Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kitui West District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Kitui West District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011

JINA: .................................................................................... NAMBA YAKO ..................................
SHULE ………...................................................................... TAREHE:.............................................
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
MUDA: SAA 2½
TAMTHMINI LA PAMOJA WILAYA YA KITUI MAGHARIBI - 2011
Hati ya Kuitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya(K.C.SE)
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
MUDA: SAA 2½
MAAGIZO
Jibu maswali yote.
Kwa matumizi ya Mtahini pekee
SWALI UPEO ALAMA
karatasi hii ina kurasa 10. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali.
URUMO AFRIKA
‘Mwenyekiti wa Kamati andalizi ya kongamano hili, mabibi na mabwana. Umaskini ndilo tatizo kubwa zaidi barani Afrika. Je, maana yake halisi ni nini? Umaskini ni ile hali ya mtu kukosa chakula, makazi na uwezo wa kumiliki mali au kushiriki shughuli za kuzalisha mali. Nchini Kenya, mtu husemekana kuwa mkata iwapo pato lake ni chini ya shilingi 1,239 kwa mwezi. Umaskini umetopea barani Afrika kiasi kwamba asilimia 60 ya wakazi wake wametota katika dimbwi la uchochole. Dhiki kubwa ya hali hii inapatikana majijini ambamo wengi wanaishi katika mitaa ya mabanda.
Kuna mambo mengi yanayochangia kuwepo umaskini. Moja ya mambo haya ni kuongezeka kwa idadi
ya watu. Hivi sasa, kuna waafrika milioni 800, wakiwemo Wakenya milioni 29; jambo la pili, ni kuwa chumi zimeporomoka na mapato ya kitaifa ya nchi nyingi yamedidimia. Kwa hivyo, serikali zinashindwa kutoa huduma za kimsingi kama chakula, maji na afya kwa raia. Ili kujiokoa, nchi nyingi zinaamua kukopa kutoka nchi zilizoendelea. Baadaye, nchi za Kiafrika hulazimika kutumia fedha kidogo zinazopata kulipia riba huku wananchi wakiteseka. Hivi ninapozungumza, Bara la Afrika lina deni la dola bilioni 300. Kati ya hizi, Kenya inadaiwa dola bilioni saba.
Bwana mweneyekiti, jambo la tatu lichangialo ufakiri ni masharti yanayoambatana na mikopo. Nchi nyingi zimelazimishwa kuweka soko huru, kubinafsisha mashirika ya umma na kupunguza idadi za wafanyakazi. Matokeo ni kuwa bidhaa kutoka nje zinaangamiza viwanda. Tena nafasi za ajira sasa ni finyu hata vijana wenye shahada za vyuo vikuu leo wanasaga lami mitaani kutafuta kazi.
Umaskini Afrika pia unatokana na bei duni ya masoko ya nje. Bara la Afrika limekuwa likiuza raslimali na mazao kwa nchi zilizoendelea kwa bei ya kijungu jiko. Hivyo, nchi za afrika hazipati faida za kuweza kuimarisha hali ya maisha ya watu wake. Isisahaulike kuwa sisiwenyewe tunachangia umaskini. Hii ni kutokana na uongozi mbaya. Mipango ya watawala wengi ni mibaya. Mfano wa hii ni ubadhirifu wa pesa kwa mieadi ya fahari kama viwanda vya silaha ambavyo havina faida kwa raia.
Utawala mbaya husababisha masumbuko, chuki na uadui ambao huchochea migogoro na vita vya sisi kwa sisi. Jambo hili husababisha sio tu uharibifu wa mali na mazingira, lakini vifo vya waafrika wengi. Bila amani shughuli za kuinua uchumi hukwama.
Sote twafahamu uovu wa rushwa. Lakini katika nchi nyingi za Kiafrika, ufisadi umejisimika vilivyo.
Rasimali ambazo zingewafaidi wote, huporwa na kunufaisha vigogo wachache tu na vibaraka wao. Aidha majanga mengine husababisha umaskini. Baadhi ya haya ni matukio ya kimaumbile kama vile mafuriko, ukame na mitetemeko ya ardhi. Matukio haya huangamiza watu na kuharibu mali na miundo msingi kama vile barabara. Hivi sasa, bara letu linakabiliwa na tisho kubwa; Ukimwi. Kila siku watu takriban 20,000 wanapoteza maisha. Pesa nyingi zimetumiwa kugharamia matibabu, mazishi na kutunza mayatima.
Mabibi na Mabwana. Umaskini ni ugonjwa mbaya. Unapotokea, husambaa na kusababisha matatizo
mengine mengi. Ulevi, uasherati, mauji, uhalifu, uombaji, maradhi, matumizi ya dawa za kulevya, uchafuzi wa mazingara na kadhalika, ni matokeo ya umaskini. Swali kuu ni: je, tufanye nini ili tujiondoe kwenye makucha makali ya umaskini?
Maswali
1. Nchi za kigeni zilizoendelea huchngia umaskini barani Afrika kwa njia gani?(Alama3)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………...
2. Eleza mambo manne ambayo hayakutajwa na mwandishi yanayosababisha umaskini barani Afrika.(Al 4)
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………..
3. Eleza umuhimu wa mikutano kama hii. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
4. Fafanua maana ya msemo huu.”Bei ya kijungu Jiko” (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
5. Eleza maana ya maneneo haya kama yaliyotumiwa katika taarifa (Alama 4)
a) Umetota
………………………………………………………………………………………………………………
b) Kutopea
………………………………………………………………………………………………………………
c) Riba
………………………………………………………………………………………………………………
d) Umejisimika
………………………………………………………………………………………………………………
2. UFUPISHO
Dhuluma kwa wanawake sio matokeo ya siasa baada ya uhuru, bali ni matokeo ya hali iliyokuwepo tangu enzi za mababu zetu; kabla ya ukoloni. Kubaguliwa na kudhulumiwa kwa wanawake kisiasa kunaoana na kunyonywa kwake kijamii kunakoshuhudiwa siku nenda miaka rudi.
Elimu ya jadi ilimwandaa mwanamke kuwa chombo kitiifu cha mwanamume. Mwanamke aliandaliwa katika unyago na katika mfumo mzima wa malezi kuwa chombo cha kutumikia mwanamume-kumstarehesha,
kumfariji, kumlisha na kumzalia watoto. Mwanamke tangu jadi hakuruhusiwa kushiriki katika shughuli za kisiasa na utawala wala hakuna mtu aliyeamini kwamba mwanmke angeweza kushikilia wadhifa wowote wa uongozi.
Demokrasia ya jadi naihusudu sana; ambapo wazee walikaa chini ya mbuyu na kuamua mambo ya jumuiya.
Mahakama ya kijiji ilikuwa aghalabu ni ya wazee na na wanaume peke yao. Hakukuwa na mwanamke aliyeshirikishwa, hata kama alikuwa ajuza. Sifa waliyokuwa nayo wanawake ni ile ya usihiri na uganga.
Mwanamke yeyote ailiyezeeka alidhaniwa kuwa bingwa wa uchawi, ulozi na ushirikina. Kwa hivyo,wanawake ndio waliokuwa washirikina wakubwa, maana fursa ya kupata elimu pana zaidi hawakuwa nayo.
Si ajabu kuwa mwanamke alipojitokeza na kusema jambo la busara, alipuuzwa na pengine kutukanwa hadharani.
Kwa bahati nzuri, kumezuka mwamko uliotuingiza katika enzi mpya. Vita vya wanawake vya kujihami na kujiendeleza katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume vimetapakaa kote katika kila sehemu ya dunia.
Wanawake wengi wamekiuka misingi na miziz ya utamanduni na kung’oa asasi za kijamii na itikadi ambazo daima zimeendelea kumyanyasa na kumuumbua utu mwanamke tangu jadi. Watetezi wa haki za wanawake zamani walilaumu suala la serikali za mataifa mwaka hadi mwaka. Huku masuala ya wanawake ya kijamii, utu na utamaduni yakishangiliwa kupitishwa, watetezi wameeleza wasiwasi wao ikiwa kupitishwa kwa maazimio kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wanawake kimataifa au katika nchi moja. Fauka ya hayo, baadhi ya wachunguzi wanaonelea kuwa maazimio mengi hayadokezi hatua za kufikiwa haki za wanawake.
Maazimio mengine yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake, kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa, majukumu yao katika jamii, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa wanawake (Unifem) na kuimarisha hadhi ya wanawake katika sekretariati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa shughuli nyingine katika mkabala huu.
Wanawake wameonyesha vipaji vyao katika nyanja mbalimbali za maisha; siasa, uchumi, utawala na kadhalika. Wanawake wamejikakamua na kudhihirisha kuwa wao pia wana jukumu muhimu la kutekeleza ili kuyaongoza maisha yao naya watu wengi. Wadumishaji wa dhuluma za kijinsia hawana budi kusalimu amri na kuukubali ukweli huu, wapende wasipende. Mtazamo juu ya haki sawa unatokana na kukubaliwa na kuondolewa kwa aina zote za ubaya dhidi ya wanwake wanojitolea mhanga kutetea hadhi yao pamoja naya wanyonge wengine. Wao huonekana kama waasi, wapinga mila na watovu wa utii.
a) Bila kubadilisha maana asilia, fupisha aya tatu za kwanza. (Maneno 45-55) (Alama 6,1 ya utiririko)
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
Jibu.
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………..
b) Kwa kurejelea aya tatu za mwisho, pambanua hoja muhimu zinazoguziwa na mwandishi. (Maneno 60-65)
(Alama 9, 2 za utiririko)
Matayarisho
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
Jibu
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
a) Irabu i na o hutamkiwa wapi? (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
b) Tofautisha matumizi ya neno vibaya katika sentensi hii
Rehema alisoma vibaya vitabu vile vibaya (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
c) Yakinisha sentensi ifuatayo.
Nisipomwona nitamlipa pesa zake (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
d) Tumia kivumishi cha ‘a’ unganifu katika sentensi ukitumia nomino katika ngeli ya A-WA. (Alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
e) Tambulisha aina za vitenzi vilivyotumika katika sentensi hizi
i) Kazi hii ni nzuri (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
ii) Mazingira yamekuwa yakihifadhiwa. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
f) Andika kisawe cha kielezi . (Alama 1)
…………………………………………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………………………………………….
g) Toa maana mbili ya sentensi hii
Nionyeshe vile nitakavyobeba. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………….
h) Tambulisha nyakati na hali katika sentensi .
Wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………….
i) Andika katika usemi wa taarifa.
“Tutakwenda kanisani kesho kutwa.” Zawadi alisema. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
j) Changanua sentensi hii kwa kutumia kielezo jedwali (Alama 4)
“Mshale huu mrefu umevunjika mara mbili
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
k) Tunga sentensi mbili tofauti ili kudhihirisha matumizi ya ‘mshazari’ (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
l) Unganisha sentensi hii kwa kutumia kirejeshi ‘O’ Kucha zake ni ndefu. Kucha zimekatwa. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
m) Eleza matumizi ya ‘Ki’ katika sentensi
Ukirusha kipira kitapotea (Alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
n) Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizoonyeshwa. (Alama 2)
i) La (kutendeshana).
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
ii) Pa (kutendesha).
……………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………….
o) Taja konsonanti mbili aina ya viyeyusho. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
p) Andika kwa wingi
Mtoto yuyu huyu ndiye aliyeiba nguo yangu. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
q) Unda sentensi yenye vijenzi vifuatavyo vya kisarufi.
Kiwakilishi + kivumishi + kitenzi + kielezi (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
r) Akifisha sentensi ifuatayo ;
Bw. Juma alimwambia bibi yake nitakuchapa ukiendelea kunijibu vibaya. (Alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
a) Ndada, mbona umerara sana na kecho akuna kazi.
i) Mzungumzaji ana tatizo gani? (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
ii) Tatizo hili limesababishwa na nini? (Alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………
b) Watu wanapozungumza huenda wakafanya makosa ya sarufi na ya kimatamshi hapa na pale, na hata hutumia msamiati vibaya.
Eleza sababu saba za kufanywa makosa haya (Alama 7)
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………

More Question Papers

Popular Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams

Return to Question Papers