Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nyamira District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Nyamira District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni lazima
• Maswali hayo mengine matatu kutoka sehemu nne zilizobaki yaani, tamthilia,riwaya , Ushairi na
fasihi simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A: HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI: K.W Wamitila.
1. LAZIMA
“….. Ni…. Nisubiri kidogo mpenzi….. naja hivi punde… tuyamaliza uyasemayo.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
b) Anayosema mnenewa yanaashiria matatizo yanayomkumba. Jadili kwa kutoa mifano kitabuni manne
ya matatizo hayo ambayo pia ni matatizo yanayoikumba jamii. (ala.8)
c) Ni vipi matatizo hayo yanavyoweza kusuluhishwa? (ala.8)
SEHEMU YA B : RIWAYA
S.A Mohamed : UTENGANO
Jibu swali la 2 au la 3
2. “ Shoga Futoni ni Futoni kweli, mambo yake ni mfutofuto, hakuna mtaji mkubwa hata hivyo kwa
mimi na wewe…...”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala.4)
b) Eleza jinsi njia alizotumia kujipatia riziki mnenewa zilivyomtia mashakani (ala. 10)
c) Eleza jinsi mnenewa hakubadilisha maisha yake. (ala.6)
au
3. Huku ukitoa mifano onyesha jinsi mwandishi amefaulu katika matumizi ya mbinu zifuatazo za sanaa:
(i) Rejea (ala.10)
(ii) Sadfa (ala.10)
SEHEMU YA V: USHAIRI
4. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
UTII
Raia Mwema ni yule, aliyejaa utii,
Si ubishi na kelele, akanywalo hasikii,
Ni mwasi huyo jinale, achunguzwe kwa bidii,
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye
Uonapo uhalifu, usambe huuzuii,
Ndio huo uvunjifu, kamawe huzingatii
Mwananchi mwadilifu,hilo halikadirii
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye
Utii kama haupo,sheria haziagii
Imani huwa haipo, na mema hayatujii
Usalama hufa papo, mara nchi ikadhii
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye
Nia za watu watano, ambazo hazififii
Uchao ni tangamano, si chusa hawachukii
Hushinda kumi na tano, ambao hawatulii
Raia asiyetii, ni fasidi wa nchiye.
Kila raia nchini, ni ile au ni hii
Ana hisa wastani,ingawa haitumii
Hazuiliwi hanani,kusema hatumbukii
Raia asiyetii, ni fisadi wa nchiye.
Maswali.
(a)Taja sifa mbili za raia Mtiifa. (ala. 2)
(b) Ni mambo gani ambayo hutokea wananchi wanapokosa utii? ( ala.2)
(c) Eleza ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari ( ala 4)
(d) Onyesha mbinu mbili zilizotumiwa ili kuonyesha uhuru wa mtunzi,kwa kutolea mifano.( ala.2)
(e) Hili ni shairi la aina gani? Toa sababu. ( ala.2)
(f) Eleza muundo wa shairi. (alam 4)
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi. (ala.4)
(i) Mwasi
(ii) haziagii
(iii) Tangamano
(v) hisa
5. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Wana –haramu
Hebu nikuulize mama Afrika
Kwa nini………………
Mimba changa ukajichukulia
Ya haramu sana ilotepetea
Ukazaa wana walo jahilia
Wasiojijua, wala yao njia ?
Kuzurura ukamalizikia
Bila muruwa, heba kukupotea
Ukawa ganda la kupita njia
Usije maoni ya kuonelea?
Kwa nini……………..
Ukazaa kizazi kilo kiwete
Kilihasirika kwa wakati wote
Kilichopagawa kwa kingi kite
Hata utu wake ukakipotea?
Ah moyo waumia!
Hupigwa na mshangao
Niwafikiriapo
Wale barobaro wanao
Wasaliti wanati walo na vyeo
Walomdhidi mama mzazi wao
Kwa muradi wao.
Lakini sijali
Sijali kwani najua
Siku moja itawadia
Wanaharamu watajihalalia
Kila cha haramu kukuondolea
Na kukurakasa…..
Mama wasikia?
Hiyo siku ya siku itakapofika
Kila la dhuluma litajikatika
Na kila mahali utadhihirika
Mwisho wa salata na uharamia…….
Mama wasikia?
Maswali
(a) mwandihsi analalamikia mambo yapi katika shairi hili? ( ala.5)
(b) Mwandishi ametumia mbinu gani katika kutumia maneno. “ Mama Afriaka?” Neno hili
limetumika kumaanisha nini? ( ala. 4)
(c) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari. ( ala.4)
(d) Eleza maana ya maneno yafuatatyo: ( ala 5)
(i) jahilia (ii) Muruwa
(iii) Kilohasirika (iv) kite
(v) Barobaro.
(e) Mtunzi anamaanisha nini anaposema, ‘ukazaa kizazi kilo kiwete?’ ( ala. 2)
SEHEMU YA C : THAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
6. Huku ukitoa mifano jadili mambo mbalimbali yanayodhinirisha ubaya wa utawala wa
Mtemi Bokono. ( ala. 20)
SEHEMU YA D: FASIHI SIMULIZI.
7. (a) Kwa kutoa mifano taja mambo yoyote manne yanayozua lakabu (ala.4)
(b) Jadili kwa kutoa mifano, umuhimu wa lakabu (ala.8)
(c)El eza sifa zozote nne za lakabu (ala.8)
More Question Papers