Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Narok District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Narok District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/3
KISWAHILI (FASIHI)
SEHEMU A.
1. FASIHI SIMULIZI (ALAMA 20) *Nrk*
Soma utungo ufuatao halafu ujibu maswali uliyoulizwa.
Hapo zamani za kale mamba na tumbiri walikuwa marafiki wakubwa sana. Siku moja mamba
akamwendea rafiki yake tumbiri na kumwambia. “Rafiki yangu” Tumbiri akaitikia, “Naam”
Mamba akajiandaa na kusema, “Siku zote mimi ndiye nijaye nchi kavu kukutembelea. Mbona
wewe huji kwangu majini kunitembelea?” Tumbiri akawaza na kujibu, “sasa nitakuja vipi mimi na sijui kuogelea?”Mamba akamwambia, “Ahh hilo tu? Panda mgongoni kwangu, nitakuchukua
mpaka nyumbani.” Tumbiri akapanda, safari ya kwenda kwa mamba ikaanza.
Wakaenda pa! pa! pa! walipofika katikati ya mto mamba akamwambia, “Si unajua rafiki kuwa
ninakupenda sana?” Tumbiri akaitikia, “Naam!” Mamba akaendelea, “Sasa huko kwetu mtu
akimpenda mwingine sana hula moyo wake. Basi nipe moyo wako niule!” Tumbiri akawaza,
akawaza wee mpaka akapata la kusema. “Ahh moyo wangu? Mbona basi hukuniambia tangu hapo?
Mimi kawaida huuacha moyo wangu nyumbani. Basi turudi nikakuchukulie rafiki yangu”. Mamba
akageuka paap! Akarudi nchi kavu huku ana matumaini makubwa. Tumbiri akachapa mbio na
kukimbilia mtini. Alipokuwa huko juu akatunda embe na kumrushia mamba akisema, “Moyo
wangu huo!” Mamba akalikimbilia embe hilo kwa kudhani ni moyo wa tumbiri. Alishindwa
kuuona moyo huo kutokana na matope ya mtoni. Mpaka leo mamba anaonekana akizunguka
kuutafuta moyo wa tumbiri. Tumbiri naye hathubutu tena kumkaribia Mamba.
MASWALI
a) i) Hii ni ngano ya aina gani? (alama 1) *Nrk*
ii) Je, ni wasifu gani wa kitabia unawakilishwa na mamba? (alama 3) *Nrk*
iii) Eleza sifa tatu kuu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika ngano hii
(alama 3) *Nrk*
iv) Ikiwa utaiwasilisha ngano hii mbele ya hadhira ni mambo gani utakayosisitiza katika
uwasilishaji huo? (alama 3) *Nrk*
b) (i) Eleza umuhimu wa vitanza-ndimi (alama 2) *Nrk*
(ii) Taja sifa mbili za vitendawili (alama 2) *Nrk*
(iii) Taja na uelezee umuhimu wa vitendawili (alama 6) *Nrk*
SEHEMU YA B. TAMTHILIA
KIFO KISIMANI- KITHAKA WA MBERIA
1. AMA
Eleza jinsi mfumo wa utawala wa Mtemi Bokono unavyodhihirisha udikteta
(Utawala wa kimabafu ) (alama 20) *Nrk*
AU
2. a) Je, mbinu rejeshi imetumika vipi katika tamthilia ya Kifo Kisimani? (alama 10) *Nrk*
b) Eleza matumizi ya Jazanda zifuatazo katika tamthilia ya Kifo Kisimani
(alama 10) *Nrk*
(i) Kisima
(ii) Mkate wa wishwa
(iii) Jiwe
(iv) Jua
(v) Tupa aliyopelekewa Mwelusi
SEHEMU YA C (RIWAYA) MWISHO WA KOSA – Z. Burhani
AMA
I Soma dondoo hili kisha ujibu maswali yafuatayo (alama 20) *Nrk*
“Ninajua hayo. Juu ya hivyo sidhani kuwa tunaweza kufanya lolote. Hatuwezi kuyaingilia, hayo
ni maisha yao. Ni yeye tu, Muna, atakayeweza kutenda lolote.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) *Nrk*
b) Mzungumziwa alikuwa na nia gain? (alama 4) *Nrk*
c) Ni kwa vipi msemaji anaweza kulaumiwa kwa kuchangia katika jambo analolishughulikia?
(alama 4) *Nrk*
d) Eleza visababisho vinne vya ugomvi kati ya Muna na Hasani (alama 4) *Nrk*
e) Linganisha na utofautishe wahusika Muna na Monika (alama 4) *Nrk*
AU
2. “Mvunja nchi ni Mwananchi” Onyesha ukweli wa methali hii ukizingatia yale yaliyomo
katika Mwisho wa Kosa (alama 20) *Nrk*
SEHEMU D. USHAIRI
Soma shairi lifuatalo, kisha ujibu maswali; (alama 20) *Nrk*
Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwendani,
Afiya yangu dhahili, mno nataka amani,
Nawe umenikabili, nenende sipitalini,
Sisi tokea azali, twenda zetu mizimuni,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mababu hawakujali, wajihisipo tabani,
Tuna dawa za asili, hupati sipitalini,
Kwa nguvu za kirijali, mkuyati uamini,
Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele Fulani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mtu akiwa halali, tumbo lina walakini,
Dawa yake ni subili, au zongo huauni,
Zabadi pia sahali, kwa maradhi yalondani,
Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini,
Dakitari k’ona mwili, tanena kensa tumboni,
Visu vitiwe makali, tayari kwa pirisheni,
Ukatwe kama figili, tumbo nyangwe na maini,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Japo maradhi dhahili, kuteguliwa tegoni,
Yakifika sipitali, huwa hayana kifani,
Wambiwa damu kalili, ndugu msaidieni,
Watu wakitaamali, kumbe ndiyo buriani,
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mizimu wakupa kweli, wakueleze undani,
Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani,
Ulete kuku wawili, wa manjano na kijani,
Matunda pia asali, vitu vyae chanoni,
Nafwatani sipitali, na dawa zi mlangoni?
MASWALI – USHAIRI (ALAMA 20) *Nrk*
a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili. (alama 2) *Nrk*
b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili? (alama 2) *Nrk*
c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitali? (alama 4) *Nrk*
d) Kwa kuzingatia muundo wa shairi hili, eleza mbinu zilizotumika (alama 6) *Nrk*
e) kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi? (alama 2) *Nrk*
f) Andika maana ya maneno yafuatayo yalivyotumika katika shairi (alama 4) *Nrk*
i) Dhahili
ii) Azali
iii) Sahali
iv) Tumbo nyangwe
SEHEMU E
1. HADITHI FUPI
K.W. Wamitila (Mh) Mayai waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine.
Soma dondoo lifuatalo halafu ujibu maswali uliyoulizwa. Dondoo hili limetolewa kutoka hadithi fupi
K.W Wamitila ya “Kachukua Hatua Nyingine”
“ Mwulize mzee Mavitu naye, “pesa zikiwaona maskini zinakimbia” Mara mbili-tatu alishamweleza
mkewe kuwa hali ikiendelea jinsi hii, “nitachukua hatua nyingine” moyoni kwa shemeji Mavitu
alikuwa “Bwana Hatua Nyingine”, kusema kweli Mavitu alijua fika kuzichukua hatu”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4) *Nrk*
b) Taja hatua sita alizozichukua Mavitu na ueleze matokeo yake. (alama 12) *Nrk*
c) Kwa kuzingatia mkondo mzima wa hadithi fupi hii, onyesha tofauti kati ya wahusika wawili
wanaozungumziwa katika dondoo hili. (alama 4) *Nrk*






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers