Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Kakamega East District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Kakamega East District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Sahihi .................................... ………………………………………….. Tarehe: ……………..................
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni la lazima
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani:Tamthilia ,
Hadithi fupi,Ushairi na fasihi simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A : RIWAYA
UTENGANO: S.A. Mohamed :
LAZIMA
1. Wahusika wafuatao wakiondolewa katika riwaya ya utengano, ujumbe wa mwandishi hautafikia
wasomaji. Thibitisha kauli hii ukirejelea wahusika uliopewa.
(i)Maksuudi
(ii)Kazija
(iii) Maimuna
(iv) Biti Kocho (Alama 20)
SEHEMU YA B: TAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
2. “Unajua nini, pombe haipendi tumbo tupu. Hupenda tumbo ambalo limewekwa matandiko mazuri.
(i) Nani alitoa kauli hii ? Kwa nini? (Alama 2)
(ii) Pombe ilisusiwa na mtu fulani, Nani ? Na kwa nini ? (alama 4)
(iii) Pombe ilikuja na vitu kadhaa, vitaje pamoja na kusema umuhimu wa kila kimoja. (Alama 6)
(iv) Onyesha sadfa zinazojitokeza katika matukio ya muktadha huu. (Alama 6)
(v) Kutokana na dondoo hili, onyesha udhaifu wa walinzi hawa. (Alama 2)
3. (a) Kwa kurejelea wahusika katika tamthilia ya kifo kisimani, thibitisha vile ambavyo wanawake ni kiini cha ukombozi wa wanabutangi. (Alama 10)
(b) Eleza kwa kutolea mifano mwafaka nafasi ya vijana katika tamthilia ya Kifo Kisimani.
(Alama 10)
SEHEMU C : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE : K.M.Wamitila
4. Kwa kurejelea diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine, thibitisha kuwa ulaghai umeenea sana katika jamii. (Alama 20)
5. “Au ataka mahari yarudishwe” kiingiacho kwa mganga hakitoki babu”
(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
(ii) Onyesha jinsi wanawake walivyodhalilishwa katika hadithi husika. (Alama 10)
(iii) Fafanua athari sita za kudhalilishwa huku. (Alama 6)
SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI
6. (i) Taja mambo yanayopambanua muundo wa nyimbo katika jamii. (Alama 7)
(ii) Eleza wajibu wa nyimbo katika jamii. (Alama 8)
(iii) Ingawa nyimbo ni nzuri zina ubaya wake. Fafanua huku ukitoa mifano. (Alama 5)
SEHEMU E: USHAIRI
7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
DUNIANI husifiki
Wala hupati
Yalisemwa hukumbiki?
Na wazee wa zamani
“Mkono haurambiki
Bila kitu kiganjani.
Wangapi watu azizi,
Fulani bin Fulani,
Waliokichinja mbuzi,
Kukirimu mitaani,
Sasa kama wapuuzi
Kwa hali kuwa ta’bani
Walifanya makubeli,
Wakaapo hadharani
La uongo huwa kweli,
Kubishika kitaani,
Na tangu kukosa mali,
Wamekuwa kama nyani!
Walifanya mahashumu,
Kuwaliko masultani,
Ushehe na ualimu,
Kufasiri vitabuni
Na leo wana wazimu,
Kama si wanachuoni.
MASWALI
(i) Eleza ujumbe wa mshairi (Alama 1)
(ii) Onyesha jinsi mshairi alivyousisitiza ujumbe katika shairi. (Alama 3)
(iii) Eleza kwa tafsili umbo la shairi. (Alama 4)
(iv) Andika ubeti wa kwanza katika lugha ya nathari. (Alama 3)
(v) Onyesha idhini ya kishairi ilivyotumika katika shairi kwa kutolea mifano. (Alama 4)
(v) Toa mifano ya mbinu za lugha zilizotumiwa katika shairi. (Alama 2)
(vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi.
(a) Kukirimu
(b) Makubeli
(c) Mahashumu (Alama 3)
More Question Papers