Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Teso District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Teso District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2006
102/3
KISWAHILI (FASIHI)
Swali la kwanza.
Fasihi simulizi
1. Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale, Murungu (Mungu) alimtuma Kinyonga kwa watu. Alimwambia; “Nenda
kwa waja wangu na uwaeleze kuwa mtu akifa, awekwe nyuma ya nyumba na baada ya siku
mbili atafufuka’’.
Kinyonga akaanza safari. Alitembea polepole. Akapanda milima na kuvuka mabonde. Njiani
akakutana na Sungura.
Sungura akamuliza, “Unaenda wapi Kinyonga?” Kinyonga akamjibu, “Naenda kwa watu
kuwapelekea ujumbe kutoka kwa Mungu kuwa mtu akiaga dunia awekwe nyuma ya nyumba
kwa muda wa siku mbili kisha ataweza kufufuka”.
Sungura hakufurahia jambo hilo.
Akamwabia Kinyonga kwa vile ana mbio, amwachie jukumu hilo apeleke ujumbe huo kwa
watu. Kinyonga hakukubali. Hivyo, Sungura alimwacha Kinyonga na kuchana mbuga.
Sungura alikimbia kukuru kakara kukuru kakara hadi kwa watu. Alipowasili aliwaambia,
“Nimetumwa na Mungu,” Watu waliposikia hivyo, wakafungua, masikio yao. “Nimeambiwa
na Mungu kuwa mtu akifa, afe alale na kuzikwa mara moja’’ Nusura watu wamuue kwa kuleta
ujumbe huo. Wengine walitaka kumfanya kitoweo lakini Sungura akatoroka.
Sungura akiwa njiani kurudi alimwona Kinyonga kwa mbali. Akajificha kichakani. Sungura
alisukuma jiwe kubwa akilielekeza alikokuwa Kinyonga. Jiwe lilimwangukia Kinyonga pu! Na
kumuua papo hapo.
Sungura alipofika kwa Mungu na kumweleza aliyowaambia watu, Mungu alikasirika ja mkizi.
Alimvuta Sungura masikio yakawa marefu na kumwonya Usiseme uwongo tena’’.
Kinyonga hakufikisha ujumbe sasa watu huamini ujumbe wa kweli kutoka Mungu. Mpaka sasa
watu huamini ujumbe ulioletwa na Sungura.
Maswali
(a) (i) Hii ni hadithi ya aina gani? (alama1) *Tso*
(ii) Toa sababu (alama1) *Tso*
(b) Ni sifa zipi zinazotambulisha kuwa hadithi ni ya fasihi simulizi? (alama3) *Tso*
(c) Ni mafunzo gani yanayopatikana katika hadithi hii. (alama3) *Tso*
(d) Fafanua jinsi matumizi ya lugha yanavyodhihirika katika hadithi hii. (alama3) *Tso*
(e) Eleza umuhimu wa hadithi katika jamii. (alama4) *Tso*
(f) Hizi ni nyimbo aina gani? (alama3) *Tso*
(i) Bembezi
(ii) Wawe
(iii) Nyiso
(g) Taja sifa zozote za vitendawili. (alama2) *Tso*
SEHEMU YA B: TAMTHILIA
KIFO KISIMANI: Kitheka Wamberia.
2. Tamthilia ya kifo kisimani inaeleza kwa tafsili uhalisia wa mambo yanayotendeka katika bara letu.
Thibitisha. (alama 20) *Tso*
3. “Nasikia mkewe ni chui kasoro mkia na manyoya. Nasikia alimshambulia mwanamke mmoja kwa
maneno”
(a) Weka dondoo hili katika muktadha. (alama 4) *Tso*
(b) Taja na utoe ithibati mbinu ya sanaa iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2) *Tso*
(c) Simulia yaliyotokea baada ya dondoo hili . (alama 4) *Tso*
(d) Taja sifa za yule anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 10) *Tso*
SEHEMU YA C
RIWAYA
MWISHO WA KOSA : Z. Burhani
4. Onyesha ufaafu wa anwani “Mwisho wa kosa’’ ( alama 20) *Tso*
5. “Nieleze hasa sababu ya kuumwaga uji wangu namna ile, ndio nini? “Ndio mchafu kuunywa leo?
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. ( alama 4) *Tso*
b) Ni kina nani wanaorejelewa katika muktadha wa dondoo hili? (alama 2) *Tso*
c) Eleza kwa kina tabia za aliyemwaga uji. ( alama 10) *Tso*
d) Unajifunza nini kutokana na tabia hizi. ( alama 4) *Tso*
SEHEMU YA D
HADITHI FUPI
Mayai waziri wa Maradhi.
6. Taja na ueleze kwa kina maudhui yanayojitokeza katika hadithi hii “Mayai waziri wa maradhi”.
( alama 20) *Tso*
Msamaria mwema – Na K.W. Wamitila
7. “Akilini alikuwa akiyacheua mafundisho ya leo kanisani, alikwenda kwa ajili ya kukipata chakula
cha kiroho”
a) Ni nani anayerejelewa?
b) Eleza kwa kirefu masaibu yaliyompata anayerejelewa.
c) Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika hadithi hii.
d) Eleza hulka za Kizito Kibambo.
SEHEMU YA E
USHAIRI
8. SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.
Wataalamu muwe macho, vuani moto muenge,
Muenge hicho ambacho, cha watu wenye mawenge,
Mawenge yenye kijicho, kiswahili wakivunge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Sichafue kiswahili, barakala tuwapinge,
Apige kila hali, wasiguse tuwainge,
Tuwainge wende mbali, kiswahili tujijenge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Sichafue yetu lugha, waharibu Wabanange,
Wabanange iwe nyagha, waiweke tengetenge,
Lugha kuitwa; ulugha, lafidhi watia denge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Tuichange heshima, na ulugha tuupinge,
Tuhifadhi kwa salama, na kisingio unyonge,
Kelele za maamuna, si watu ni visinge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Kasema sheikh Amri, kiswahili tukisenge,
Kistawi kinawiri, kitumike kwenye bunge,
Hii ni yetu fahari, lugha yetu tuichunge.
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
Kikipatwa na maradhi, kwa sindano tukidunge,
Kila jama kutidhi, kipatwe hapo tupunge,
Tukitia mfawadhi, kama kunde na kihenge,
Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.
MASWALI
(a) Ni mtindo gani aliotumia mshairi katika kutunga ubeti wa 1 na 2. (fafanua kwa kutoa mfano)
(alama 4) *Tso*
(b) Mshairi ametoa mapendekezo kadha katika shairi kuhusu jinsi ya kuimarisha na kuhifadhi
lugha ya kiswahili. Taja na ufafanue matano kati ya hayo. (alama 5) *Tso*
(c) Mshairi anazungumza na akina nani? Anazungumzia nini? (alama 4) *Tso*
(d) Mshairi ametumia tamathali mbalimbali kuwasilisha ujumbe wake. Taja mifano mitatu tofauti ya tamathali hizo. (alama 3) *Tso*
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 4) *Tso*
(i) Muenge
(ii) Barakala
(iii) Mtawadhi
(iv) Maamuma.
9. SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWAHILI
Haki ya mtu thawabu, kudai sitasita,
Hata nipatishe tabu, muhali mimi kukita,
Kulitenda la wajibu, liwe hai au mata,
Nitafanya majaribu, na inapobidi matata,
Haki yangu taidai, hata iwe ni kwa vita.
Haki ya mtu u’ngwana, siseme mimi nateta,
Sitaukiri ubwana, na jeuri unoteta,
Na ikiwa ni kuwana, sitajali sitajuta,
Haki yangu ¢taidai, hata iwe ni kwa vita.
Haki ifukie chini, ipige na kuibuta,
Tumbukize baharini, tazamia kuifwata,
Ukaifiche milimani, nitakwenda kuiteta,
Itundike milimani, nitawana kupata,
Haki yangu ¢taidai, hata iwe ni kwa vita.
Haki ijengee ng’ombe, izingushie na kuta,
Na fususi sisimame, iwe inapitapita,
Tainuka nishikame, haki yangu kukamata,
Sifa kubwa mwanamme, kwenenda huku wasota,
Haki yaungu ¢taidai, hata iwe ni kwa vita.
Tangawana siuuzi, kwa vijugu au kashata,
Ahadi za upuuzi, na rai kuitaita,
Kwa kila alo maizi, hawi mithili ya bata,
Tope yake makaazi, na chakula cha kunata,
Haki yaungu ¢taidai, hata iwe ni kwa vita.
MASWALI
(a) Eleza maana ya kibwagizo cha shairi hili. (alama 1) *Tso*
(b) Eleza muundo wa shairi hili. (alama5) *Tso*
(c) Mshairi yuko tayari kufanya nini ili aipate haki yake? (alama4) *Tso*
(d) Shairi hili lina umuhimu gani kwa msomaji na nchi kwa ujumla? (alama2) *Tso*
(e) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 5) *Tso*
(f) Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumiwa katika shairi. (alama 3) *Tso*
i) Mata
ii) Maizi
iii) Fususi
More Question Papers