Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nzambani District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Nzambani District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



JINA: .......................................................................... NAMBA YAKO :...................................
SHULE …………….................................................... TAREHE :...............................................
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
MUDA: SAA 2 ½
TAMTHMINI LA PAMOJA, WILAYA YA NZAMBANI - 2011
Cheti Cha Kuhitimu Masomo ya Sekondari Kenya (K.C.S.E)
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
MAAGIZO
a). Jibu maswali manne pekee.
b). Swali la kwanza ni la lazima.
c). Maswali hayo mengine matatu yachanguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani,
Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Fasihi Simulizi.
Ilani: Usijibu maswali mawili kutoka kwa sehemu moja – yaani Tamthilia au Riwaya.
d). Kila swali lina alama 20
Karatasi hii ina kurasa 4
Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA 1; USHAIRI
1. Swali la lazima
Shairi A:
1. Jaribu kuwa mpole, kwa wenzio darasani,
Jihadhari na kelele, na utusi mdomoni,
Wala siwe kama wale, wanafunzi maluuni,
Waso akili vichwani, katu usiwaingilie.
2. Ujipanyapo ja vile, watoto wale wahuni,
Juwa jatakwenda mbele, utashindwa mtihani,
Na toka dakika ile, utaingia mashakani,
Jaribu uwe twaani, mwanafunzi zingatile.
3. Mtoto kiwa mpole, nakueleza yakini,
Huwa ni mfahamile, wa elimu akilini,
Ni shida kuangukile, kushindwa na mtihani,
Yataka utamakani, mwanafunzi siliwale.
4. Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani,
Sizowee kusengenya, sengenyo madarasani,
Kama hilo ukifanya, utakuwa mashakani,
Ni hayo nilowaonya, kwa hiyo nawaageni.
Shairi B:
Aliniusia babu, zamani za utotoni
Kanambia jitanibu, na mambo ya nukaani
Na wala usijaribu, kwa mbali wala jirani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.
Liche jambo la aibu, lipalo mtu huzuni
Liuvunjao wajibu, m’bora akawa duni
Lau chamba utatubu, kulipwa hukosekani
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.
Usipolipwa karibu, lakutoka fahamuni
Lazima lije jawabu, ingawa pindi mwakani
Japo kuwa ughaibu, au mwisho uzeeni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.
Kila neno lina jibu, usitafute kwa nini
Mambo yenda taratibu, pupa jingi lafaani
Akopeshae zabibu, atalipwa zaituni
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.
Ahimilie taabu, hupata mema mwishoni
La raha au sulubu, malifi ni duniani
Mambo bahati nasibu, viumbe tahadharini
Malifi ni duniani, kuzimu kwenda hisabu.
Maswali:
a) i) Linganisha shairi A na B kwa kuzingatia maudhui. (Alama 6)
ii) Linganisha na kutofautisha mashairi A na B ukizingatia sifa za arudhi. (Alama 6)
b) Toa mifano miwili yoyote ya inkisari kutoka kwa mashairi haya. (Alama 2)
c) Fafanua maana ya mishororo ifuatayo kama ilivyotumiwa katika mashairi haya. (Alama 2)
i) Kanambia jitanibu, na mambo ya nuksani.
ii) Mwanafunzi nakukanya, kwa yale mawi mwandani.
d) Eleza maana ya msamiati ufuatao (Alama 4)
i) Nuksani
ii) Sulubu
iii) Malifi
iv) Katu
SEHEMU YA 2; TAMTHILIA
Kithaka wa Mberia. Kifo Kisimani.
Jibu swali la 2 au la 3
2. Mwandishi wa tamthilia ya KIFO KISIMANI ameshirikisha wahusika wafuatao katika sanaa yake.
i) Makea
ii) Dato
iii) Askari mkuu
iv) Mbutwe
Eleza kwa kuzingatia kila mhusika muktadha na umuhimu wake katika tamthilia. (Alama 20)
3. “Ndiyo kweli; Dhiki maishani mwetu imesababishwa na utawala mbaya. Zamani tulikuwa na chemichemi
za maji, zimekauka”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Fafanua kwa tafsili dhiki zinazowakumba wanabutangi. (Alama 16)
SEHEMU YA 3; RIWAYA
S.A Mohamed: Utengano.
Jibu swali la 4 au la 5
4. “Na ungefedheheka kweli kwa huo uzushi wako. A-a katafute kwingine kuutua huo wimbo wako.
Nimekusudia ujenzi.
a) Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 6)
b) Taja na ueleze tofauti moja dhahiri iliyoko kati ya wazungumzaji hawa. (Alama 4).
c) Kwa kutolea mifano mwafaka, onyesha jinsi mhusika KABI alivyo na ueleze umuhimu wake
katika riwaya hii. (Alama 10)
5. Fafanua mbinu zifuatazo za lugha kama zilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya utengano
i) Sadfa
ii) Kinaya
iii) Majazi
iv) Tashhisi
SEHEMU YA 4; HADITHI FUPI
K.W wamitila : Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine.
Jibu swali la 6 au la 7
6. “Umdhaniye ndiye kumbe siye “
Ukirejelea mkusanyiko wa hadithi tano thibitisha ukweli wa kauli hii. (Alama 20)
SEHEMU YA 5; FASIHI SIMULIZI
7. a) Eleza maana ya maghani ni nini? (Alama 2)
b) Eleza maana ya neno ulumbi. (Alama 4)
c) Bainisha sifa za mlumbi. (Alama 10)
d) Eleza umuhimu wa ulumbi. (Alama 4)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers