Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nakuru District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Nakuru District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina………………………………………………… Namba yako …………………….
Sahihi:………………………………………………...
102/3
KISWAHILI
Karatasi 3
FASIHI
Julai / Agosti - 2011
Muda: Saa 2½
MTIHANI WA MWIGO WA WILAYA YA NAKURU -
2011
MAAGIZO KWA MTAHINIWA
a) Jibu maswali Manne pekee katika karatasi uliyopewa
b) Swali la kwanza ni la LAZIMA.
c) Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani:
Riwaya, Hadithi fupu, Fasihi Simulizi na Ushairi
d) Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
e) Karatasi hii ina kurasa nne. Zilizopigwa chapa
f) Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa
sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
Fungua ukurasa
SEHEMU A HADITH FUPI (ALAMA 20)
K.W. WAMITILA: Mayai Waziri wa maradhi na Hadithi nyingine
1. (Lazima)
“Hapa sasa ni Makao yako mapya. Hutahangaishwa na mtu yeyote bali utasoma hadi
uhitimu masomo yako”
(a) Eleza muktadha wa kauli hii (alama 4)
(b) Elimu ya mtoto wa kike imekumbwa na matatizo mengi. Fafanua kauli hii ukirejelea
diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi Nyingine (alama 16)
USHAIRI
Jibu swali la 2 au la 3
2. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
Kila nikaapo hushika tama
Na kuiwazia hali inayonizunguka
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki
Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia yangu ya kike
Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wanidharau kwa kuukosoa utamaduni
Hukaa na kujiuliza
I wapi afua yangu dunia hii?
I wapi raha yangu ulimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?
a) Pendekeza kichwa mwafaka kwa shairi hili {alama 1}
b) Ni nini dhamira ya mshairi? {alama 2)
c) Eleza maudhui yanayojitokeza katika shairi hili {alama 4}
(d)Taja mifano ya tamathali zilizotumika katika shairi hili {alama4}
(e) Dhibitisha kwamba hili ni shairi huru {alama 3}
(f) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari {alama 4}
(g) Eleza msamiati ufuatao ulivyotumiwa katika shairi hili {alama 2}
(i) afua
(ii) hawanishiki mikono
3. Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata
Bahari
1. Bahari uzuri, wake tawambia,
Sifa tabashiri, kuwahadithia,
Ambazo ni nzuri, na faida pia
2. Na faida pia, na kwamba ujue,
Nakukuelea, nawe utambue
Na sasa sikia, uzifafanue.
3 Uzifafanue, bahari za pambo
Lenye uzuriwe, pia na urembo
Ni siri ujue, na pia ni tambo
4 Na pia ni tambo, ni siri yakini,
Aidha ni fumbo haiwezekani,
Ina mengi mambo, yenye na thamani
5 Yenye na thamani, kwa watu wa pwani,
Nawapa yakini, nanyi sikizani,
Humo baharini, kwanza pulikani.
6 Kwanza pulikani, lulu twaipata,
Samaki yakini, faida huleta,
Aidha wendani, pia huokota
7 Pia huokota, ambari zinduna,
Munyu na mafuta, vinapatikana,
Faida yaleta, pulikiza sana.
8 Pulikiza sana, tia sikioni,
Tija ya maana, ilo baharini,
Inapatikana, kwa kila ya fani.
9 Kwa kila ya fani, samaki twauza,
Mapezi yakini, ya papa sikiza,
Huleta thamani, yenye muangaza.
10 Yenye muangaza, pia na forodha,
Pato huongeza, la kuleta fedha,
Pia yaangaza, bahari kwa adha.
11 Bahari kwa adha, adhaye upepo,
Hapana orodha na ichafukapo,
Huondoka ladha, tena hapo ndipo.
12 Tena hapo ndipo, chombo hutotoma,
Nyote muliopo, hapana msema,
Ndipo muliyapo, “Mama, yoo mama!”,
Maswali
a) Shairi hili ni la bahari gani? Eleza sababu yako {alama 3}
b) Taja faida mbili na hasara mbili za bahari kama anavyoeleza mshairi {alama 4}
c) Kwa kuzingatia beti mbili za mwisho eleza umbo la shairi hili {alama 4}
d) Kwa kutoa mifano, eleza idhini ya kishairi alizotumia mtunzi. {alama 4}
e) Andika ubeti wa nane katika lugha nathari. {alama 3}
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi {alama2}
(i) pulikani
(ii) adhaye
SEHEMU B. RIWAYA
S.A MOHAMED: (Utengano)
Jibu swali la 4
4. Unafiki unajitokeza waziwazi katika Riwaya ya Utengano: Fafanua {alama 20}
SEHEMU C. TAMTHLIA
KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani
Jibu swali la 5 au la 6
5. ……………binadamu ana akili. Anatumia akili hiyo kuyabadilisha mazingira yake na
kuyafanya yamfae zaidi.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili {alama 4}
(b) Maandeleo ya Butangi yalikwamizwa kutokana na kule kutotumia akili. Fafanua
kauli hii ukirejelea tamthilia ya Kifo Kisimani {alama 16}
6. Ufisadi ni donda ndugu katika jamii ya Butangi. Thibitisha kauli hii kwa mujibu wa
tamthilia ya Kifo Kisimani {alama 20}
FASIHI SIMULIZI
7 (a) Tofautisha baina ya Kipera cha misimu na kile cha lakabu {alama 2}
(a) Eleza sifa nne kwa kila kipera {alama 8}
(c) Eleza dhima ya misimu katika jamii {alama 10}
More Question Papers