Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Masaku District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Masaku District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2011
Jina ________________________ Nambari ____________________
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
JULAI / AGOSTI 2011
SAA: 2 ½
MJARABU WA KIDATO CHA NNE MUHULA WA PILI 2011 WILAYA YA
MASAKU
Hati ya Kuhitimu Elimu ya Sekondari
KISWAHILI
KARATASI YA 3
SAA: 2 ½
MAAGIZO
1. Jibu maswali manne
2. Swali la kwanza ni la lazima.
3. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
Kijitabu hiki kina kurasa 3 ambazo zimepigwa chapa
Fungua ukurasa
SWALI LA LAZIMA
FASIHI SIMULIZI
1. (a) Tambua tamathali zilizotumika katika methali zifuatazo:
( alama5 )
(i) Ujana ni moshi ukienda haurudi.
(ii) Kupotea njia ndiko kujua njia.
(iii) Bandubandu humaliza gogo.
(iv) Usipoziba ufa, utajenga ukuta.
(v) Churururu si ndo ndo ndo.
(b) Nyimbo zina umuhimu gani katika jamii.
( alama5 )
(c ) Eleza aina zifuatazo za ngano.
( alama 5 )
(i) Khurafa
(ii) Ngano za mashujaa
(iii) Hekaya
(iv) Ngano za mtanziko
(v) Ngano za usuli
(d) Eleza sifa za ngomezi.
( alama 5 )
SEHEMU B: TAMTHILIA – KIFO KISIMANI
Kithaka wa Mberia
2. Jibu swali la 2 au la 3
‘Nimeshakwambia tulale hapa langoni! Tulale umati unaokuja kumtoa mfungwa
gerezani utukute hapa. Watu wanatupenda sana kwa kazi ya kumzuia mfungwa
gerezani. Kwa hivyo tuwasubiri waje watupake mafuta.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
( alama 4 )
(b) (i) Taja mbinu iliyotumika kwenye dondoo.
( alama 2 )
(ii) Fafanua matumizi ya mbinu hii kwenye dondoo.
( alama 6 )
(c ) Ni maovu gani yaliyotekelezwa na wahusika katika dondoo hii.
( alama 8 )
3. Jadili huku ukitoa mifano mwafaka matumizi ya mbinu ya uzungumzi nafsia
kwenye
tamthilia ya Kifo Kisimani.
( alama 20 )
SEHEMU C : RIWAYA
UTENGANO : S.A MOHAMMED
Jibu swali la 4 au la 5.
4. Riwaya ya Utengano imejaa kinaya. Fafanua kwa kutoa mifano mwafaka kwenye
riwaya. (alama 20 )
5. “Now, now, now – tusije huko tena, usinitie kwenye – ee, no”
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
( alama 4 )
(b) Taja mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika muktadha huu.
( alama 4 )
(c ) Mzungumzaji alikuwa amealikwa kwa madhumuni gani?
( alama 4 )
(d) Mzungumziwa alipewa mashauri mengi. Yataje.
( alama 8 )
2.
SEHEMU D : HADITHI FUPI – MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI
NYINGINE
K.W WAMITILA
6. Zena ni kielelezo cha mwanamke wa kisasa ambaye anajaribu kujikomboa.
Eleza changamoto anazokumbana nazo katika juhudi za kujikomboa.
( alama 20 )
7. SEHEMU E : USHAIRI
Soma shairi kisha ujibu maswali;
Vile walalama, kwa yale ulotendwa,
Huyakumbuki ya nyuma, pindi ulipochachwa,
Ulipotenda unyama, uliona ndio sawa
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.
Ulizusha uhasma, leo wewe wapagawa,
Walia bila kukoma, tungedhani umefiwa,
Sasa huna usalama, huwezi kujiopowa!
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.
Tenda mambo kwa kupima, usiinuke huna bwawa,
Una macho kutazama, na akili umepewa,
Matendo hurudi nyuma, atendaye hurudiwa,
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.
Dunia haishi njama, sijione umepewa,
Ukadhani u salama, binadamu kupagawa,
Ukahisi ni wanyama, waso hali kama ngawa,
Mtenda alitendwa, hulalama kaonewa.
Unapotenda zahama, siku yako ikakuwa,
Ambapo utaungwama, useme umechachiwa,
Na uanze kutetema, ulie umeonewa,
Mtenda akitendwa, hulalama kaonewa.
Maswali.
(a) Lipe kichwa shairi hili.
( alama 2 )
(b) Hili ni shairi la aina gani.
( alama 2 )
(c ) Eleza muundo wa ubeti wa pili.
( alama 4 )
(d) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari.
( alama 4 )
(e) Toa mifano miwili ya inkisari na uindeleze inavyofaa.
( alama 4 )
(f) Ni kaida zipi zilizotumiwa na mwandishi wa shairi hili.
( alama 2 )
(g) Eleza maana ya
(alama 2 )
(i) Uhasama
(ii) Umepowa
More Question Papers