Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nzambani District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Nzambani District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011

JINA: .......................................................................... NAMBA YAKO :...................................
SHULE …………….................................................... TAREHE :...............................................
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
MUDA: SAA 2½
TATHMINI LA PAMOJA, WILAYA YA NZAMBANI - 2011
Cheti Cha Kuhitimu Masomo ya Sekondari Kenya (K.C.S.E)
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
MUDA: SAA 2½
MAAGIZO
Jibu maswali yote.
karatasi hii ina kurasa 10 Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Asilimia ya chakula na mavuno yanayopotezwa katika nchi zinazoendelea ni kubwa. Baadhi ya
wataalamu wanadai kuwa kiwango cha hasara na kupotezwa kwa mazao baada ya mavuno kinafikia asilimia 10 ya uzalishaji wote. Suala la hasara ya mazao au mavuno halijatiliwa maanani inavyopasa. Hata hivyo ikiwa mataifa haya yanataka kuhakikisha kuwa dhiki ya njaa haiyakumbi, pana haja kubwa ya kulikabili suala hili muhimu. Waama hili ni suala ambalo linahitaji kutandarukiwa.
wataalamu ambao wamelichunguza suala wanatofautisha kati ya hasara za kimsingi na za kiwango cha pili. Hasara za kimsingi ni zile zinazohusishwa na vyanzo vya kibioloji kama wadudu, wagugunaji, ndege, fukusi pamoja na wanyama wakubwa. Katika kundi hili tunaweza pia kuweka hasara zinazoweza kusababishwa na bakteria. Hasara nyingine za mazao au mavuno huweza kusababishwa na tatizo la kuchanganya kemikali ambazo zina matokeo mabaya. Katika kundi hili kuna hasara zinazotokana na utakaji wa maganda, kutobolewa kwa vifaa na vyombo vya kuhifadhia mbegu, ukosefu wa vifuniko au vizibo bora.
Hasara nyingine hutokana na joto jingi au hata baridi ya mizizimo au mazingira yasiyofaa. Aidha inawezekana pakawako tatizo la ukuaji wa mbegu, kuzeeka kwa nafaka au mboga.
Hasara za kiwango cha pili ni zile ambazo husababisha hali ambapo hasara za kimsingi huweza
kutokea. Hizi huhusishwa kutokuwa na au kutumia vifaa vya kukaushia ambavyo havisibu au kutokausha mbegu ipasavyo; kutokuwa na mahali pa kuhifadhia mazao ili kuyahifadhi mazao hayo dhidi ya wadudu, wagugunaji, ndege, mvua na unyevu wa hali ya juu. Pia huhusishwa na ukosefu wa njia za usafirishaji wa mazao yenyewe au udhaifu wa muundo msingi wa kumwezesha mkulima au anayehusika kuyafikisha mazao sokoni. Tatizo jingine ni kutokuwa na uwezo wa njia mufidi au zifaazo za kuhifadhi, au utiaji baridi wa mazao yanayoharibika haraka, au ukosefu wa mfumo mzuri wa uuzaji au masoko.
Hasara ya mazao huweza kutokea wakati wowote kuanzia kuvunwa kwa mazao hadi kutumiwa
kwake. Je, nchi hizi zinapaswa kufanya nini ili kuzuia hasara hizi za mazao? Mkazo mkubwa kwenye harakati za kubana au kuzuia hasara unapaswa kuwa kwenye njia za kuhifadhi mazao au cyakula. Mazao mengi huharibika kutokana na kuwako kwa njia na mbinu duni za kuhifadhi mazao. Njia hizi ni kama kukausha mbegu vizuri na kwa njia zifaazo; kuhakikisha kuwa mboga na vyakula vinavyoweza kuharibika vinahifadhiwa vyema kwa mitambo ya umeme au vinatiwa makoponi. Mbinu nyingine ya kuhakikisha kuwa hakuna hasara kubwa ya vyakula na mazao ni kuhakikisha kuwa vyakula au mazao hayo yametunzwa vizuri.
Pana umuhimu pia wa kuhakikisha kuwa njia za usafirishaji au miundo msingi ya mataifa
yanayoendelea imeboreshwa. Kwa njia hii tutahakikisha kuwa hapana mazao yanayopotea au kuharibika kwa sababu ya kutofikishwa sokoni kwa wakati ufaao. Suala hili linahitaji mchango mkubwa wa serikali za mataifa haya kutambua umuhimu wa mfumo mzuri wa usafirishaji pamoja na usambazaji na upanuzi wa masoko ya mazao yanayohusika. Pana umuhimu pia wa kuhakikisha kuwa njia zinazotumiwa kukaushia mbegu zinafaa. Katika mataifa mengi yanayoendelea, wakulima hutegemea jua na ukaushaji wa hewa.
Inawezekana pakahitajika njia ya ziada ya kukaushia. Hata hivyo pana haja ya kuwa makini kwa sababu ukaushaji uliopiku unaweza kuzifanya mbegu kuwa dhaifu, kuzibabua, kuzipararisha, kuharibu uwezo wake wa kuchipuza au hata kuathiri uwezo wake wa lishe.
Ipo haja ya kuhakikisha kuwa dawa zinazofaa kupambana na wadudu, kama fukusi au wadudu
wengine,na tatizo la kuvu, zipo na zinapatikana kwa urahisi. Wakulima wanapaswa kuelimishwa kuhusu njia bora za kuhifadhi mazao.
Maswali
i. Eleza aina mbili kuu za hasara za mazao. (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
ii. Je, ni matatizo yepi makuu yanayokabiliwa na wakulima katika nchi zinazoendelea? (Alama 4)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
iii. Ni hatua zipi zinastahili kuchukuliwa kuhakikisha kuwa nchi zinazoendelea hazipotezi mazao mengi.
(Alama 4)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
iv. Serikali za mataifa yanayoendelea zina majukumu yepi katika suala zima la kuhakikisha mavuno
hayaharibiki? (Alama 2)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
v. Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu. (Alama 3)
• Kipaumbele.
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………….
• Muundo msingi.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
• Fukusi.
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………….
2. MUHTASARI (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali uliyoulizwa
Uzalishaji wa vyakula popote pale ulimwenguni unahusiana, na labda hata kuthibitiwa, na mazingira ambamo wanaohusika wanaishi. Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kuwa uharibifu wa kimazingira umefikia hatua ya kusikitisha. Uharibifu huu unaweza kuelezwa kama tanzia mpya ya karne tunamoishi.
Uharibifu huo unatokana na amali nyingi za binadamu ambazo zinaishia kuwa msingi wa mazingira yake kuathirika. Ikiwa mazingira yameharibiwa kwa jinsi yoyote kuna athari hasi ambazo hutokea. Kwanza, rutuba iliyoko mchangani inafifia. Kiwango cha mvua kinafifizwa pia na matendo hayo sawa na kuzuka kwa ongezeko la joto. Wataalamu wanaeleza kuwa jangwa la Sahara linapanuka kwa zaidi ya kilometa kumi kwa mwaka. Ikiwa hali hii itaendelea, itachukua miaka michache kwa sehemu kubwa ya bara la Africa kugubikwa na mchanga wa jangwa hilo. Mgubiko huo utakuwa na matokeo ambayo ni ya kusikitisha.
Yapo maeneo ambako miaka michache iliyopita yalisheheni rutuba na mboji nyingi lakini sasa hivi hayana uwezo wa kuikuza mimea yoyote ile. Zipo njia nyingi ambazo huchangia kwenye tatizo hili la mazingira. Mojawapo katika matatizo hayo ni ukataji wa miti kiholela. Ukataji huu una athari mbaya hasa pale ambapo kiwango cha miti iliyokatwa kinapiku cha miti inayopandwa au miche inayoatikwa. Tatizo jingine ni ufugaji unaokiuka uwezo wa kipande cha ardhi cha kuhimili mifugo. Ufugaji wa aina hii unatokana na kupungua kwa malisho yenyewe na labda kwa kiasi fulani kuendelezwa kwa tamaduni zinazohimiza ufugaji pasi na kuwepo juhudi za kuipunguza mifugo yenyewe. Lipo tatizo linalohusiana na kilimo, yaani ulimaji uliozidi. Ulimaji huu unahusisha upandaji wa zao lile lile katika ardhi ile ile msimu hadi msimu. Huhusisha kilimo kisichotegemea mbolea au samadi. Hali kama hii inaweza kutokana na wakulima kutumia mabua kwa mabaki ya chakula kwa ajili ya moto badala ya kuwa nyenzo ya kuundia mbolea.
Kuwepo kwa mazingira kuna mchango mkubwa kwenye lishe ya jamii inayohusika. Kwa mfano,
miti na mimea inaweza kuwa chanzo cha rutuba ya udongo usimomonyolewe na maji. Husaidia pia kwa kuhifadhi maji.
Hali kama hii inawezesha kuwepo kwa miti ya matunda kama miembe, michungwa, mitufaha,
mipera na kadhalika. Hali hii pia husaidia kuwepo kwa miti inayozalisha mafuta kama minazi. Mazingira mazuri ni msingi muhimu wa kuwepo kwa majani. Majani haya ni chakula muhimu cha wanyama ambao pia ni chanzo cha chakula kwa wanadamu. Misitu inayokua katika mazingira ya mvua huwa maskani ya nyuki (wanaoleta asali) na mimea kama uyoga (unaoliwa). Mikoko inayoota karibu na bahari ni mazingira mazuri ya kamba na samaki wengine. Isitoshe, miti huweza kuwa chanzo cha kuni za kupikia.
Maswali
a) Andika maelezo mafupi kuhusu uharibifu wa mazingira (Maneno 25 – 35) (Alama 6)
Maandalizi.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
Jibu.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
b) Kwa maneno yasiyozidi themanine (80) eleza jinsi ambavyo mazingira yanayohusiana na lishe.
(Alama 9)
Maandalizi.
…………………………………………………………………………………………………………………

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
a) Andika katika msemo halisi. (Alama 2)
Mwalimu aliwahakikishia wanafunzi kuwa kitabu kingesomwa na mwanafunzi mgeni shuleni.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
b) Unda nomino moja moja kutokana na vitenzi hivi. (Alama 2)
Sadiki……………………………………………
Sahau……………………………………………..
c) Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi hii.
(Alama 2)
Mwanasiasa aliyejitia umaarufu ameanguka uchaguzi.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
d) Eleza matumizi ya (PO) katika sentensi hizi. (Alama 2)
i. Ajapo mgeni mpokee.
.……………………………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………………
ii. Aelekeapo ni hoteli ya Leopords.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
e) Tambua viambishi awali, mzizi na viambishi tamati katika neno hili. (Alama 3)
Mwaliani?
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
f) Unda nomino moja ya mtendaji kutokana na mzizi huu wa kitenzi.
(Alama 2)
(Lind- )
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
g) Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi ya kistari kifupi kama kiakifishi.
(Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
h) Tunga sentensi moja kudhihirisha matumizi ya shamirisho ala.
(Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
i) Tambua na ueleze aina ya vielezi katika sentensi hizi.
(Alama 2)
i. Alianguka majini chubwi.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
ii. Mimi sijui alikokwenda Kamau.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
j) Tambulisha ngeli za nomino ulizopewa katika sentensi uliyopewa. (Alama 2)
Rais wa Taifa la Tujenge anapenda maendeleo.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
k) Andika upya ukitumia kiambishi (ndi- ). (Alama 2)
Githongo alifichua kashfa ya wizi.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
l) Andika katika hali ya wingi. (Alama 2)
Kwa matumaini nilimhimiza kujikakamua ili kumshinda adui yake.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
m) Pambanua sentensi hii kwa njia ya vishale. (Alama 4)
Riwaya nzuri sana imechapisha mwaka huu.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
n) Zitaje sauti mbili za konsonanti ambazo ni za midomo-meno. (Alama 1)
………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………..
o) Andika vitenzi hivi katika jinsi ya kutendesha. (Alama 2)
i. Takata……………
……………………………………………………………………….
ii. Ona
………………………………………………………………………………………
p) Kanusha sentensi uliyopewa. (Alama 2)
Giza la ujinga lililotamalaki limetanzuka.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
q) Andika sentensi katika hali ya kuamrisha. (Alama 2)
Tafadhali acheni kucheka ovyo.
…………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
r) Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii. (Alama 2)
Amina amesumbuliwa na mtoto kwa siku nyingi.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
s) Kwa kutunga sentensi moja onyesha matumizi sahihi ya kiunganishi ama. (Alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………..
4. ISIMU JAMII (Alama 10)
a) Tofautisha lugha ya kimataifa na lugha ya kitaifa na utolee mfano mmoja mmoja. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
b) Eleza harakati zinazotumiwa nchini Kenya kukiendeleza Kiswahili. (Alama 8)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………

More Question Papers

Popular Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams

Return to Question Papers