Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kericho District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Kericho District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



JINA: ……………………………………………………........……….. NAMBARI: ......……………
SHULE: ...………………………………………………………………………………………….
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI/AGOSTI 2007
MUDA: SAA 2 ½
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
KERICHO
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI 2007
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali yote.
 Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika karatasi hii ya maswali.
 Karatasi hii ina kurasa kumi na mbili zilizopigwa chapa. Hakikisha kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Mzawa alikuwa mziwanda miongoni mwa ndugu zake wanne. Alipopigwa darubini, alionekana kuwa
mwanagenzi ambaye falau angemakinika angefikia upeo wa ufanisi masomoni kwa kuwa na vipawa
adimu vilivyofaa kuchochewa, kufukutwa, kurandiwa na kapigwa msasa. Nia ingekuwepo njia
ingepatikana. Wala hakuwa peke yake. Kulikuwa na wengi kama yeye. Na kisiki kilichomkingamia kilikuwa kipi? Kisiki kilichokuwepo kilikuwa kwamba licha ya kuwa katika kidato cha tatu na mwenye umri wa miaka yapata kumi na sita, alikuwa mfano wa ajabu ya shingo kukataa kulala chini, hakukomaa.
Na mtu ataitwa mtu vipi bila kukomaa? Wenzake darasani walimwita ‘toto kuu’ kwa kuwa japo
alionekana katutumka, tena mlingoti, alidinda kukaramka. Nao utu mzima hufunzwa katika taasisi gani?
Jawabu la swali hili lingalipatikana lingalimfaa sana Mzawa.
Na usidhani wasiokomaa ni waziwando tu, hata vifunguamimba na wanuna wao wote waweza kukomaa kutegemea misukumo, ari na mazingira yaliyo karibu nao. Mtoto azaliwapo, bongo lake huwa ombwe tupu na chochote kiingiacho humo huwa kama kinachoandikwa kwa wino usiofutika, hunata kama gundi.
Ukomavu huanzia hapa na mzazi akifanya waa katika maneno na vitendo afanyavyo kwa mtoto, huenda akachangia kwa kutokomaa kwake.
Mzawa hakuwa na umbu. Hii ilionyesha kuwa, kwa kuwa wazaziwe walikuwa wamejikopoa wana wanne wa jinsia moja, walimngojea mwana wa jinsia tofauti kwa hamu na ghamu. Si ajabu kuwa pindi alipozaliwa waliamua kufikisha uzazi hatima yake baada ya kupata walichokikamia. Msisimko uliowapata wazazi wa Mzawa ndio uliowapeleka kumtendekeza. Na ni kwa nini wazazi wengi huwa hawatosheki kamwe kwa kuwapata watoto wa jinsia moja tu? Si ajabu kuwaona wengine wakijifungua hata zaidi ya wana kumi, tena katika karne hii ya upangaji uzazi, lengo likiwa kusaka jinsia wasiyojaliwa kuipata. Sijui ni nani atakayeuganga ukongo huu.
Mama Mzawa alipofunga mkaja, walisitisha shughuli zao zote, wakawa wanasherehekea kwa
vigelegele, wakikipakata kitoto chao kwa zamu zilizorembeshwa kwa mashairi ya sifa za utanashati wa mwanao kwa mahadhi mbalimbali yaliyotiwa udamisi ajabu. Msisimko kama huu lazima uwepo huwatokea wampatao mwanao wa kwanza na hasa waliolimatia kujikopoa, hivyo baba mtu akaamua hataitwa tena jongoo asiyeukwea mtungi na mama hataitwa tasa. Hili huzua hatari ya kumdekeza mwana,naye atadeka milele kama huyu Mzawa.
Wazazi wa Mzawa hawakumkomaza. Kila kuchao walimwita ‘mtoto’, naye akawa mtoto wa kweli hata akafikia kidato cha tatu. Yasemwa kuwa Mzawa alilikamata ziwa la mamaye hata akafikia darasa la tano.
Haikuwa ajabu kumpata mamake akimsubiri njiani eti waziwa yanamwasha, naye mwanawe amekishika kilembe kadamnasi ya watu huko njiani, huku amepakatwa kiweoni. Kisha akishakinai kuama,angeelekwa kwa ubeleko hadi nyumbani alikomkuta babaye aliyemngojea kwa ilhamu na kwa nyimbo za kumuongoa hadi alale.
Hadi afike hapo alipokuwa sasa, Mzawa hakujua hata kunawa uso. Daima alioshwa na mvyele wake bila hata kuona soni kwa kuwa aliamini kuwa bado ni mtoto- mfikirie mtu aliyevunja ungo akioshwa na mamaye! Izara yafaa kumkumba, ila Mzawa alinyimwa soni. Ama ndiye aliyezua maneno, “waso haya wana mji wao?” Kama walisema avuliwaye nguo huchutama, ikawaje hata Mzawa avuliwa nguo na hata kukoshwa? Jitihada za nduguze kumkebehi na kumwambia ajitegemee na zile za majirani kuwasuta wazazi wa Mzawa ziliambulia patupu.
Hii sasa ni shule ya sita aliyosomea. Mzawa tangu aingize mguu wake katika shule ya upili. Kila aingiayo haimweki. Mara atasingizia kuwakosa wazazi wake, mara atalia eti chakula ni kigumu, atasema aona baridi akilala peke yake kwa kuzoea kulala mbavuni mwa wazae wake, homa ikimpata hulia kuwa hatunzwi, mwili haogi na hata anaposhikiwa shokoa na wenzake hajui kunawa hata uso! Huyaacha matongo yakiwamulika watu. Naye hunuka fee! Mahali alalamo ungedhani ni makao ya beberu kwa
mnuko. Harufu aliyotoa viatuni mwake ingesababisha pua kung’oka na mapafu kurudi. Alimradi Mzawa au “toto kuu,” kama alivyobatizwa, alikuwa zaidi ya mtoto. Na ingawa ni mapema sana huyawaza haya,je, Mzawa atakomaa, atengenee, apate ajira, apate mbawaze arukie au atakuwa kinda milele? Atapata kufu yake hatimaye?
Wako wapi hawa vifungamimba, wanuna au waziwanda waliokomaa wawakomaze wawakomaze
wasiokomaa? Ama wewe usomaye wasubiri kwenda likizoni kupakatwa na wazazio? Tabia zisizoafiki umri wa mtu huongonga, na wenye hekima walitufaa waliposema, “Mtoto akinyea kiweo hakikatwi,”
tutakiosha ‘kiweo’ chenyewe mtoto aadilishwe aadilike, aadibishwe aadibike.
MASWALI
(a) Yape makala haya anwani mwafaka. ( alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza vile wazazi wa mzawa walivyochangia katika tabia yake (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(c) Kwa nini shule mbalimbali hazikuweza kumweka Mzawa? (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(d) Kwa kuitolea mifano, taja aina nne ya tamathali za usemi zilizotumika katika taarifa uliyoisoma.
(alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika makala. (alama 3)
(i) Mziwanda –
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Kukaramuka –
……………………………………………………………………………………………………
(iii) Waa-
……………………………………………………………………………………………………
2. UFUPISHO
Soma makala yafuatayo kisha jibu maswali yanayofuata.
Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki
kila kitu; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa idhini maalum ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama. Hawa ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.
Kwa sababu ya bongo alizo nazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake
na ithibati ipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini;
amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.
Chambacho wavyele, akili nyingi huondoa maarifa. Binadamu amekuwa dubwana linalojenga
kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole. Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lilo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu
mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri, akamwambia binadamu, “haya,
twende kazi.”
Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji – taka ovyo hadi mitoni, maziwa na baharini na
matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambayo ni urithi aliopewa na
muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa
sumu na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Moshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta madhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’ bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima.
Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi
kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?
Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kiholela kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.
Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na
barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengine kuangamia kwa sababu ya
ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemichemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. Kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya basafu!
Maswali
(a) Bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya kwanza na ya pili. (maneno 50-60).
(alama 5 – alama1 ya Mtiririko).
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
Jibu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza mambo muhimu yaliyoshughulikiwa na mwandishi katika aya nne za mwisho.
(maneno 90-100) (alama 8- alama 1ya mtiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
Jibu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
3. Matumizi ya lugha
(a) Akifisha kifungu kifuatacho
mimi naona ni kazi ngumu nilimjibu si kazi ngumu ni mboga tu aliniambia huku akiniangalia kwa jicho la kunirai ( alama 4)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(b) Sahihisha sentensi zifuatazo:
(i) Kikombe ya mwalimu yetu ambacho kilichovunjika kilikuwa ndani ya kabatini.
(alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Mgeni alikodisha chumba cha kulala baada ya kuburudika na muziki.
(alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(c) Eleza maana ya sentensi hizi:
(i) Alitukimbia kabisa. ( alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Alitukimbilia kabisa (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(d) Andika katika usemi wa taarifa.
“Rejelea maelezo katika kitabu ili kuhakiki majibu yako.” Mwalimu alimwambia mwanafunzi.
(alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(e) Tumia nomino zifuatazo katika sentensi kama vivumishi.
(i) mlevi (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) huru (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(f) Onyesha fungu nomino na fungu tenzi katika sentensi ifuatayo:
Anapenda kusoma gazeti lenye maswala ya kijamii. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(g) Majina yafuatayo hupatikana katika ngeli gani?
(i) Chumvi (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Nyama (alama 1)
(h) Onyesha silabi inayawekwa shadda kwenye maneno haya:
(i) Karatasi (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(ii) Samahani (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(i) Onyesha chagizo na yambwa katika sentensi ifuatayo:
Mwanafunzi amesoma kitabu vizuri sana. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(j) Tumia –amba katika sentensi hii:
Ua limealo huwa limetiwa mbolea. ( alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(k) Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo:
(i) Barmasai huzungumza kilatini vizuri sana. (Tumia wakati usiodhihirika).
(alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(ii) Mtoto huyu hula chakula kingi sana. ( Kanusha katika hali ya ukubwa)
(alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(l) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi:
(i) Hakiki (alama 1)
……………………………………………………………………………………
(ii) Subiri (alama 1)
……………………………………………………………………………………
(iii) Sajili (alama 1)
……………………………………………………………………………………
(m) Andika sentensi ifuatayo katika wingi hali ya kukubali
Mgonjwa hasemi hajanywa dawa. ( alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(n) Tambua aina za maneno katika sentensi ifuatayo:
Walicheka sana walipoambiwa hadithi hiyo. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(o) Tunga sentensi ukitumia semi zifuatazo:
(i) Kula uhondo (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Regea parafujo za mwili (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(p) Tumia neno “mpaka” katika sentensi kueleza dhana ya:
(i) Wakati (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Mahali (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(iii) Kiwango (alama1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(q) Tunga sentensi ukitumia kivumishi cha pekee ‘o-ote’ katika ngeli ya u-u (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII
Ponda mali: Karibu! Wamama wang’are mali safi ambayo huwezi kupata popote
duniani.
Amina: Unauzaje hilo rinda?
Ponda mali: Bei ni kusikilizana, hatuwezi kukosana.
Amina: Nitakupaa shilling hamsini, naona ni mtumba.
Ponda mali: Mama hilo rinda ni original kutoka Marekani kwa meli.
Amina: Nitaongeza shilingi kumi basi.
Ponda mali: Ongeza kidogo, usiniue.
(a) (i) Hii ni sajili gani? (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Eleza sifa za sajili uliyotaja hapo juu (alama 4)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(b) Eleza sifa zozote tano za sajili ya kidini. (alama 5)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers