Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Mumias District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper
Mumias District Mock- Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA:SAA 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi1
102/3
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni la lazima
• Chagua maswali mengine matatu, kutoka sehemu nne zilizobaki yaani, Tamthilia , Riwaya ,
Ushairi na Fasihi Simulizi.
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA HADITHI FUPI
(SWALI LA LAZIMA)
MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE:K.W WAMITILA
1. “Pwagu hupata pwaguzi” Thibitisha kwa kurejelea hadithi ya Pwaguzi. (Alama 20)
SEHEMU YA TAMTHILIA
KIFO KISIMANI: KITHAKA wa MBERIA
Jibu swali la 2 au la 3
2. “Yetu imekuwa na vikwazo kwa miongo miwili…ukitaka nikuitie silaha yako nitakuitia….”
(a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
(b) Taja mbinu moja ya lugha iliyotumiwa kufanikisha ujumbe wa mwandishi katika dondoo hili
na uitolee mifano miwili. (alama 3)
(c) Fafanua ‘vikwazo’ anavyorejelea mzungumzaji. (alama 7)
(d) Wanaharakati wa Butangi walitumia mbinu mbalimbali katika juhudi yao ya kuondoa
‘vikwazo’ vinavyorejelewa. Thibitisha. (alama 6)
3. “Kufanikisha harakati za ukombozi kunahitaji kujitoa mhanga.” Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia
ya Kifo Kisimani. (alama 20)
SEHEMU YA RIWAYA
UTENGANO: S. A MOHAMMED
Jibu swali la 4 au la 5
4. “Lakini hatimaye alinyamaza na kilio chake kilikatika moja kwa moja, na chozi lake, lile aliloliita
‘chozi la mliwa’ lilikauka moja kwa moja pia.
(a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
(b) ‘Chozi la mliwa’
(i) Mliwa ni nani na analiwa na nani? (alama 2)
(ii) Eleza jinsi alivyoliwa. (alama 14)
5. Fafanua migogoro mbalimbali inayojitokeza katika riwaya ya Utengano. (alama 20)
SEHEMU YA USHAIRI
6. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
1. Sina ni kukosekana, si kuwa ni ubahili,
Watu hutarajiana, kupana zao fadhili,
Kiwapo chapatikana, chenye kuzidi shughuli,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
2. Iwapo mwenzio hana, cha ziada kukujali,
Ndipo anenapo sina, kukuafu yako hali,
Usidhani ni hiyana, chake kuwa hakubali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
3. Yapasa kukumbukana, tuishipo mbali mbali,
Kila mtu jambo yuna, limtialo thakili,
Akawa ni mwenye dhana,la kesho kulikabili,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
4. Na pindi anapoona, tarehe mno i mbali,
Na katika muawana, punje ya rasilimali,
Nyumbani kiwa hakuna, kukupa mtu muhali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
5. Kutaka ungekazana, nasaha na tafadhali,
Endapo hana namna, mwenzio lile na hili,
Bora ni kuombeana, Mungu awape sahali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
6. Wajua watu hupana, kiasi cha kuhimili,
Mioyo kukunjuana, imani kuwa kamili,
Akwambaye leo sina, kesho kweli takujali,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
7. Hasa munaopendana, pendo lisotamthili,
Kichache na zaidana, furahani na madhili
Daima mwaambatana, leo ni gani ajili,
Sina si kuwa bahili, sina ni kukosekana.
Maswali
1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 2)
2. Taja na ueleze bahari mbili zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
3. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
4. Andika ubeti wa 6 kwa lugha nathari (ya kawaida). (alama 4)
5. Taja mifano mitatu ya maneno ambayo yameandikwa kishairi na kisha
uyaandike kisanifu. (alama 3)
6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi:
a) bahili (alama 1)
b) fadhili (alama 1)
c) thakili (alama 1)
SEHEMU YA FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 7 au la 8
7. Soma utungo ufuatayo kisha ujibu maswali ya fuatayo
Zimepita siku ayami
Siku chungu tangu giza lipotanda
Wakati lipotazama kwa kiwewe na shauku
Pumzizo kipania, roho kupigania
Ziraili alipokakamaa aushiyo kufakamia.
Nalikwita kwa sauti
Ela penzi hukunitika
Machoyo litunga rnbele
Kumkabili huyu nduli
Nikabaki kunyong’onyeya
Jaala kitumainia,
Mtima kijiinamia
Hatima kungojea.
Ya mwisho lipopumua,
alfajiri ya kiza kikuu
Nalidhani wanichezea,
mizaha yako kawaida
Lijaribu kupulizia
Hewa toka langu pafu,
tumaini kiniambia pumzi zangu takuhuisha
Sikujua hizo likuwa Juhudi za mfa maji muhebi.
Macho libaki kutunduiya, tabasamuyo kitaraji
Kumbe mwenzangu kaniacha!
Ukiwa ulinivaa, ukungu ukatwandama
Pa kuegema, sikujua fundo chungu linisakama
Tabibu alipoingia na kutangaza rasmi mauko.
Ilikuwa kana kwamba ndo jana lipofunga nikahi.
Kumbukizi zilinijia kwa chozi teletele
Japo kifo ni faradhi ndwele hino halieleweki
Ama jicho la hasidi,
limekuangaza jamani?
Koja hili ninalokuwekea,
kando ya kasri hili la shakawa
Ni hakikisho toka kwangu, nitatamba sana na njia
Kutafuta alotwendea kinyume kutupoka,
mauko kutuleteya.
Maswali
(a) Utungo uliosoma ni wa aina gani? Thibitisha. (alama 3)
(b) Utungo huu unasawiri msimamo gani wa jamii husika kuhusu kifo ? (alama 4)
(c) Andika tamathali na mbinu za lugha zilizotumiwa katika mtungo huu. (alama 6)
(d) Nani nafsineni/mzungumzaji katika utungo huu? (alama 2)
(e) Utungo huu una umuhimu gani katika jamii? (alama 5)
8 (a) Jamii ya Kisasa imeweza kuendeleza fasihi simulizi vipi? (alama10)
(b) Eleza njia zozote tano zinazoweza kutumiwa kukusanya fasihi simulizi. (alama10)
More Question Papers