Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Mutomo/Ikutha Districts Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Mutomo/Ikutha Districts Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
JINA: …………………………….…………………………. NAMBA YAKO: ………………………
SHULE: …………………………..………………………… TAREHE: ..……………………………
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
MUDA: SAA 2 ½
TAMTHMINI LA PAMOJA WILAYA YA MUTOMO/IKUTHA – 2011
Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Sekondari Kenya (K.C.SE)
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
MAAGIZO
a). Jibu maswali manne pekee.
b). Swali la kwanza ni la lazima.
c). Maswali hayo mengine matatu yachanguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani,
Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Fasihi Simulizi.
Ilani: Usijibu maswali mawili kutoka kwa sehemu moja.
d). Kila swali lina alama 20.
Karatasi hii ina kurasa 4
Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU A
LAZIMA: FASIHI SIMULIZI
1. a) Eleza sifa za utani kama kipera cha mazungumzo katika fasihi simulizi. (Alama 4)
b) Utani una umuhimu gani? (Alama 8)
c) Onyesha changamoto zinazokabili kipera hiki cha utani. (Alama 8)
SEHEMU B: TAMTHLIA
KIFO KISIMANI – KITHAKA WA MBERIA
2. Kwa kurejelea tamthlia ya ‘kifo kisimani’ onyesha athari za utawala mbaya barani Afrika.
3. “Bila shaka simwelewi vizuri. Njiwa atamwelewaji vizuri kozi?”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Eleza sifa na umuhimu wa msemaji. (Alama 6)
c) Taja mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo hili na utolee mfano wa kila mojawapo. (Alama 2)
d) Eleza mbinu nne wanaharakati wa ukombozi walitumia kufanikisha juhudi zao. (Alama 8)
SEHEMU C: RIWAYA
UTENGANO: S.A. MOHAMMED
4. Ndoto na nyimbo za Maimuna ni ufundi wa kisimulizi unaojikita katika misingi ya taswira.
Huku ukianza kwa kufafanua taswira, eleza jinsi mwandishi anavyozitumia kufanikisha malengo yake ya
usimulizi. (Alama 20)
5……. Anakerwa kuchagua mwendo wa kuwateka wanaume, anachukia, anachukia, mwisho wa kuchukia,
lakini atafanyaje?.........
a) Weka dondoo hili katika muktadha. (Alama 4)
b) Kwa kutolea mifano, taja mbinu za uandishi katika dondoo hili. (Alama 2)
c) Eleza sifa na umuhimu wa anayezungumziwa. (Alama 10)
d) Fafanunua maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili. (Alama 4)
SEHEMU D
HADITHI FUPI – MAYAI, WAZIRI WA MARADHI K.W. WAMITILA
6. Eleza matatizo yanayokumba sekta ya elimu ukirejelea hadithi ziuatazo (Alama 20)
a) Fumbo la mwana (sijiri mukuba)
b) Ndimi za mauti (Timothy M. Arege)
c) Uteuzi wa Moyoni (Rayya Timammy)
SEHEMU E: USHAIRI
7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki
Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki
Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo
Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago
Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo
Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo
Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuliza wazo
Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai
Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui
Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo
Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo
Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa
Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa
Ama nitimue mbio, fuadinininanena, akilini nazuiwa
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Maswali
a) Toa kichwa cha shairi hili (Alama 1)
b) Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili (Alama 3)
c) Eleza umbo la shairi hili (Alama 4)
d) Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari (Alama 4)
e) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili (Alama 4)
f) Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili (Alama 2)
g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyo tumika katika shairi
i) Zani
ii) Faraghani (Alama 2)
More Question Papers