Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Teso District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Teso District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/2
KISWAHILI
UFAHAMU ( ALAMA 15)
1. Soma tarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Jamii yoyote ile ulimwenguni haiwezi kukua, kuimarika na kuendelea bighairi ya kuwatunza na
kuwaenzi watoto wake. Watoto ni mbegu ya jamii ya kesho na kama mbegu hiyo haikutunzwa
ipaasavyo jamii ya kesho haitakua na endapo itakua itadumaa na kushindwa kuendelea. Ili
kuhakikisha kuwa watoto wametunzwa ipasavyo, inaijuzu jamii nzima kufanya kulihali kuhakikisha kuwa watoto wake wamepata elimu ifaayo, afya inayowastahiki, ulinzi murua na usalama unaostahili.
Jamii hiyo lazima ithamini haki za kibinadamu alizo nazo mtoto.
Serikali zote uilmwenguni zinapaswa kuthamini na kuenzi Muafaka kuhusu Haki za Mtoto. Nchi nyingi ulimwenguni zimekwisha kuafiki Muafaka kuhusu haki za mtoto. Muafaka huo unahakikisha kuwa zinaridhia kuhakikisha kuwa haki za mtoto hazitakiukwa na endapo zitakiukwa ziko tayari kukubali ukiukwaji huo mbele ya jumuiya ya ulimwengu mzima. Muafaka huo unashadidia haki za kimsingi za mtoto popote pale na bila ya ubaguzi. Haki hizi ni haki ya kuishi, haki ya kujiendeleza ipasavyo; haki ya kulindwa dhidi ya taathira mbaya, kudhalilishwa au unyanyasaji wa jinsi yoyote ile; kushiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii, kiuchumi na hata kisiasa pamoja na dhidi ya kongwa la ajira.
Katika mataifa mengi, watoto wamesakamwa na wingi wa matatizo. Mathalan, kusokomezwa kwenye vita vya kikabila, ajira ya watoto, unyanyasaji wa kijinsia na maovu mengine ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu. Zipo nchi ambapo watoto wanaoishi katika maeneo ya mashambani wana fursa chache za kupata elimu ifaayo na afya ya kimsingi wakilinganishwa na wenzao wanaosakini katika maeneo ya mijini.
Muafaka huu unasisitiza kuwa kuwepo kwa tofauti za jinsi hii katika jamii ni ukiukaji wa haki za kibinadamu. Inahalisi serikali za nchi hizo kuhakikisha kuwa hali hizi zimefilia majinani.
SEHEMU YA A: UFAHAMU ALAMA 15
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuatia
(a) Kwa nini jamii ya kesho inategemea hali nzuri ya watoto? (alama1) *Tso*
(b) Ni hatua gani kuu ambazo zafaa kuchukuliwa kuhakikisha kuwa watoto wanatunzwa ipasavyo?
(alama4) *Tso*
(c) Eleza haki zozote mbili za kimsingi walizo nazo watoto. (alama4) *Tso*
(d) Taja dhiki wanazokumbana nazo watoto. (alama3) *Tso*
(e) Eleza maana ya vifungu hivi vilivyotumika katika kifungu: (alama 3) *Tso*
(i) bighairi ya
(ii) Kufanya kulihali
(iii) Kongwa la ajira
MUHTASARI
2. Soma taarifa hii kisha ujibu maswali:
Ukeketaji ni mfumo wa upasuaji unaofanyiwa wanawake na wasichana sehemu nyingi duniani. Istilahi hii ya ukeketaji ina maana pana kwani inaweza kutumiwa kuelezea upashaji tohara kwa wasichana na ukataji wa sehemu za siri kwa wanawake.
Ukeketaji haupatikani tu katika bara la Afrika bali katika sehemu nyingi ulimwenguni. Umri ambapo ukeketaji hufanyika hutegemea jamii inayohusika. Mwanamke anaweza kufanyiwa ukeketaji siku chache baada ya kuzaliwa au baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza. Miongoni mwa jamii ambazo hupasha tohara wanawake, huthamini sana amali hii kwani kwao ni hatua muhimu ya mpito wa maisha katika jamii za jadi mwanamke hupitishwa kutoka rika moja hadi lingine, yaani kutoka utotoni na kuingia kwenye utu uzima. Ukeketaji unafungamana na sherehe ya kuwapa wasichana mafunzo kuhusu kanuni za uzazi, malezi na ndoa. Dhima kuu ya sherehe hiyo ya kuwapasha wasichana tohara inadaiwa ya kwamba ni kuwapunguzia wanawake uchu na kuhifadhi ubikira. Jamii nyingine hutekeleza tohara kwa sababu za kidini zinazoshikilia kuwa mwanamke aliyetahiriwa huwa nadhifu. Wengine wanaamini kuwa tohara huwafanya watoto wanapozaliwa kuwa na nafasi nzuri ya kuishi, ilhali wengine hupashwa tohara ili wapate waume wa kuwaoa. Kwenye jamii ambazo wanaume wanasisitiza tohara kama kigezo cha mwanamke kuolewa ukeketaji umeshamiri. Katika jamii kama hizi wanaume huwa hawataki kuoa wanawake ambao hawajatahiriwa.
Wanawake wenyewe huhakikisha ya kwamba watoto au wajukuu wao wanapelekwa kupashwa tohara.
Wakati mwingine mipango ya siri hupangwa na kina mama hao pamoja na mangariba, kuhakikisha
kuwa jambo hili linatekelezwa. Kwa hivyo jambo hili la ukeketaji lina utata miongoni mwa jamii nyingi ulimwenguni.
Hata hivyo ukweli ni kwamba swala zima hili la ukeketaji lina madhara makubwa na linamdhalilisha mwanamke. Katika hali ya upashaji tohara wanawake huvuja damu nyingi na aghalabu huaga dunia.
Wale wanaopona huwa kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa ambayo huharibu sehemu za
uzazi. Kwani madaktari wanadai uchungu wa uzazi huwa mwingi na hudumu muda mrefu.
Kwa sababu tohara hufanywa mara moja kwa mwaka, wasichana wote wa rika moja hukusanyika
mahali maalum ili kufanyiwa tohara. Kifaa ambacho hutumiwa sana ni wembe. Wembe huo hutumiwa kuwakatia wasichana wote ambao wanapashwa tohara katika kipindi hicho. Wembe huo hauchemshwi anagalau kuua viini vinavyosababisha na kueneza magonjwa mbalimbali. Hali hii huwaweka wasichana hao kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa hatari wa ukimwi. Licha ya hivyo wasichana waliotahiriwa nguvu za kinga dhidi ya magonjwa hupungua. Kwa hivyo wanaweza kupata magonjwa mengine ya kuambukiza kwa urahisi. Kwa hivyo ukeketaji ni tendo la hatari na la kumdhalilisha mwanadamu ambalo linastahili kulaaniwa.
(a) Ukizingatia mambo muhimu anayoeleza mwandishi, fupisha aya tatu za kwanza.
Maneno (60-70) (alama 9) *Tso*
Nakala chafu.
Nakala safi.
(b) Eleza mambo anayoeleza mwandishi katika aya mbili za mwisho. Maneno 40-50
(alama 6) *Tso*
Nakala chafu.
Nakala safi.
MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
3. a) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi. (alama 2*Tso*
(i) Sujudu
(ii) Haribu
(iii) Hiliki
(iv) Abiri
b) Onyesha silabi inayowekewa shadda kwenye maneno haya. (alama 4) *Tso*
(i) Karatasi
ii)Samahani
c) Akifisha kifungu kifuatacho (alama 3) *Tso*
Karibu mgeni akaitikia mwenyeji mbona huingii na mlango u wazi naam stareheni kwenye kiti
ahsante wakajibu.
d) Andika sentensi hizi kwa udogo. (alama 2) *Tso*
(i) Mlete huyo mwizi afunguliwe mashtaka.
(ii) Sijui kwa nini hindi lake ni bichi
(e ) Andika sentensi hii kulingana na maagizo. (alama 2) *Tso*
Chombo kilichozama kiliandikishwa uingereza.
(Maliza kwa kiliandikishwa)
(f ) Onyesha kinyume cha vitenzi vifuatavyo. (alama 2) *Tso*
(i) Epua
(ii) Tapanya
(iii) Nena
(iv) Unga
(g) Kanusha ( alama 3) *Tso*
(i) Chovi angekuwa na bidii angependwa na wengi.
(ii) Kilima kwake kulisifiwa sana.
(iii) Ukicheza na moto utachomeka.
h) Geuza kwa wingi. (alama 2) *Tso*
(i) Njia hii huenda Kisumu
(ii) Wembe huu utafaa.
i) Tumia kauli ya kutendesha katika sentensi zifuatazo:. (alama 2) *Tso*
(i) Mukhwana alikunywa pombe mpaka akalewa sana
(ii) Tafadhali hakikisha Omari ameelimika vizuri
j) Changanua sentensi hii. (alama 4) *Tso*
Watoto wanafanya kazi zao lakini wazazi wanazungumza sana.
k) Geuza katika msemo wa taarifa. (alama2) *Tso*
“Lo! Siamini kuwa yule mtoto aliyetaabika vile ameishia kupata udhamini” Alisema Mariamu
l) Sahihisha sentensi zifuatazo. (alama2) *Tso*
i)Hao mandugu wamekosana juu ya pesa.
ii) Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.
m) Eleza matumizi ya KWA katika sentensi zifuatayo: (alama 2) *Tso*
(i) Wanawake kwa wanaume walifika mkutanoni.
(ii) Yule mtaalam alielezea maana ya utandawazi kwa ufasaha.
n) Fafanua maana mbili zinazojitokeza katika sentnsi hii.
(alama 2)
Jambazi lilimwibia Okoth gari jipya.
o) Tunga sentensi kubainisha maana tofauti ya maneno haya; (alama 2) *Tso*
i) Dalili
ii) Dhalili
p) Toa neno jingine lenye maana sawa na; (alama3) *Tso*
i) Karadha
ii) Mtaji
iii) Mshitiri
q) Eleza maana ya misemo hii. (alama2) *Tso*
i) Umbo la mkonge
ii) Kupata hiji wa hoja
r) Eleza maana ya methali ifuatayo: (alama2) *Tso*
Akikalia kigoda mtii.
SEHEMU YA D. ISIMU JAMII (alama10) *Tso*
4. Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
“Karibu wageni karibuni
Come and learn with us lugha ya kiswahili.
Nyote mtabenefit sana”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu its a national language”
a) Lugha ngapi zimetumika katika muktadha huu?
b) Mtindo wa kutumia lugha zaidi ya moja katikia mazungumuzo huitwaje?(alama2) *Tso*
c) Eleza sababu za wazungumzaji kutumia lugha zaidi ya moja. (alama5) *Tso*
d) Mzungumzaji mwenye uwezo wa kutumia lugha zaidi ya mbili anaitwaje?(alama2) *Tso*






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers