Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Kakamega District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper
Kakamega District Mock - Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2007
JINA: …..………………………………………………………………… NAMBARI: ………..……
SHULE:………..……………………………………………………………………………………...…
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI / AGOSTI 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
KAKAMEGA
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI
(K.C.S.E) 2007
102/2
KISWAHILI
LUGHA
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
Andika jina lako na nambari yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
Jibu maswali yote.
Majibu yako yaandikwe katika kijitabu cha maswali
Watahiniwa wanaweza kuadhibiwa ikiwa hawatafuata maagizo yaliyotolewa katika karatasi
hii.
1. UFAHAMU
Soma taarifa hii kasha ujibu maswali.
Asifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiyo pingika, na kuutilia shaka ni sawa na kudai jua linaweza kubadilika na kuchomoza upande wa magharibi badala ya mashariki. Huu ndio ukweli uliodhihirika juzi katika vyombo vyetu vya magazeti.
Lisemwalo lipo, nakama halipo li njiani. Waama, pafukapo moshi pana moto.mwanafunzi
mmoja wa kike kwa jina P.N. katika chuo kikuu kimojawapo nchini aliushangaza umma wa
Kenya na ulimwengu kwa jumla alipodai kuwaambukiza wanafunzi wenzake wa kiume mia moja
na ishirini na wanee virusi vya ukimwi.
Kisa na maana? Aliambukizwa ukimwi na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akifanya
majaribio ya ualimu katika shule yao ya upili.baada ya kushawishika sana, alijuana naye kimwili,na matokeo yakawa kifo ambacho sasa alikuwa anawagawia wenzake.
Kisa kama hiki kinachangia kueleza kina kirefu cha kutamauka na upweke ambao maisha ya
waja wengi yameingia kiasi cha kuwaacha wanyama ijapo wanaenda kwa miguumiwili bado.
Katika mojawapo ya mafunzo ya kidini ambayo padre alinifunza mimi na wanafunzi wenzangu,
tuliambiwa kisasi nichake Mola, sisi waja letu nikushukuru tu. Mbona mwanafunzi kama huyu
kutaka kulipiza?
Ima fa ima, waswahili husema,”Mlaumu nunda na kuku pia.” Huyu mwanafunzi hawezi
kuwachiwa atende alivyotenda. Aliyekula naye raha alikuwa mtu aliyefahamika vyema sana
kwake.isitoshe, huenda wakati huo alikosana na mama na baba kwa kulala nje. Huenda alikosana na ndugu zake kwa kuhepa nyumbani usiku wa manane kwenda kumuona huyo kalameni. Huenda alikosana na mwalimu wake kwa sababu kiburi kilianza kuingia. Kwa vyovyote vile, alikula raha na hastahili kuwaadhibu watu wasio na hatia kufidia makosa yake. Je, kama yeye na huyo jamaa wasingekuwa na ukimwi, raha kiasi gani wangezila hadi leo?
Jamii na watu wote kwa ujumla hawanabudi basi kulaani vitendo vya P.N.vya
kuwaambukiza wanafunzi wenzake virusi huku akijua. Hili nikosa ambalo linastahili adhabu ya
kifo. Dawa yamoto ni moto; adhdabu inastahili kuchukuliwa hgaraka ili P.N.ambaye tayari
amekiri hatia, atiwe nguvuni na adhabu itolewe.
Barua ya P.N. inafafanua jambo jingine sugu kwamba kiwango cha maadili katika vyuo
vyetu kimezorota kiasi cha kufanyiana unyama usiosemeka. Vijana wengi siku hizi wanashiriki
tendo la ngono nje ya ndoa bila ya haya. Huu upotovu wa maadili katika jamii wapaswa
kushutumiwa na wote. P.N. hana sababu yoyote ya kibinadamu , kidini au kitu chochote kile
kudai haki kwa uovu huo wake.
MASWALI
(a) Taja mada mwafaka kwa makala haya Alama 1
………………………………………………………………………………………………
(b) Mwandishi anamlaumu mwanafunzi kwa kosa gani katika aya mbili za kwanza? Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(c) Eleza asili ya tabia za P.N. Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(d) Barua ya P.N. imeonyesha uvumbuzi mpya. Ni upi? Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(e) Fafanua namna P.N. anavyoepuka ukweli. Alama 3
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(f) Ni hatua gani ambayo mwandishi anataka P.N.achukuliwe? kwa nini? Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(g) Eleza vifungu vifuatavyo kwa muktadha wa taarifa Alama 3
(i) Kina kirefu cha kutamauka-
…………………………………………………………………………………………….
(ii) Ima fa ima-
…………………………………………………………………………………………….
(iii)Kufidia makosa yake-
…………………………………………………………………………………………….
2. UFUPISHO
Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke,"Ajizi ni nyumba ya njaa". Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga.
Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa lenye watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao mashambani, kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka, Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo pia lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi ni wale wenye mawazo ya kwamba, lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika; mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wengine ambao hawahusiki.
Mafunzo tunayopata majumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua
mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya Mwanakenya kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu lazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja, "Utengano ni uvundo", Lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu, wakati tunapokosea, lazima tukubali tumekosea na kufanya masahihisho mara moja kwani, "Usipoziba ufa, utajenga ukuta". Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi.
Sisi tukiwa vijana sharti tujishughulishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambola kusikitisha kwamba sisi vijana twashutumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo, amani na upendo, lazima tuwe na bidii, ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo. Tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na
maendeleo, basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama kama kwa utajiri wake. Kwa hivyo basi,
tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba kubwa au ya utajiri.
MASWALI
(a) Ni nini dhamira ya mwandishi? (maneno 20)
Nakala chafu/matayarisho Alama 3(1 utiririko)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
(b) Katika aya ya kwanza, mwandishi anawahimiza vijana kufanya nini ili kuleta maendeleo
nchini? (maneno 30-40)
Nakala chafu Alama 7(1 mtiririko)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
(c) Ni mambo gani yaliyochangia kuzorota kwa maendeleo nchini Kenya kwa mujibu wa
taarifa? (maneno 40-50)
Nakala chafu Alama 8(1 utiririko)
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA
(a) Andika wingi wa ukanushaji wa sentensi zifuatazo.
i) Panga lilitumiwa kukata ulezi wenyewe Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
ii) Kiti kingenunuliwa, walimu wangeketi vizuri ofisini Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(b) Tambua kirai, kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo.
Mtoto aliyepotea jana, amepatikana leo asubuhi Alama 3
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(c) Akifisha kifungu kifuatacho Alama 4
alipokuwa akiagana na mpenziwe jacky alimwandikia anwani yake ambayo ni SLP 6703
panyako kenya Alama 4
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(d) Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii.
Alipoondoka kwao alisafiri kwa ndege hadi kwa kituo cha matatu. Alama 1 ½
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(e) Eleza matumizi ya na katika sentensi hii. Alama 3
Betty na Lumbasi wanaandaliwa chai na mpishi.
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(f) Ainisha aina za maneno katika sentensi ifuatayo.
Aka! mtoto huyu hawaheshimu kizee. Alama 2 ½
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(g) Changanua sentensi hii kwa jedwali.
Wazee walikuwa wakila mle chumbani. Alama 4
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(h) Eleza tofauti kati ya ghuna na sighuna kimatamshi Alama 1
………………………………………………………………………………………………
(i) Tumia Po katika sentensi kubainisha:
(i) Wakati maalum
………………………………………………………………………………………………
(ii) Wakati wowote
………………………………………………………………………………………………
(iii) Mahali
………………………………………………………………………………………………
(j) Tunga sentesi kuonyesha tofauti ya vitate vifuatavyo Alama 2
– Mjuzi
– Mjusi
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(k) Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa.
Mbuzi wa kike aliuharibu mche wangu. Alama 2
……………………………………………………………………………………………………
(l) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizotajwa kwenye mabano Alama 3
i) Zindua (kutendata)- ----------------------------------------
ii) Pika (kutendesha)- ----------------------------------------
iii) Jenga (kutendua)- ----------------------------------------
(m) Unda nomino mbili kutokana na kitenzi –ita. Alama 2
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(n) Tunga sentensi ukitumia mifano ya aina za vivumishi vifuatavyo.
i) a-unganifu-
………………………………………………………………………………………………
ii) kirejeshi’O’-
………………………………………………………………………………………………
(o) Andika usemi ufuatao kwa usemi wa taarifa.
“Kefule! Mtoto huyu ni kaidi kama kirongwe. Hamheshimu babake! ”. Alisema Mzee Selele.
Alama 3
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
ISIMU JAMII:
Jadili dhima ya lugha katika jamii Alama 10
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
More Question Papers