Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Ndhiwa District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Ndhiwa District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni lazima
• Maswali hayo mengine matatu ya chaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Riwaya, Hadithi fupi,
Fasihi simulizi na ushairi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A : THAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kithaka wa Mberia
LAZIMA
1. Tamthilia ya kifo Kisimani ni muhtasari wa matatizo yanayotokana na uongozi mbaya barani Afrika.
Yataje na kuyathibitisha kutoka tamthiliani. (Alama 20)
SEHEMU YA B : RIWAYA
S.A Mohamed : UTENGANO
Jibu swali la 2 au la 3
2. Kwa njia ya tafsili eleza namna mwandishi alivyoshughulikia maudhui ya ufisadi katika riwaya
Utengano. (Alama 20)
au
3. “Mabadiliko, sasa alisema kwa kinywa kipana kisha...”
(a) Nani aliyesema? (Alama 2)
(b) Eleza mabadiliko aliyokuwa amepitia (Alama 10)
(c ) Wahusika wafuatao walikuwa wamekumbwa na mabadiliko yapi? (Alama 8)
(i)Mussa
(ii)Maimuna
SEHEMU YA C : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADH NA HADITHI NYINGINE.
Jibu swali la 4 au la 5
4. Wanawake ni kikwazo kwa uhuru wao. Jadili kauli hii huku ukitoa mifano kutoka hadithi tatu tofauti
katika mayai waziri wa maradhi. (Alama 20)
Au
5. Hadithi ya mkimbizi ni kioo cha matukio yanayotokea katika nchi za kiafrika. Fafanua vyanzo na athari
za vita vya kikabila kwa kurejelea hadithi yenyewe. (Alama 20)
SEHEMU YA D: FASIHI SIMULIZI.
Jibu swali la 6 au la 7
6. (a) Wimbo ni nini? (Alama 2)
(b) Taja sifa zozote nne za nyimbo (Alama 4)
(c ) Kwa kurejelea muundo wa wimbo, onyesha namna nyimbo na ushairi zinahusian.
(Alama2)
(d) Ni nini umuhimu wa nyimbo? (Alama3)
(e) Taja na kueleza aina zozote tatu za nyimbo. (Alama3)
(f) Eleza umuhimu wa ulumbi. (Alama2)
(g) Toa maana ya ndani ya methali hizi. (Alama4)
(i) Mti mkuu ukianguka ndege yu mashakani.
(ii) Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
SEHEMU YA E : USHAIRI
7. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Hayawani nondokeya, nondokeya nenda mbali
melaniwa huna haya, leo haja kukabili.
Kimbiya nenda waya, up indo wako usuli?
Umbakaji haini.
Watoto waulizani, changudoa mekushinda?
Umezua vya uhuni, kuyachafua makinda
Pinga kama si punguani, adilifu mekushinda
Umbakaji haini
Wahanyahanya yayaya, mitaani patupatu
Matendoyo kubwayaya , umewasinya wenetu
Nairobi na siaya, kote kote lithubutu
Umbakaji haini.
Jogoo kuparagia, kifaranga ni halali?
Ukimwi wawapatia, huna akili kamili
Nakutungia sheria, takufunga ukubali
Umbakaji haini.
Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (Alama1)
(b) Shairi hili ni la bahari gani? Thibitisha (Alama2)
(c) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa pili (Alama2)
(d) Taja na ueleze tamathali mbili za lugha alizotumia mtunzi (Alama2)
(e) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (Alama4)
(f) Taja matendo yoyote matatu mabaya ya anayesemwa. (Alama3)
(g) Eleza jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake wa utunzi. (Alama4)
(h) Eleza maana ya maneno yafuatayo
(i) Hayawani (Alama1)
(ii) Umewasinya (Alama1)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers