Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Butere/Mumias District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Butere/Mumias District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Nambari. …………………….
Shule ………………………………………………...
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI / AGOSTI. 2007
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUTERE MUMIAS-2007
Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI YA 3
JULAI / AGOSTI. 2007
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO
• Jibu maswali manne
• Swali la kwanza ni la lazima
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
2. Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungeliona, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
3. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
4. Walakini subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti,
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
5. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezewe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
6. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati ,
Sote tungeambatana, pa kulima hatupati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
7. Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana , ingelikuwa ni bahati,
Vipi tungelisukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
8. Mbele sitakwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaeleni waungwana, shauri yake jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
MASWALI
a) Shairi hili ni la bahari gani? (alama 2)
b) kwa kutoa mifano mwafaka onyesha jinsi mtunzi wa shairi hili alivyotumia
uhuru wa utunzi (alama 2)
c) Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
c) Andika ubeti wa tano katika lugha nathari. (alama 4)
d) Tambulisha mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi (alama 4)
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi
i)katiti
ii) yakuti
iii) Hatuwati
iv) Nasukuti (alama 4)
SEHEMU B
KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA
2. Eleza jinsi utawala wa mtemi Bokono unavyodhihirisha udikteta. (alama 20)
AU
3. “ --- kimoja hakipo tena kimenyakuliwa na kozi. Mheshimuni kozi.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
(alama 4)
c) Kipi kinachonyakuliwa na kina umuhimu upi? (alama 6)
d) Fafanua sifa za mnenaji (alama 6)
SEHEMU YA C
MWISHO WA KOSA
4. Jadili jinsi mwandishi alivyoisawiri jinsia ya kike (alama 20)
Au
“Ninajua hayo. Juu ya hivyo sidhani kuwa tunaweza kufanya lolote. Hatuwezi kuyaingilia,
hayo ni maisha yao. Ni yeye tu Muna, atakayeweza kutenda lolote”.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Mzungumziwa alikuwa na nia gani. (alama 4)
c) Kwa vipi msemaji anaweza kulaumiwa kwa kuchangia katika jambo analolishughulikia.
(alama 4)
d) Eleza visababisho vinne vya ugomvi kati ya Muna na Hasani. (alama 8)
SEHEMU YA D
HADITHI FUPI: MAYAI WAZIRI WA MARADHI
6. Eleza maswala yafuatayo jinsi yanavyojitokeza katika hadithi ya mayai waziri wa maradhi.
a) Ukombozi
b) Uongozi mbaya
c) Elimu
d) Ushirikina (alama 20)
AU
7. Majuto ni mjukuu, Onyesha ukweli wa methali hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
a) Uteuzi wa moyoni.
b) Ndimi za mauti.
c) Pwaguzi
d) Fumbo la mwana. (alama 20)
SEHEMU YA E
FASIHI SIMULIZI
8. a) Taja na ueleze aina zozote tano za Hadithi. (alama 5)
b) Tofautisha kati ya
(i) Mbolezi na Bembezi
(ii) Vitendawili na chemsha bongo. (alama 4)
c) Eleza umuhimu wa vitanza ndimi (alama 3)
d) Taja na ueleze sifa nne ambazo mtambaji anapaswa kuwa nazo. (alama 4)
e) (i) Fafanua maana ya methali. (alama 2)
(ii) Taja methali zinazohusu:
a) Kilimo
b) Kuliwaza. (alama 2)
MWISHO






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers