Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Masinga District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Masinga District Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
JINA: .......................................................................... NAMBA YAKO :...................................
SHULE …………….................................................... TAREHE :...............................................
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
MUDA: SAA 2½
TAMTHMINI LA PAMOJA, WILAYA YA MASINGA - 2011
Cheti cha Kuhitimu Masomo ya Sekondari Kenya (K.C.SE)
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
MUDA: SAA 2½
MAAGIZO
Jibu maswali yote.
karatasi hii ina kurasa 10 Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU (Alama 15)
Soma habari iliyopo, kisha jibu maswali yanayofuatia.
Kigumba kwa Nguruwe.
Kikamilifu methali hii ni: Kigumba kwa nguruwe kwa mwanadamu ki chungu. Kufahamu maana yake, ni lazima tuchunguze kijuujuu maana ya maneno yaliyotumiwa. Kigumba ni chembe cha mshale, mkuki au chusa kinachotumiwa kuchoma na kumjeruhi mnyama. Nguruwe ni mnyama anayesakwa na kufumwa na
kufurahikiwa na wasasi anapopatwa. Uchungu ni maumivu yanayoletwa na kitendo hicho cha kufuma.
Nguruwe hufisidi mimea ya wakulima. Hapo basi husakwa kwa mishale na mikuki na kuuawa. Watu hupata uhondo wa nyama. Wakati mwingine, katika zile hekaheka za kusaka, huenda mshale au mkuki ukamdunga mtu badala ya yule mnyama.Vivyo hivyo anapaswa afahamu kuwa uchungu anaousikia yeye ndio ule aliousikia nguruwe.
Mzee Kisheta alikuwa mraibu wa bangi, na kwa sababu hiyo, hakuweza kumkimu yeyote; si mkewe, si watoto hata mwenyewe na aila yake yote. Kila hela aliyoipata, alilongeza katika vihindo vya wauzaji bangi.
Mkewe, Kitete, alikuwa akienda kutafuta vibarua angalau awasitiri wanawe. Chochote kile alichopata, ilimbidi akifiche, kwani mumewe alivisaka vibetini, mitoni na matandikoni, chini ya mivungu ilimradi nyumba nzima aliichakura. Akikipata hukimbilia kwa wachuuzi wake. Asipokiona, humkabili mkewe kwa matusi na magumi. Mkewe, aliyechekelea sana kufufutwa, humtolea nusu ya pesa alizopata ili aipoze ghaidhi ya mumewe. Kisheta huchomoka huyoo! Hapo basi Kitete huepukana na kero.
Siku moja, Kitete alirudi na shilanga lake begani huku akitabasamia mwanawe mdogo Kita, aliyeuona uso wa furaha wa mamaye uliobashiri mafanikio aliuliza, “Mama una furaha leo! Je, umetuletea nini?” Mamake alimjibu kuwa alikuwa na furaha sana siku ile kwa sababu bibi aliyemlimia ngwe siku hiyo alimpa bahashishi ya shilingi ishirini kwa kazi yake nzuri. Badala ya shilingi hamsini alipata shilingi sabini. Ilikuwa furaha iliyoje! Alipomaliza kumjibu mwanawe kwa furaha, aliliingiza jembe lake ndani na kutoka haraka haraka awahi kwenda madukani kabla ya Kisheta kufika pale na kumnyang`anya pesa zake alizozipata kwa jasho.
Alipotoka nje ya nyumba tu, alikutana na mumewe aliyezuka ghafula, haijulikani kutoka wapi! Papo hapo alimtolea jicho mkewe mkono kaunyosha akitaka kupewa ujira wote alioupata siku hiyo.Mama Kita alikataa katakata akisema hakupata chochote siku ile.
Kisheta alikuja juu, akamshika mkewe akitaka kumvunja kama ukuni mkavu. Mkewe alilia kwa uchungu akijaribu kujikwamua, lakini mikono yake Kisheta ilikuwa imemkaba kama koleo. Hakuweza kumtoka.
Mwanawe, Kita, alipomwona mamaye alivyokuwa akiteseka alisema, “Mama, kwa nini ufe na pesa unazo?
Si umpe baba hizo shilingi sabini ulizozifunga hapo katika pindo la leso?” Kusikia hivyo, Kisheta alimwachilia mkewe kwa kumkita chini na kumwamrisha ampe pesa zile. Bibi huyo hakuwa na la kufanya ila kuzitoa. Kisha akakaa chini na kujiinamia kwa huzuni. Mzee Kisheta alifurahi na kumnyanyua Kita juu na kusema. “Wewe u dume kweli! Unampenda baba yako. Kua mwanangu na uwe kama babako.” Mtoto huyo alisikiza maneno hayo, lakini hakuonekana kuelewa aliyoambiwa.
Siku nyingi zilipita na maisha ya Kisheta yalizidi kuzorota. Jumapili moja baada ya kupotea kutwa nzima, asijulikane alikokuwa. Kisheta alirudi akiandamana na watu wawili hadi pale nyumbani kwake. Walipofika mkabala wa ukumbi, Kisheta alisikika akisema, “Mabwana, mimi asilani sivuti hata sigara, lakini ikiwa mwasisitiza kuwa mwataka kuingia ndani basi mwakaribishwa.” Kita aliposikia babake akisema hivyo,alidakia, “Wewe baba huvuta sigara. Hata jana ulinituma sigara sita kubwa dukani kwa Ali.” Kisheta alimrukia Kita akataka kumzaba makofi. Kumbe wale mabwana aliokuwa nao walikuwa askari kanzu.
Walimzuia asimpige mtoto; walilisaka banda lake la nyumba na kuona vipande sita vya misokoto ya bangi chini ya sanduku la mbao lililokuwa na suruali moja iliyojaa viraka na fulana moja kuukuu. Kisheta alitiwa pingu na kupelekwa kwenye kituo cha polisi. Alipokuwa akitolewa mle nyumbani, aliropoka laana kwa mwanawe Kita. Mama Kita matumbo yalimsokota akamkabili mumewe na kumsuta. “Msalie Mtume?
Usinilaanie mwanangu? Malipo ni hapa duniani. Jambazi we! Umepata stahili yako!”
Maswali:
1. Toa fasili ya kigumba katika kisa hiki. (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
2. Eleza uhusiano kati ya Kisheta na mkewe katika hali yao ya maisha. (Alama 3)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
3. Ni kitu gani kilichopandisha mori Kisheta hata akawa karibu kumwumiza mkewe? (Alama 1)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
4. Taja sababu zilizomfanya mtoto Kita kutoboa kuwa mamaye alikuwa na pesa na babaye alivuta sigara?
(Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
5. Ni mafunzo gani tunayoyapata kutokana na kisa hiki? (Alama 3)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
6. “Kutojua ni usiku wa giza.” Fafanua msemo huu ukilinganisha na makala uliyosoma. (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
7. “Jambazi we! Umepata stahili yako!” Fafanua. (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
2. MUHTASARI: (Alama 15)
Ponografia na athari zake:
Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kufanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, video, magazeti, vitabu, muziki, televisheni, wavuti, DVD n.k.
Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa sababu imeenea ulimwenguni kote mithili ya moto katika mbuga wakati wa kiangazi. Uenezi
umechangiwa na mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi umetokana na kuimarika kwa vyombo
vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali vya picha yamesambaza ponografia haraka na kwa wingi.
Haifahamiki barabara jinsi ponografia ilivyoanza. Hata hivyo hubuniwa au kutengenezwa na makundi mbalimbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza uchafu huu kwa lengo la ama kuvuruga maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni lile la wanaoichukulia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la wanaotumia matusi haya kama njia ya kuchuma.
Kwa mfano, kuna wanamziki ambao hutumia ponografia kuvutia wateja na hivyo kuzindisha mauzo yao.
Kushamiri kwa wimbi la uonyeshaji ponografia kuna athari kubwa kwa jamii na hasa watoto. Ingawa watu wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wanaotazama picha za ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kuwa kinachoonekana na jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikra au hisia.
Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama masomo watu huanza kutafakari mambo machafu.
Vijana wengi ni kama bendera. Hivyo basi huanza kuiga wanayoyaona na kusikia. Hili ni tatizo linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Kutokana na uchafu huu, watu wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni mengi. Haya ni pamoja na ukahaba. Utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mambo yasiyotarajiwa.
Vijana wengi huacha shule kabisa.Wengine wao huambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo huwaletea
mauti.
Inasemekana kuwa akili za binadamu hunata zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha. Si ajabu, vijana huyadumisha matusi haya katika kumbukumbu zao na kuyafanya sehemu ya maisha yao. Wengi huanza kuandama tabia mbovu kama ushoga, ubasha na usagaji. Kuna wale ambao huanza kujichua. Kujichua ni hali ya mwanamke au mwanamume kumaliza haja za kimaumbile bila kufanya mapenzi na mtu mwingine.
Ponografia imechangia pakubwa kuenea kwa haya.
Jambo hili limegeuza mielekeo ya vijana.Wanaiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao.
Halikadhalika, huiga lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono. Yote haya yanapingana na desturi za mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kila kuchapo.
Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama unywaji wa pombe, matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za kuchochea uchu wa ngono. Mambo haya huwapa vijana tabia za unyama.
Jambo hatari ni kuwa, kuendelea kutazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, yaani huondoa makali. Hata katika utu uzima, mtu atapoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasiyo kizuizi.
Jambo la kwanza ni kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi. Kwa namna hii
itawezekana kupunguza mahitaji na uuzaji wa ponografia. Aidha ni vizuri watu wazima wawajibike ili wawalinde hasa vijana kutokana na adhari hizi. Inapasa wenye midahilishi, video na sinema wasiwaruhusu vijana kutazama uchafu huu.
Tatizo la kuenea kwa ponografia limeendelea kuwepo kwa sababu ya udhaifu wa sheria. Kilicho basi ni kuweka sheria za kuzuia utengenezaji na usambazaji wa upungufu huu. Kuambatana na haya, hatua kali zichukuliwe kwa wanaovunja sheria hizi. Halikadhalika, ushirikiano wa karibu baina ya wadau uimarishwe katika ulimwengu mzima. Serikali na mashirika ya midahilishi yajumuike kutambua chanzo cha taka hizi kisha wanaohusika wakabiliwe ipasavyo. Jamii ingependa kuona michakato ya kuharamisha utengenezaji, usambasaji na utangazaji wa ponografia ikiwekwa.
Wazazi nao wasijipweteke tu bali wasaidie. Ni muhimu washikilie kwa dhati juhudi zao za kuwaelekeza na kuwashauri watoto kuzingatia uongofu na kukwepa picha hizi najisi. Watoto lazima waelezwe kuwa haifai kutazama picha au michoro michafu. Itikadi na imani za kidini na utamaduni wa kiafrika unakataza vikali mtu kuona uchi wa mtu mwingine. Matokeo ya kuasi makatazo haya yana madhara makubwa kwa watu na jamii.
Maswali:
1. Ponografia hutengenezwa na akina nani na kwa nini?(maneno 20) (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………….
2. Eleza sababu za ponografia kusambaa ulimwenguni namna ilivyofanywa.(maneno 10) (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
3. Fupisha aya za mwisho tatu kwa maneno 60. (Alama 7)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(Utiririko. Alama 2 baada ya kupitia kama wavutia la sivyo pima uwezo wa mtahiniwa.) (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
a) Taja sauti mbili zinazotamkiwa mdomoni. (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
b) Sahihisha sentensi ifuatayo.
Usikule chakula chenye iliyo na baridi. (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
c) Tumia kihusishi mpaka ili kudhihirisha dhana za:- (Alama 2)
i) Wakati
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Kiwango (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
d) Tunga sentensi ukidhihirisha matumizi ya ngeli ya U- YA. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
e) Kanusha sentensi hii
Mmeonana leo? (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
f) Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. (Alama 2)
Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
g) Andika umoja wa sentensi hizi. (Alama 2)
i) Hii miche ni mizuri sana itatufaa.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Magofu ni mabaki ya nyumba zilizokuwa zikitumiwa zamani na ambazo hazitumiki sasa.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
h) Changanua sentensi hii ukitumia visanduku. (Alama 4)
Wasomi wanasoma vitabu na waachuuzi wanasikiza.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………….…………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
i) Neno ‘chuo’ lina maana ya shule inayotoa mafunzo maalum ya kazi fulani. Tunga sentensi mbili
kubainisha matumizi mengine mawili ya neno hili. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………….…………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
j) Andika sentensi ifuatayo upya kutegemea maagizo.
Wageni wamefika kwetu kutoka Uganda. Anza: Sisi (Alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
k) Eleza matumizi manne tofauti ya -na-. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………….…………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
l) Eleza matumizi ya hii katika sentensi hizi.
i) Kalamu hii ni nzuri . (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Hii ni nzuri (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
m) Unda jina moja moja kutokana na vivumishi vifuatavyo (Alama 1)
i) Zuri-
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Erevu-
……………………………………………………………………………………………………………
n) Kamilisha sentensi kwa kutumia maneno ya kutilia mkazo (Alama 2)
i) Rai ya mgonjwa mahututi…………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
ii) Vyakula vimejaa maghalani………….
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
o) Andika sentensi ifuatayo katika nafsi ya pili wingi.
Mimi nimefika hapa ili kumwona mtume. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
p) Kwa nini umekuwa nazi kwa mbuzi? (Alama 2)
(Geuza swali liwe kauli ya kutendewa)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
q) Akifisha sentensi ifuatayo (Alama 2)
Fanya mtihani wako kwa makini sana ukicheza utaanguka asha mama alimwambia.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
r) Eleza maana ya misemo hii (Alama 2)
i) Mwendo wa ulimbwende-
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Pua na mdomo-
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
s) Tofautisha maana ya sentensi hizi (Alama 4)
i) Walipokelewa wageni
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Walipokezwa wageni
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
t) Kanusha sentensi hii (Alama 1)
Walalapo hukoroma na kujichekea.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
u) Haya ni malipo gani? (Alama 1)
Mapoza.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII (Alama 10)
Matumizi ya lugha yoyote hudhibitiwa na mambo fulani. Fafanua matano kati ya hayo. (Alama 10).
…………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………….
More Question Papers