Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Narok District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Narok District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/2
KISWAHILI
1. UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Watoto wamekuwa wakiteswa na kusumbuliwa sana kwa miaka mingi. Wengi wao wamekuwa
wakinyimwa chakula, kukosa elimu, kuishi katika maisha ya dhiki na kufanyizwa kazi ngumu.
Lakini hapana msiba wa milele. Hali hii imeanza kubadilika baada ya ulimwengu mzima kutambua umuhimu wa haki za watoto.
Takriban mataifa yote ya ulimwengu ambayo ni wanachama wa umoja wa mataifa isipokuwa Somalia (ambayo haina serikali kuu) na Marekani yametiana saini makubaliano kuhusu haki za watoto.
Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa uliofanyika mwaka wa
1989. Hata hivyo, utekelezaji wenyewe wa makubaliano hayo ulianza mwezi wa Septemba mwaka wa 1990. Je, haki hizo za watoto ni zipi lakini? Haki za watoto zinaweza kupangwa katika makundi manne makuu ambayo ni: haki za kukua, haki za kuishi, haki za kulindwa na haki za kushiriki.
Haki ya kimsingi kabisa ni ile ya kuishi. Mtoto yeyote hawezi kufurahia haki zozote zile asipokuwepo,lazima awe hai. Maisha ya mtoto hayapaswi kukatizwa na chochote kile. Lazima ziwepo juhudi za kupinga vitendo vyovyote vinavyotishia maisha ya mtoto. Aidha, lazima mtoto atunzwe ipasavyo kimatibabu.
Haki nyingine ya watoto ni ile ya kulindwa. Aghalabu ulinzi wa mtoto hufanyika katika familia.
Lakini sio watoto wote ambao wana bahati ya kuwa na familia inayoweza kuwapa ulinzi ufaao. Hawa wanapaswa kulindwa na kutunzwa na familia nyingine au na taasisi ambazo zinahusika na watoto.
Ulinzi huo lazima ufungamane na sheria na utamaduni wa mtoto anayehusika. Mtoto pia ana haki ya kulindwa dhidi ya ajira ya watoto ambayo inawahusu watoto wanaofanya kazi wakiwa na umri wa chini ya miaka kumi na sita. Kazi huathiri ukuaji wa akili, kimwili, kijamii na hata kimaadili kwa mtoto anayehusika. Isitoshe, lazima mtoto alindwe dhidi ya mateso, dhuluma, adhabu na kunyimwa haki na uhuru wa aina yoyote ile. Kwa mfano, haifai mtoto kuadhibiwa kwa hukumu ya maisha au kif'ungo cha maisha gerezani. Mtoto anapaswa kulindwa pia dhidi ya kubaguliwa kwa misingi yoyote ile, majanga, kulazimishwa kushiriki vitani na kuteswa kwa sababu ya maumbile yake. Pia tunapaswa kuhakikisha kuwa mtoto hateswi wala kudhulumiwa kwa sababu ya utamaduni fulani. Kwa mfano, zipo tamaduni zinazowalazimisha watoto wa kike kuolewa mapema au hata kupashwa tohara.
Haki nyingine kwa mtoto ni haki za maendeleo. Msingi mkubwa wa maendeleo ni elimu. Mtoto
aliyepata elimu bora anaweza kuzielewa na kuzifurahia haki nyinginezo kwa njia nzuri na akawa anaishi maisha mazuri. Suala hili la maendeleo lazima lihusiane pia na uhuru wa kuweza kutambuliwa na kupewa utambulisho bila kubaguliwa.
Mwisho kabisa kuna haki ya kuishi. Haitoshi tu kuweza kuishi bali pia lazima mambo mengine
muhimu yazingatiwe. Kwa mfano mtoto ana haki ya kupata habari kuhusu mambo mbalimbali
yanayomhusu na kuhusu jamii yake. Habari ni msingi mkubwa wa kuwa na uwezo wa kujielewa.
Mtoto anaweza kupata habari hizi kwa njia mbalimbali kama kupitia vyombo vya habari, kwa kupitia kompyuta n.k. Hata hivyo lazima mtoto huyo alindwe na picha au habari zinazoweza kumpotosha.
Mtoto pia anao uhuru wa kushiriki na kujumuika na wenzake na hata kujiunga na vikundi vingine anavyopendelea. Haki hii ya kuishi haikamiliki bila ya kuwapo kwa haki ya kufikiri na kutoa maoni na hata kafanya maamuzi.
Jamii yetu inapaswa kushirikiana bega kwa bega kuhakikisha kuwa watoto hawatendewi dhuluma ya aina yoyote. Asilimia kubwa ya jamii zetu ni vijana ambao ndio tegemeo la jamii ya kesho. Ikiwa tunataka kuujenga msingi imara na mzuri wa jamii hiyo ya kesho, pana umuhimu mkubwa wa kuhakikisha kuwa tumewatunza watoto vizuri.
Maswali:
1. i). Toa anwani itakayofaa sana kwa taarifa hii.. (Alama 2) *Nrk*
ii). Kifungu. "hapana msiba wa milele" ina maana gani kulingana na taarifa hii?(Alama 2) *Nrk*
iii). Je, ajira ya watoto ni nini? (Alama 2) *Nrk*
iv). Ajira ya watoto huwaathiri vipi? (Alama 2) *Nrk*
v). Maendeleo ya mtoto hayawezi kunawiri bila uhuru. Thibitisha (Alama 2) *Nrk*
vi). Mtoto atasaidiwa na nini ili aweze kupanua akili yake vizuri? (Alama 2). *Nrk*
vii) Msingi mkubwa wa maendeleo katika taarifa hii ni nini ? (Alama 1) *Nrk*
viii) Eleza maana za
2. -Takribani (Alama 1) *Nrk*
3. - Tia Saini (Alama 1) *Nrk*
2. SEHEMU YA B: Ufupisho
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo.
Uhalifu ni tendo lolote linalokwenda kinyume na matarajio ya watu, jamii, au taifa na linaloweza kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo ambao unakwenda kinyume na sheria za kidini au kanuni za kimaadili. Kwa mfano, mwananchi anayemwona mwenzake akiibiwa mkoba wake na kusimama bila kufanya lolote, amefanya kosa la kimaadili. Lakini tuangalie ni matendo yapi ambayo yanachukiliwa kama yanayokwenda kinyume na sheria za nchi, yaani matendo ya kihalifu?
Kuna matendo ya kihalifu yanayotendwa dhidi ya usalama wa umma au maadili ya jamii. Uhalifu
dhidi ya mtu mwingine unahusu kitendo kinachomwathiri mtu mwingine kama mauaji, ubakaji na
unajisi, wizi na ushambulizi. Uhalifu dhidi ya mali ambapo hapana uhusiano kati ya mtu mmoja na mwingine, huhusisha wizi wa kuvunja nyumba, uchomaji magari, uchomaji moto mali, wizi, na uharibifu wa mali. Uhalifu unaohusisha usalama wa umma na maadili unahusisha matendo kama uchezaji kamari, ukahaba, uvunjaji wa sheria zinazohusiana na matumizi ya dawa, udanganyifu unaohusisha amana au mali ya umma na ulevi.
Uhalifu pia huweza kuainishwa kwa kutegemea adhabu anayopewa mhalifu anayehusika. Kuna
makosa makubwa au makosa ya jinai na makosa madogo kisheria. Makosa ya jinai ni yale ambayo
yanahusisha kifungo gerezani aghalabu cha zaidi ya mwaka mmoja. Kwa mfano, wizi wa kutumia
nguvu, uporaji wa magari, mauaji na ubakaji ni makosa ya jinai.
Swali:
Kwa maneno yasiyozidi themanini, fupisha hoja kuu katika aya mbili za mwisho.
(Alama 15) *Nrk*
3. MATUMIZI YA LUGHA
4. a) Kanusha sentensi zifuatazo; (alama 2) *Nrk*
(i) Uliugua malaria
(ii) Nimejenga kasri
b) Andika nomino mbili katika ngeli ya U – YA. (alama 2) *Nrk*
c) Andika nomino zinazoweza kuundwa kutokana na vitenzi vifuatavyo.(alama 2) *Nrk*
(i) Safiri
ii) Penda.
5. d) Andika kwa umoja (alama 2) *Nrk*
i) Machaka ya waridi hayazai maua meusi
ii) Walituandikia nyaraka ndefu.
e) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kivumishi cha pekee ulichopewa.
(alama 2) *Nrk*
i) -Ote
ii) –o-ote
f) Onyesha vihisishi katika sentensi zifuatazo. (alama 2) *Nrk*
i) Sawa sawa tutakutana kesho.
ii) Nabii Musa! Eti kifaru hula nyama
6. g) Geuza sentensi zifuatazo katika usemi wa taarifa (alama 4) *Nrk*
i) “Mabasi hayapiti hapa siku hizi, kuna nini” Mazrui aliuliza
ii) Karen: Tafadhali usiukanyage mguu wangu
Kadzo: Ah! Mbona niukanyage?
7. Ukitumia mifano mwafaka, tunga sentensi kudhihirisha matumizi mbalimbali ya;
(alama 2) *Nrk*
i) Jinsi
ii) Ikiwa
8. i) Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maelezo. (alama 2) *Nrk*
i) Mchwa wamezila mbao zetu zote. (Anza na mbao)
ii) Sijali hata kama hunipendi. (Andika kinyume)
j) Kamilisha jedwali hili (alama 4) *Nrk*
Kitenzi Kutenda Kutendana
Fa ………………………………. ………………………………
Cha ……………………………….. ……………………………...
9. Ukitumia mchoro wa matawi, onyesha muundo wa sentensi ifuatayo.(alama 4) *Nrk*
Mtoto huyu alikunywa maziwa mengi
10. Tofautisha maana za sentensi hizi. (alama 2) *Nrk*
i) Ningalipandishwa madaraka, ningalinunua gari
ii) Ningepandishwa madaraka ningenunua gari
11. Eleza matumizi ya ni katika sentensi hizi. (alama 2) *Nrk*
i) Njooni kwangu nyinyi nyote
ii) Duniani waja wote ni sawa
n) Taja aina ya vitenzi vilivyopigiwa mstari chini katika sentensi zifuatazo.
12. (alama 2) *Nrk*
i) Huyu ndiye aliyetukomboa.
ii) Baba amekuwa mgonjwa
13. II. a) Eleza maana ya semi zifuatazo (alama 2) *Nrk*
i) Kata bei
ii) Tia ngoa
14. b) Kamilisha majina haya ya makundi. (alama 2) *Nrk*
i) Mkungu wa ……………………………………………………………………..
ii) Thurea ya ………………………………………………………………………
c) Andika visawe vya; (Alama 2) *Nrk*
i) Sarafu …………………………………………………………………………..
ii) Daktari ………………………………………………………………………….
4. ISIMUJAMII
15. (a) Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata (alama 10) *Nrk*
A: Habari yako ndugu
B: Ndugu…… Ahh! (Anamsogelea) Bwana asifiwe!
A: Asifiwe sana ndugu!
B: Amen! Ahh ndugu yangu, imekuwa vipi umepotea hivyo?
A: Usiwe ha hofu ndugu. Nilikuwa nimeenda kuhubiri huko Nakuru. (Anatua kidogo).
Ilinibidi niende huko, ili kutimiza amri ya Bwana.
B: Eeh, hata Yohana alienda kuhubiri ……………
A: Habari ya siku nyingi?
B: Nzuri, Bwana ameendelea kunineemeshea baraka zake
A: Amen!
B: Nimeona mkono wake katika kila jambo
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Amen
A: Ameendelea kunibariki sana. Shetani hana nafasi katika maisha yangu
B: Shetani ashindwe
A: Ashindwe Ibilisi.
Maswali
16. i) Toa muktadha wa mazungumzo haya. (alama 1) *Nrk*
ii) Taja sifa zozote mbili zilizojitokeza katika mazungumzo haya. (alama 2) *Nrk*
17. iii) Huku ukitoa mifano mitatu onyesha tofauti iliyoko kati ya mazungumzo haya na mazungumzo
yanayoweza kutokea mahakamani. (alama 3) *Nrk*
b) atatizo ya lugha katika matamshi yafuatayo yanasababishwa na nini? Andika lugha sanifu
(i) Nipeko jai nikunyenge wakati nikikungojeanga (alama 1)*Nrk*
(ii) Tsambi sangu sote simeoswa na tamu ya Yesu. (alama 1) *Nrk*
(iii) Alienda kukojoa baada yake kuhara. (alama 1) *Nrk*
iv) Mimi ninakuja kwa hapa. (alama 1) *Nrk*






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers