Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Busia District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Busia District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni ya lazima
• Maswali hayo mengine matatu kutoka sehemu nne zilizobaki yaani, Riwaya , na HADITHI
Fupi.tamthilia, fasihi Simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A: U SHAIRI.
1. LAZIMA
Soma shairi lifuatalo kwa makini,halafu ujibu maswali yanayofuatia.
Hakika yamekithiri, ni nani asoyajua?
Wazazi wayahubiri,na hivyo kutubagua
Hayana komwe fahari,ila kweli yatua.
Uhuru wa kuoana,ni lini tutaupata?
Mwanamke siyo huyo? baba mtu anasema
Mwanamke kwani huyo? anateta naye mama,
Sababu waitoayo, haina nguvu wima,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutampata?
Kabila letu nihili,sharuti uoe huko,
Unazomewa ukali,kuoa nje ni mwiko
Hivyo twafanywa dhalili,viumbe tuso mashiko
Uhuru wa kuoana ,ni lini tutaupata.
Wanachunguza tabaka,ndipo wazushe wahaka
Wauliza kwa haraka,wajue lake tabaka,
Wasioridhika wafika,arudi alikotoka,
Uhuru wa kuona, ni lini tutaupata?
Waichuja yake dini,ndo ndoa ibarikiwe
Lazima yake imani,iwe sawa na yakuwe
Huu kweli ni uhuru,wataka uondolewe,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?
Japo mwanipa elimu,uhuru ninautaka,
Na mie muniheshimu,nipate nilomtaka
Kuoa kitu adhimu, so mchezo kwa hakika
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?
Nawashauri wazazi,twahitaji kupumua,
Wawili ndo waamuzi , hata Mungu anajua,
Wasifu pasi ajizi, kwa yao njema hatua,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?
Ndoa ikivunjikana,wawili wajisakeni,
Isije kusemekana,wazazi ndio kiini,
Ndiposa hata Rabana,situtie lawamani,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?
Aliye na masikio,mesikia kwa makini,
Tusitamani kilio,mithili tulo vitani,
Wakioa sema ndio. Mola asikulaani
Uhuru wa kuoana ni lini tataupata?
Maswali.
a) Lipe shiari hili anwani mwafaka. (ala.1)
b) Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari mbili.Zitaje huku ukitoa sababu ( ala.4)
c) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipolitunga shairi hili?
d) Ni masharti gani kijana nafaa kuyatimiza kabla ya and oa na ambazo mshairi analalamikia
Taja manne. (ala.4)
e) Vijana wanafaa kuchaguliwa mke/mume wa kuoa? Toa maoni yako. (ala.2)
f) Ukizingatia shairi ulilopewa eleza jinsi mtunzi alivyotumia uhuru wake. (ala.4)
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika shairi. (ala. 3)
(i) Wahaka
(ii) Yamekithiri
(iii) Dhalili.
SEHEMU YA B : RIWAYA
S.A Mohamed : UTENGANO
Jibu swali la 2 au la 3
2. “ Riwaya ya Utengano inadhihirisha vile kisasi kimekithiri katika jamii husika. Eleza kwa tafsili
ukitolea mifano mwafaka. (ala.20)
3. “ Si mchezo kwake kujaza chungu cha kumtosha yeye na watoto wake na huyo Shoka, ambaye haleti
chochote kwake lakini hodari wa kungoja kimeshapi kwa apandie”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala.4)
b) Taja ba ufafanue tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (ala.4)
c) Eleza umuhimu wa kisa kinachorejelewa na dondoo. (ala.4)
d) Ukitumia mifano mingine katika riwaya ya Utengano, fafanua maudhui mawili yanayodokezwa
na dondoo hili. (ala.8)
SEHEMU YA C: THAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
Jibu swali la 4 au la 5
4. “……..siyo uongozi wangu! Kamwe siyo uongozi wa mtemi Bokono! Niwaruhusu kuutia nyufa,
abadani siyo mimi! Watakomeshwa. Watakomeshwa wakome walivyo koma kunyonya matiti ya
mama zao….”
a) Eleza muktadha wa maneo haya. (ala.4)
b) Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika kifungu hiki. (ala.6)
c) “Watakomeshwa”. Eleza kwa tafsili maana ya neno hili,ukizingatia tamthilia ya kifo kisimani.
(ala.10)
5 Mhini na mhiniwa njia yao ni moja. Thibitisha ukweli wa methali hii kwa mujibu wa kifo kisimani.
SEHEMU YA D : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI wa MARADHI na HADITHI NYINGINE : K.W Wamitila.
6. Mtoto wakike amesawiriwaje katika diwani ya Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyinginezo.
(ala. 20)
SEHEMU YA E : FASIHI SIMULIZI. (ALAMA 20)
a) (i) Eleza maana ya kitendawili (ala.2)
(ii) Eleza sifa bainifu za vitendawili. (ala 4)
(iii) Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii ( ala.4)
b) (i) Nini maana ya mighani/migani . (ala.2)
(ii) Fafanua sifa nne za mighani. (ala.8)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers