Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Matungu District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper
Matungu District Mock- Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina: …………………………………………………………………… Nambari: ………...………
Shule: ………………………………………………………………. Sahihi ....................................
Tarehe: …………….....................................................................……
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI/AGOSTI 2011
MUDA:SAA 2 ½
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya.( K.C.S.E)
Kiswahili
Fasihi
MAAGIZO
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni la lazima
• Maswali hayo mengine matatu chagua kutoka sehemu nne zilizobaki yaani, Riwaya , Tathilia,
Hadithi fupi na Fasihi Simulizi
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A : HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI wa MARADHI na HADITHI NYINGINE. K.W Wamitila
1. (a) Kulingana na hadithi ya ndimi za mauti, viongozi wa wanafunzi walikuwa na malalamiko gani?
(Alama 4)
(b) Ni nini madhara ya migomo shuleni? (Alama 4)
(c) Pendekeza jina mwafaka ya kukabiliana na migomo shuleni. (Alama 12)
SEHEMU YA B : TAMTHILIA
KIFO KISIMANI Kithaka wa Mberia
Jibu swali la 2 au la 3
2. Ukirejelea tamthilia ya Kifo kisimani, onyesha mchango wa wanawake katika vita dhidi ya utawala dhalimu. (Alama 20)
3. “Bahati nasibu inapomteremkia mtu, mara nyingine uhalisi huonekana kama ndoto. Mambo huwa hayaeleweki kwa urahisi. ”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
(b) Onyesha bahati inayorejelewa katika dondoo hili. (Alama 10)
(c) Bahati hii ingepatikana vipi? (Alama 6)
SEHEMU YA C: RIWAYA
UTENGANO-S.A Mohammed.
SEHEMU YA D. USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Nimeona, milima na mabonde, misitu na nyika
Nimeona, majani na umande, uliotandazika
Nimeona, mkulima yuwenda shambani.
Nimeona, uwanda na magugu, yalimkabili
Nimeona, na vurugu, wiano mkali
Nimeona, mkulima akiwa tayari.
Nimeona, kwa hari na juhudi, anatupa jembe
Nimeona, kakaza ukaidi, kwa nguvu achimbe
Nimeona, mkulima akiwa mbioni.
Nimeona, kujua kinawaka, kama jahanamu
Nimeona, jembe lainuka, linapohujumu
Nimeona, mkulima akiwa mbioni.
Nimeona, mvua yamiminika, naye halohisi
Nimeona, kwa kani anatimika, bila wasiwasi
Nimeona, mkulima akiwa kazini.
Na sioni, jasho linapomwaika, yendapo mazao
Na sioni hadiye kutukuka, ila kilio
Kwa nini, Nauliza mkulima, kwani?
Maswali
(a) Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 5)
(b)Taja na ufafanue tamathali katika shairi hili.
(c)Taja taswira zilizoko katika shairi hili. (alama 2)
(d) Onyesha jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumika katika shairi hili. (alama 2)
(e) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 3)
(f) Eleza maudhui ya shairi hili. (alama 4)
6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
1. Ni sumu, sumu hatari 3. Ni sumu, sumu legezi
Unahatarisha watoto Unalegeza watoto
Kwa ndoto zako leweshi Kwa mazoea yako tenganishi
Za kupanda ngazi Ya daima kunywa ‘moja band’
Ndoto motomoto ambazo Mazoea mabaya ambayo
Zimejenga ukuta Ulevi
Baina ya watoto Yakufunga katika klabu
Na maneno laini Hadi saa nane usiku baridi
Ya ulimi wa mzazi Huku yakilenga kutofahamiana
Baina ya watoto na mzazi
2. Ni sumu, sumu hasiri 4. Ni sumu, sumu jeruhi
Unahasiri watoto Unajeruhi watoto kwa pesa
Kwa pupa yako hangaishi Kwa mapenzi yako hatari
Ya kuwa tajiri mtajika Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa
Pupa pumbazi ambayo Zinawafikisha kwenye sigara na
Imezaa jangwa bahili Na kisha kwenya madawa
Badala ya chemichemi Ya kulevya
Ya mazungumzo na maadili Barabara inayofikisha kwenye
Baina ya watoto na mzazi Giza
La kaburi la asubuhi.
Maswali
(a) Pendekeza kichwa kwa shairi hili. (alama 1)
(b) Fafanua maudhui ya shairi hili (alama 4)
(c) Ni kwa njia gani kinachozungumziwa kinajenga ukuta? (alama 2)
(d) Dondoa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi na uzitolee mifano. (alama 4)
(e) Eleza umbo la shairi hili. (alama 3)
(f) Uandike ubeti wa nne kwa lugha nadhari. (alama 4)
(g) Eleza maana ya vifungu hivi vilivyotumika katika shairi. (alama 2)
(i) Giza baridi
(ii) Yana kufunga katika klabu
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
7. (a) Eleza kwa kina maana ya neno ‘wimbo’ katika fasihi simulizi. (alama 2)
(b) Eleza sifa zozote nne za nyimbo kwa ukamilifu. (alama 4)
(c) Eleza sifa zozote nne za nyimbo za kisiasa. (alama 4)
(d) Eleza umuhimu wa nyimbo. (alama10)
More Question Papers