayodokezwa na dondoo hili (alama 4)
(d) Dhihirisha matumizi ya mbinu zifuatazo katika riwaya ya utengano: (alama 6)
(i) Taharuki
(ii) Kisengere nyuma
(iii) Kinaya
SEHEMU C: USHAIRI (alama 6)
(Jibu swali la 4 au la 5)
4. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Bahari
1. Bahari uzuri, wake tawambia,
Sifa tabashiri, kuwahadithia,
Ambazo ni nzuri, na faida pia.
2. Na faida pia, na kwamba ujue
Nakukuelea, nawe utambue,
Na sasa sikia, uzifafanue.
3. Uzifafanue, bahari za pambo,
Lenye uzuriwe, pia ni urembo,
Ni siri ujue, na pia ni tambo.
4. Na pia ni tambo, ni siri yakini,
Aidha ni fumbo, haiwezekani,
Ina mengi mambo, yenye na thamani.
5. Yenye na thamani, kwa watu wa pwani,
Nawapa yakini, nanyi sikizani,
Humo baharini, kwanza pulikani.
6. Kwanza Pu1ikani, lulu twaipata,
Samaki yakini, faida huleta,
Aidha wendani, pia huokota.
7. Pia huokota, ambari zinduna,
Munyu na mafuta, vinapatikana,
Faida yaleta, pulikiza sana.
8. Pulikiza sana, tia sikioni,
Tija ya maana, ilo baharini,
Imepatikana, kwa kila ya fani.
9. Kwa kila ya fani, samaki twauza
Mapezi yakini, ya papa sikiza,
Huleta thamani, yenye muangaza.
10. Yenye muangaza, pia na forodha,
Pato huongeza, Ia kuleta fedha,
Pia yaangaza, bahari kwa adha.
11. Bahari kwa adha, adhaye upepo,
Hapana orodha, na ichafukapo,
Huondoka ladha, tena hapo ndipo.
12. Tena hapo ndipo,- chombo hutotoma,
Nyote muliopo, hapana msema,
Ndipo muliyapo, “Mama, yoo mama!”
MASWALI
(a) Shairi hili ni la bahari gani? Toa ithibati. (alama 2)
(b) Taja faida mbili na hasara mbili za bahari kama anavyoeleza mshairi. (alama 4)
(c) Kwa kuzingatia beti mbili za mwisho, eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
(d) (i) Eleza vile uhuru wa kishairi ulivyotumika katika shairi hili. (alama 4)
(ii) Andika ubeti wa tano katika lugha nathari. (alama 3)
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. (alama 3)
(i) Pulikeni
(ii) Tija
(iii) Adhaye
5. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Natunga nikiwaasa, msije kujijutia,
Mitego sije wanasa, mkaja kuangamia,
Tamaa nyingi za pesa, gereza zitawatia,
Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza.
Jela inakukonyeza, kama hutajizuwia,
Haina ndugu gereza, jela si kuchezea,
Inajuvya na kupoza, wenye nguvu kutulia,
Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza.
Rushuwa si kitu chema, walaji jihadharini,
Mkila zitawakwama, zitawatoka puwani,
Wazilao hulalama, si mimi ila Fulani,
Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza.
Ridhika na upatacho, kama moja au mbili,
Usitaraji mkocho, apatao Bwana Ali,
Tamaa zako za macho, zitakuletea mbuli,
Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza.
Nimeona kemu kemu, wenye vyeo kutimia,
Maleba wakiwahimu, rushuwa kuwaletea,
Muogopeni Karimu, beba haombwi rushuwa,
Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza.
Kuna wengi mahakimu, haki wanazopinduwa,
Yatima kuwadhulumu, kwa kupapia rushuwa,
Kwa kutaka darahimu, aso haki anapewa,
Kila mpenda rushuwa, jela inamkonyeza.
MASWALI
(a) Andika anwani mwafaka kwa utungo huu. (alama 2)
(b) Taja athari tatu za rushwa kama zilivyoelezwa katika shairi. (alama 3)
(c) Ni nini msimamo wa mwandishi kuhusu rushwa? (alama 2)
(d) Andika ubeti wa pili katika lugha sufufu. (alama 4)
(e) Eleza sifa nne zinazotambulisha utungo huu kuwa ni shairi. (alama 4)
(f) Huku ukitoa mifano, onyesha namna uhuru wa mshairi unatanda katika shairi hili. (alama 2)
(g) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (alama 3)
(i) Kupapia
(ii) Nikiwaasa
(iii) Inamkonyeza
SEHEMU D: HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE – K.W. Wamitila
6. Mwanamume amechorwa vipi katika hadithi zifuatazo?
(a) Ngome ya Nafsi
(b) Kuchukua Hatua Nyingine
(c) Uteuzi wa Moyoni (alama 20)
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
7. (a) Chambua vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi: (alama 8)
(i) Soga
(ii) Hodiya
(iii) Misimu
(iv) Ngomezi
(b) Onyesha dhima ya methali katika jamii. (alama 4)
(c) Taja na ueleze aina nne za ngano. (alama 4)
(d) Eleza miundo yoyote minne ya vitendawili. (alama 4)
MWISHO






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers