Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Mumias District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper
Mumias District Mock- Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/2
KISWAHILI
LUGHA
KARATASI YA 2
JULAI/ AGOSTI 2011
MUDA: SAA 2 ½
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari Kenya (K.C.S.E)
Kiswahili
Lugha
MAAGIZO
• Andika Jina lako na Nambari yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Weka sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
• Jibu maswali yote.
• Majibu yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Nimekaa na kutafakari kwa kipindi kirefu, juu ya mabilioni ya pesa ambayo yametengwa na
serikali ili kudhamini miradi ya maendeleo ya wanawake. Kina mama au wanawake wengi wanakiri na kusema kwamba fedha hizo zimewezesha kuwaondoa katika lindi la unyanyasaji kutoka kwa waume zao, kwani kila mmoja anamheshimu mwenzake kwa sababu ya kipato alicho nacho. Wengi wameweza kuanza biashara ndogondogo ambazo huwaletea angaa kipato kidogo.
Ukweli ni kwamba fedha hizi zimesaidia kuwatoa wanawake wengi katika unyanyasaji,
kwani wengi wanaweza kuanzisha kazi za ujasiriamali na hata kuendesha shughuli mbalimabali za maendeleo.
Kutokana na mafanikio haya, wabunge waliopitisha hoja bungeni ya kuanzisha mpango huu
wa kuwakwamua wanawake kimaendeleo wanafaa kupongezwa. Mafanikio haya yamewafanya
akina mama kujikimu kimaisha na hivyo kutowategemea wanaume katika kila jambo.
Ukitaka kujua ukweli kuhusu hili, nenda kwenye masoko utaona akina mama jinsi
wanavyohangaika na biashara zao. Kwa hivyo, ujasiriamali huendelezwa na akina mama zaidi na
hivyo wanapaswa kuwezeshwa kwa kila hali na mali.
Akina mama pia wanafaa kupongezwa kwani wameamua kujitosa kukopa fedha kutoka
kwenye taasisi mbalimbali za fedha. Fedha hizo kwa kiwango kikubwa zimewainua kutoka katika
ufukara uliokithiri hadi katika maisha ya heshima. Wale ambao hawajajaribu kuchukua mikopo, ni muhimu wafanye hivyo ili wajikimu kimaisha.
Maisha ya sasa ni magumu, hivyo yanahitaji kusaidiana kwa kila hali na mali. Wanaume kwa
wanawake ni vyema wachange bia ili wazumbue riziki. Ushirikiano utarahisisha maisha yao.
Hata hivyo, sio tu akina mama hao wameondokewa na unyanyasaji waliokuwa wakiupata ndani ya
nyumba zao, toka kwa akina baba, bali hata masuala ya mrundikano wa kesi za kugombea ardhi kwa akina mama, zimepungua. Sababu ni kwamba akina mama wengi wameweza kujitafutia ardhi
wenyewe kwa fedha walizonazo.
Ukweli ni kwamba hali imebadilika. Kinyume na hapo awali, ambapo majumba ya kifahari
na mashangingi yalikuwa hifadhi ya wanaume, siku hizi wanawake wanamiliki hayo yote.
Maswali
1. Taja dhamira mbili za makala haya. (alama.2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
2. Eleza ni kwa nini msimulizi anawapongeza wabunge. (alama.2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
3. Wanaume walikuwa wakirudisha nyuma maendeleo nchini kivipi ? (alama.2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
4. Sera za sekirali zimesaidia wanawake kivipi ? (alama.3)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
5. Eleza kwa nini baadhi ya wanawake wanaishi katika lindi la umasikini kulingana na makala haya.
(alama.3)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
6. Eleza maana ya msamiati na mafungu yafuatayo kama yalivyotumika katika makala haya : (alama3)
(a) kutafakari
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(b) kuwaondoa katika lindi la unyanyasaji
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(c) riziki
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
2. UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Katika karne hii na ya kesho, urafiki ni ngome kuu duniani ambayo huhifadhi maslahi ya kila
rafiki. Rafiki mwema humpenda mwenzake si kwa sababu ni tajiri ama ana cheo kikuu nchini. Rafiki mwadilifu huridhika na hali aliyonayo rafikiye ; akiwa ni tajiri au ni masikini, ana cheo, hana. Rafiki mwema huwa mwadilifu wakati wowote. Wakati wa neema hushirikiana na rafikiye katika furaha na wakati wa shida hushirikiana naye katika huzuni na taabu zote zinazomkabili.
Sahibu mwema hutoa alichonacho kumkomboa rafiki yake, huwa radhi kabisa kufilisika kwa
ajili yake. Mahali pa finyo hujasiri kuingia ili kumkomboa rafikiye, hushughulika zaidi kuliko wana ndugu wa toka nitoke. Kwa vyovyote hula naye tamu na chungu pamoja, mkono kwa mkono katika maisha yao yote hadi mmoja wao akaitoka dunia. Urafiki wa namna hii ndio uletao baraka ya Mungu, kuwashukia viumbe hao kama umande wa asubuhi.
Urafiki ni lazima sana katika maisha ya wanadamu. Urafiki ni mfano wa mishipa ipitishayo
damu mwilini ili kurutubisha kila sehemu ya mwili. Ingawa ni bora kuwa na marafiki wengi lakini kila marafiki wanapozidi, ni hatari ya kuangukia kwenye marafiki wadanganyifu-hasidi. Pasi na shaka, ni heri maadui kuliko marafiki wadanganyifu. Hivyo basi, tukiwa na rafiki walio kinyume cha wema na upole wa kulinda haki za wanadamu na wasiomcha Mungu ni lazima tuwaepuke. Ingawa ni hivyo, vile vile sheria inatukataza tusisikilize na kujali ubaya wa mtu yeyote pasipo kuhakikisha.
Huenda ikawa ni uvumi tu usiokuwa na msingi wowote. Ikiwa rafiki ni mbaya, hakosi atajulikana kwani mtungi mbovu haukawii kuvunjika. Lazima tuwapende watu wote ili kutimiza haki za kibinadamu na kuchukia matendo maovu. Rafiki waovu si vema kuwaacha katika maangamizi ya ubaya wao bali ni lazima tuwaambie waziwazi ili wapate kuongoka. Ukimsamehe rafiki, unaponyadonda lake moyoni. Hivyo ni bora kuliko kumtazama na hali anazidi kukosa.
Maswali
(a) Kwa maneno yasiyozidi 60, fupisha aya ya kwanza na ya pili. (alama 7)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(b) Ni muhimu kuwa na rafiki na marafiki na kuwachagua kwa umakinifu. Kwa kurejelea aya ya
tatu, thibitisha kauli hii. (maneno kati ya 50-55) (alama 5)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
(a) Onyesha shadda katika maneno yafuatayo: (alama.1)
(i) Kuzungumza
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Niletee
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza matumizi ya ‘po’ katika sentensi zifuatazo:
(i) Aishipo pana hatari
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Aingiapo wanafunzi hufurahi (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(c) Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii.
Tulimchezea Jumanne.
i)………………………………………………………………………………………………………
ii)………………………………………………………………………………………………………
(d) Tunga sentensi ukitumia kiunganishi kifuatacho:
Mintarafu ya (alama.1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(e) Bainisha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi hii;
Ali alimletea Yohana chai kwa chupa. (alama.3)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(f) Tumia alama zifuatazo katika sentensi kubainisha matumizi yake.
(i) Kistari kirefu
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Mshazari (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
(g) Changanua sentensi ifuatayo ukitumia jedwali.
Mwanafunzi hodari anayechezea shule ya Hekima amepewa zawadi. (alama.4)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(h) Kutokana na kitenzi safiri, tunaweza kupata nomino safari. Je, kutokana na kitenzi hutubu
tunapata nomino gani? (alama.1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(i) Andika katika usemi wa taaarifa.
“Mkiendelea na tabia hiyo yenu, huenda msifanye vizuri katika mtihani” Mwalimu aliwaonya
watahiniwa.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(j)Linganisha sauti zifuatazo:
/r/ na /l/ (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(k) Tunga sentensi kuonyesha tofauti kati ya shombo na chombo. (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(l) Tunga sentensi moja iliyo na;
(i) Kikanushi
(ii) Kiima katika nafsi ya pili
(iii) Mtendewa nafsi ya tatu
(iv) Shina la kitenzi
(v) Kauli la kutendea
(vi) Kiishio
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(alama.3)
(m) Tambua na ueleze vielezi vya namna vilivyotumika katika sentensi zifuatazo.
(i) Mtoto anapenda kulia ovyo ovyo jioni.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Naomi alisafiri kwa ndege hadi Nairobi. (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(n) Andika maneno mawili yaliyo na muundo wa silabi funge. (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(o) Nomino iliyopigiwa mstari ni nomino aina gani?
(i) Mwanajeshi hodari alituzwa.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kucheza kwake kulipendeza. (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
(p) Tumia –refu kama nomino na kitenzi kutunga sentensi. (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(q) Bainisha virai vilivyopigiwa mstari ni vya aina gani. (alama.2)
(i) Paka amejificha kichakani.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(ii) Nguo zake ziko kando ya mto.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(r) Kanusha
Ukisoma kwa bidii utafaulu. (alama.1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(s) Andika sentensi ifuatayo kwa udogo.
Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kiafya. (alama.2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
(t) Andika katika kauli ya kutendata.
fumba. (alama.1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
ISIMU JAMII (ALAMA 10)
4. Eleza sababu za vijana kutumia lugha ya sheng’ (alama.10)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
More Question Papers