Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nyamira District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Nyamira District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/3
KISWAHILI FASIHI
USHAIRI
1. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha ujibu maswali.
Niokoa Muokozi, uniondolee mashaka.
Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika
Nimekithiri simanzi, ni katika kuudhika
Mja wako nasumbuka, nipate niyatakayo.
Mja wako nasumbuka, nataka kwao afua
Nirehemu kwa haraka, nami nipate pumua
Naomba hisikitika, na mikono hiinua
Mtenda ndiwe Moliwa, nipate niyatakayo.
Mtenda ndiwe Moliwa, we ndiwe Mola wa anga
Mazito kuyaondoa, pamoja na kuyatenga
Ukauepusha ukiwa, ya pingu zilonifunga
Nikundulia muwanga, nipate niyatakayo
Muwanga nikundulia, nipate toka kizani
Na huzuni n’ondolea, itoke mwangu moyoni
Mambo mema niegheshea, maovu nisitamani.
Nitendea we Manani, nipate niyatakayo.
Igeuze yangu nia, dhaifu unipe mema
Nili katika dunia, kwa afia na uzima
Moliwa nitimizia, yatimize yawe mema
Nifurahike mtima, nipate niyatakayo.
(a) Shairi hili ni la bahari gani? Eleza. (alama 2) *Nym *
(b) Taja madhumuni ya shairi hili. (alama 3) *Nym *
(c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4) *Nym *
(d) Thibitisha namna uhuru wa kishairi unaibuka katika shairi. (alama 4) *Nym *
(e) Andika ubeti wa pili katika lugha sufufu. (alama 4) *Nym *
(f) Toa maana ya:
(i) Nimedhikika
(ii) Muwanga nikundulia
(iii) Nifurahike mtima (alama 3) *Nym *
TAMTHILIA
Kifo kisimani: Kithaka wa Mberia
2. Jadili namna mwandishi ametumia mbinu rejea na sadfa katika kuendeleza tamthilia kifo
Kisimani (alama 20) *Nym *
3. ‘Ndiyo hukuwepo! Bafe pia hakuwepo! Nyinyi wawili hamkuwepo!
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4) *Nym *
(b) Eleza sifa zozote nne za msemaji katika dondoo hili. (alama 4) *Nym *
(c) Eleza mbinu zozote tatu zinazoambatana na dondoo hili. (alama 6) *Nym *
(d) Ni mambo yapi makuu yaliyotatiza juhudi za ukombozi katika nchi ya Butangi?
(alama 6) *Nym *
RIWAYA
MWISHO WA KOSA: Z. Burhani.
4. Riwaya ya mwisho wa kosa ni riwaya ya migogoro kadhaa. Kwa kurejelea riwaya yenyewe
tambua na ueleze asili na hatima ya migogoro yoyote minne. (alama 20) *Nym *
5. “Nitakupa hiki, ukiweke mpaka nitakapokuletea hizo pesa, ………………….
(i) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4) *Nym *
(ii) Tukio la uneni huu linabainisha hisia/ mbinu zipi za uandishi? Eleza (alama4) *Nym *
(b) Mwandishi wa riwaya ya mwisho wa kosa amesawiri elimu ya juu kuwa kizingiti dhidi ya
ukuzaji na udumishaji wa maadili katika jamii. Huku ukitoa mifano minne, fafanua kauli hii.
(alama 12) *Nym *
HADITHI FUPI
6. Yale maneno yalipokezanwa. Mwenye gari ambaye alishakiteremsha kioo chake alipoyasikia
mwanzo aliweza kuapa kuwa asingefanya hilo asilani. Lakini walichachawa. Alitoka garini
polepole kwa hadhari ya kutotaka kuchafuliwa na maji machafu yaliyokuwa pale chini.
(msamaria mwema: k.w Wamitila)
(a) Eleza mandhari ya hadithi hii fupi. (alama 4) *Nym *
(b) Ni nini kilichokuwa kimetokea muda mfupi kabla ya dondoo hili? (alama 6) *Nym *
(c) Kulingana na dondoo, mwenye gari anaonekana mtu asiye na utu na mjaa maringo.
Fafanua. (alama 4) *Nym *
(d) mtunzi wa hadithi ‘Msamaria Mwema’ ametumia vema mbinu za tashhisi, tashbihi na methali.
Eleza huku ukitoa mifano.
(alama 6) *Nym *
FASIHI SIMULIZI
7. (a) Fasihi simulizi ni sanaa yenye dhima muhimu katika jamii ya kisasa. Dhihirisha ukweli wa usemi huu kwa kurejelea vipera vifuatavyo;
(i) Nyimbo (alama 4) *Nym *
(ii) Mafumbo (alama 4) *Nym *
(iii) Vitendawili. (alama 4) *Nym *
(iv) Mighani. (alama 4) *Nym *
(b) Eleza sifa muhimu zinazobainisha fasihi simulizi. (alama 4) *Nym *






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers